Samson Charles: Kwanini wanahabari (eti mnasema) tulionekana waoga?

Mkuu sawa tufanye angetoka , swali kwako je angetumia njia gani kuonesha Watanzania yanayoendelea ikiwa
1. internet ikiwa imezimwa
2.IPP media wamezuiwa na mamlaka kuto kutoa taarifa yoyote.
Atoke sasa hivi aende kwenye nyumba zenye misiba za watoto waliopigwa risasi atangaze habari zao.
 
Unalinganisha muandishi wa habari, mtu ambaye kazi yake aliyoichagua mwenyewe inamtaka atoke nje na mtu wa kawaida ambaye hajachagua kazi hiyo?

Wewe nawe ni muandishi wa habari?
Kwani wapi nimesema angetoka?

Unaelewa hoja yangu?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Yani unaelewa kusoma kwa attention to detail sio ku skim through bila kuelewa hoja?
Mwisho wa kunukuu
 
Kama hutaki kjfa kazini usichague kazi ya uandishi wa habari.

Unachagua uanajeshi halafu unaogopa kufa vitani?
Ni wapi kazi ya uandishi wa habari imekuwa death warranty? Kazi inayokupa guarantee ya kufa ni kuwa gaidi wa kujitoa mhanga tu.
Njoo hapa uwe mstari wa mbele ubebee vifaa hao waandishi mkauwawe pamoja, au wewe hufi?

Na hakuna mwanajeshi asiyeogopa kufa vitani, wala hakuna jeshi linalofanya combatants wake wafe. Ndio maana kuna medevac, bulletproofing, mine resistant vehicles, armour na sasa hadi UAVs na robotics zinatumika kupunguza casualties kwa jeshi husika. Kama kazi ya jeshi ni kufa vitani si wangekuwa wanaswagwa frontline kama ng'ombe.

Huwezi ona nchi inakombolewa kwa raia kuufyata, huku wakitengeneza makundi fulani ya kuwapambania na kufa kwa niaba yao, wao raia wenyewe wakiwa wanawakimbia wauwaji. Hata wanajeshi wenyewe unayosema ikitokea vita huwa wanafanya mobilization kwa raia kuongeza nguvu, sasa raia kama wewe ndio mtawaambia "msiogope vifo nyinyi ni wanajeshi, mimi siji kanipiganie"

Wanawake wa Uingereza kwa vile walizuiliwa kwenda frontline kwenye WW1 na WW2 basi walitengeneza milipuko viwandani ili kusudi wanaume waelekeze nguvu yote kwenye mapigano (mabomu mizinga na risasi nyingi zilitengenezwa na wanawake) wanasayansi hakuna kwenda vitani elekeza nguvu kwenye gunduzi za kivita, vijana wadogo wakawa observers na wanaripoti kila sighting ya adui.

Sisi akina Australopithecus Africanus tiyari tumeunda makundi gani yafe kutupigania huku tumelaza matako ndani.
 
Hakika leo umeongea kitu cha maana sana, ndio maana wakati wa vita vya Gaza waandishi nguli wote walikimbilia huko, na hata penye vita ndipo mwanajeshi hukumbilia na si kujificha pangoni kwa mujibu wa kazi yake, sasa yeye anataka kusemaje wakati kazi yake ndiyo inayomdai afanye hivyo?
 
Ni wapi nimesema kazi ya uandishi wa habari ni death warranty?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Kuna jamaa mmoja akiitwa Christopher Hitchens.

Alikuwa kila siku akisoma habari za vita hapendi zinavyoandikwa.

Anaona makosa, anaona kasumba, anaona haziandikwi anavyotaka yeye.

Akasema huu ujinga, nitaenda mwenyewe huko vitani nikaandike mwenyewe.

Akaja kuwa muandiahi mzuri sana wa habari za vita na vitabu vingi.

Kuna waandishi wa habari za vita kukiwa hakuna vita wanaona maisha hayafai kuishi.

Wao wanataka kuingia kwenye sekeseke waandike habari za vita.

Sisi tuna waandishi wanajilinganisha na raia.
 
Kiranga he is totally wrong na hataki kukubali kuwa kakosea nahisi kuna shida mahala, Hata hii post hatoweza kuielewa
 
Hii ndiyo shida ya Watanzania, kuaminishwa Tz ni nchi ya amani hivyo tupende vyenye amani, wakati uhalisia haupo hivyo kabisa.
 
Hii ndiyo shida ya Watanzania, kuaminishwa Tz ni nchi ya amani hivyo tupende vyenye amani, wakati uhalisia haupo hivyo kabisa.
Hiyo habari ya Tanzania ni nchi ya amani mimi nilikuwa naikataa, nikiita "the myth of Tanzanian exceptionalism".

Nilikuwa nasema jamani msione kuwa mko special sana kuna siku Tanzania panaweza kuchafuka mkashangaa wenyewe.

Lakini hata mimi sikutegemea mambo yaharibike so much so fast hivi.
 
Pamoja sana, huu si wakati wa kulilishwa maneno matupu kama mistari ya kwenye bibilia.
 
Najua.

Ukichoelewa ni nini mpaka sasa?

Weka hapa tuchambue kwa hesabu za mantiki za Truth Tabke.

Wewe unajua Truth Table ni nini?
Suala la wewe kutaka waandishi wa habari wafe kisa walichagua kazi unayoita ya kifo halijaisha, tiyari unataka tena tubishane Truth Table? Uko sikutaki.

Waandishi machawa tu wanapigwa risasi kisa wametoka nje kuchungulia kwa macho tu, sembuse hao wenye vifaa vya kazi na wako neutral.

Mfano mwandishi wa Clouds ameuwawa akiwa nyumbani, tumechukua hatua gani kama raia?
 
Wapi nimetaka waandishi wa habari wafe?

Hivi unaelewa hata hoja yangu ni nini?

Unajua kusoma kwa ufahamu ukaelewa hoja yangu ni ipi au unakuja na kusoma kitu halafu ukanipachika maana iliyo kichwani mwako ambayo mimi sijaandika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…