Sammy Awami aeleza sababu ICC kumpiku Lissu tuzo ya Umoja wa Ulaya

Sammy Awami aeleza sababu ICC kumpiku Lissu tuzo ya Umoja wa Ulaya

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mwandishi wa habari wa BBC Swahili sammy awami amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizochangia Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutunukiwa Tuzo ya Sakharov ni mchango wake katika masuala yanayohusiana na hali inayoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Ameeleza kuwa msimamo wa ICC kuhusu masuala hayo ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kutunukiwa tuzo hiyo, akibainisha kuwa msimamo huo umeigharimu mahakama hiyo, ikiwemo kukabiliwa na vitisho kutoka Marekani.

Aidha, amemrejelea Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambaye amewahi kunukuliwa akisema kuwa atahakikisha ICC inasambaratika.

Chanzo: Samy Awami

 
Mambo ya kaninyang'anya Tonge mdomoni ndio haya sasa.
 
Hivi mnauhakika jamaa yupo cello kweli? Yaani cello halisi? Au anakula wali nyama kama sisi tu, lakini kuna mipaka hatakiwi kuvuka?
 
ICC wamepigwa vikwazo , hakuna walichofanikisha , hao jamaa muda wowote wanaweza kulipia na wasifanye chochote. Kwa taarifa yako , hata waafrika wameshaanza kuidharau ICC , wanaogopa NATO tu sio hiyo mahakama ya kinadharia.
 
Kuna wengine humu wamekuja kama wamekatwa vichwa na kusema sababu ya ICC kupewa ni Lissu kuwa mhaini!
 
Back
Top Bottom