Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,240
SΛMSUNG ni moja kati ya brand kubwa duniani katika uzalishaji na usambazaji wa vifaa vya kielektroniki.
SΛMSUNG ilianza kama duka la kuuza mbogamboga na ilianza kwa mtaji mdogo sana, ilikuwa inauza vyakula kama vile samaki wa kukausha na tambi. Ilianzishwa siku kama ya leo - March 1 mwaka 1938 na Lee Byung-chul.
Baada ya vita vya Korea ikakuza biashara yake katika sufu, bidhaa za jumla na miaka ya 1960’s ikaingia rasmi katika biashara ya vifaa vya umeme baada ya kuona soko la teknolojia likianza kwa kasi.
𝘔𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘺𝘢 𝘯𝘦𝘯𝘰 SΛMSUNG 𝘯𝘪 “𝘕𝘺𝘰𝘵𝘢 𝘛𝘢𝘵𝘶”. 𝘓𝘦𝘦 𝘉𝘺𝘶𝘯𝘨-𝘤𝘩𝘶𝘭𝘭 𝘢𝘭𝘪𝘴𝘦𝘮𝘢 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘺𝘢𝘬𝘦 𝘯𝘪 “𝘣𝘳𝘢𝘯𝘥 𝘯𝘻𝘶𝘳𝘪 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘣𝘸𝘢 𝘬𝘢𝘮𝘢 𝘯𝘺𝘰𝘵𝘢”.
SΛMSUNG ni moja kati ya brand kumi kubwa ya teknolojia duniani; ni mzalishaji mkubwa wa chip za vifaa vya kielektroniki, screen, DRAM, Flash, Hard Disks, vifaa vya majumbani, vifaa vya mawasiliano na kamera.
SΛMSUNG ndio kampuni iliyojenga jengo refu duniani la Burj Khalifa!