Samia Vs. Ndugai: Suluhisho ni Katiba Mpya. Wana CCM tuidai

Samia Vs. Ndugai: Suluhisho ni Katiba Mpya. Wana CCM tuidai

Mwingereza

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
1,115
Reaction score
2,771
Bila shaka, malumbano kati ya speaker na rais Samia imeonyesha wazi kwamba, hakuna uhuru wa mihimili yetu ya uongozi.

Mahakama haina uhuru wake, Bunge halina uhuru wake na Speaker pia ameonyesha udhaifu mkubwa sana kuomba msamaha pasipo na sababu ya msingi, na Rais Samia ameonyesha udhaifu wa kutokupenda kukosolewa na pia ameonyesha kwamba ana madaraka makubwa zaidi ya Ndugai.

Hakuna tena uwezo wa bunge kulisimamia serikali..... Suluhisho ni katiba mpya itakayoleta uhuru wa mihimili.
CCM nabici tupiganie katiba mpya. Hii ndio suluhisho !
 
Hio katiba mpya itaweza kuruhusu spika kumvimbia raisi ???
 
Ni jambo la ajabu sana kuona Spika anamuomba radhi Rais kisa ametoa maoni yenye mtizamo tofauti na Rais.

Nawaza tu hivi Rais naye angeweza kumuomba radhi Spika kwa style hii?
 
Bila shaka, malumbano kati ya speaker na rais Samia imeonyesha wazi kwamba, hakuna uhuru wa mihimili yetu ya uongozi. Mahakama haina uhuru wake, Bunge halina uhuru wake na Speaker pia ameonyesha udhaifu mkubwa sana kuomba msamaha pasipo na sababu ya msingi, na Rais Samia ameonyesha udhaifu wa kutokupenda kukosolewa na pia ameonyesha kwamba ana madaraka makubwa zaidi ya Ndugai.

Hakuna tena uwezo wa bunge kulisimamia serikali..... Suluhisho ni katiba mpya itakayoleta uhuru wa mihimili.
CCM nabici tupiganie katiba mpya. Hii ndio suluhisho !
Tuliwambia wakashupaza shingo. Leo Team Ndugai 0- katiba mpya team 10. Ndio kwanza dkk 15
 
Ni chuki zenu kwa mama Samia,

Mbona awamu ya magu hamkuona umuhimu wake?
Au magu aliifata Sana Katiba?

Huu upumbavu mmeufuga wenyewe awamu ilopita,
Sasa Tulieni dawa iwaingie.
 
Ni chuki zenu kwa mama Samia,

Mbona awamu ya magu hamkuona umuhimu wake?
Au magu aliifata Sana Katiba?

Huu upumbavu mmeufuga wenyewe awamu ilopita,
Sasa Tulieni dawa iwaingie.
Mkuu Deeppond kelele za katiba mpya zitakuwa mpya kwa wanaccm. Sisi wapinzani umekuwa ni wimbo wa siku zote miaka yote tangu 1992
 
Ndugai ni mtoto mdogo sna ,kwani unapinga
Akili ya kushindana na beberu hii. Ndugai mdogo sababu ya katiba bovu. Trump alisema jeshi la marekani liingie kuzuia maandamano na waziri wa ulinzi alikataa kwa sababu wanakatiba nzuri. Siyo kwetu katiba bovu hata rais akimtaka mke wa mtu utakuja kusema mume wa huyo mke mtoto mdogo sana.
 
Ni jambo la ajabu sana kuona Spika anamuomba radhi Rais kisa ametoa maoni yenye mtizamo tofauti na Rais.

Nawaza tu hivi Rais naye angeweza kumuomba radhi Spika kwa style hii?
Tatizo hii ni mihimili inayotegemeana tena inaongozwa na watu kutoka chama kimoja ndo maana umeona msamaha umetokea,kwani Job hajui ikulu ilipo au hazijui namba za raisi kwamba ampigie amueleze maoni yake kuhusu mikopo mpk aende kuropoka vile mbele ya camera?

Kule ni kuropoka wala si mtazamo.Una maana kuongea mambo ya nchi kuuzwa mbele ya umma ambao wengi wao fikra zao dhaifu!!!!

Kama Job hakuwa kwenye mission ni nini kumbe?
 
Asante Mungu kwa zawadi ya uhai.maana najionea mengi
 
Back
Top Bottom