Ni wapi kazi ya uandishi wa habari imekuwa death warranty? Kazi inayokupa guarantee ya kufa ni kuwa gaidi wa kujitoa mhanga tu.
Njoo hapa uwe mstari wa mbele ubebee vifaa hao waandishi mkauwawe pamoja, au wewe hufi?
Na hakuna mwanajeshi asiyeogopa kufa vitani, wala hakuna jeshi linalofanya combatants wake wafe. Ndio maana kuna medevac, bulletproofing, mine resistant vehicles, armour na sasa hadi UAVs na robotics zinatumika kupunguza casualties kwa jeshi husika. Kama kazi ya jeshi ni kufa vitani si wangekuwa wanaswagwa frontline kama ng'ombe.
Huwezi ona nchi inakombolewa kwa raia kuufyata, huku wakitengeneza makundi fulani ya kuwapambania na kufa kwa niaba yao, wao raia wenyewe wakiwa wanawakimbia wauwaji. Hata wanajeshi wenyewe unayosema ikitokea vita huwa wanafanya mobilization kwa raia kuongeza nguvu, sasa raia kama wewe ndio mtawaambia "msiogope vifo nyinyi ni wanajeshi, mimi siji kanipiganie"
Wanawake wa Uingereza kwa vile walizuiliwa kwenda frontline kwenye WW1 na WW2 basi walitengeneza milipuko viwandani ili kusudi wanaume waelekeze nguvu yote kwenye mapigano (mabomu mizinga na risasi nyingi zilitengenezwa na wanawake) wanasayansi hakuna kwenda vitani elekeza nguvu kwenye gunduzi za kivita, vijana wadogo wakawa observers na wanaripoti kila sighting ya adui.
View attachment 3497704
Sisi akina Australopithecus Africanus tiyari tumeunda makundi gani yafe kutupigania huku tumelaza matako ndani.