Samweli Shafiihuna Daniel Nujoma-"Sam Nujona"

Samweli Shafiihuna Daniel Nujoma-"Sam Nujona"

njundelekajo

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
310
Reaction score
227
SAMWELI DANIEL SHAFIIHUNA NUJONA- "SAM NUJONA"

Barabara na mitaa mingi nchuni hasa Dar-es-Salam "zimebatizwa"majina ya watu mashuhuri nyakati za ukombozi wa kupigania uhuru wa Afrika mfano Bibi Titi,Kawawa road,Kwameh Nkuruma nk.

Barabara inayotoka Mwenge kuanzia kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo inaitwa bara bara ya Sam Nujoma(Sam Nujoma road).Hili ni jina lililotelewa kuenzi harakati za mpigania huru na rais wa kwanza wa Namibia ,Samweli Nujoma.

Miaka ya 1960 sehemu kubwa ya bara la Afrika lili kua kwenye joto kubwa la harakati za Uhuru.Harakati hizo zilizotapakaa karibu pembe zote za bara hili likazaa majina makubwa yaliyoacha alama katika bara hili kama Muhammad Anwar El Saadat,Kwame Nkuruma,Julius Kambarage,Steven Biko,Abraham Tito,Samora Machel,Patrice Lumumba,Joseph Kasavubu,Andimba Toivo ya Toivo na wengine wengi akiwemo Samweli Daniel Shafiihuna Nujoma .

Nujoma aliyezaliwa Mei 12,1929 kijijini kwao Ongandjera,mji wa Etunda mkoa wa Omusat kaskazini Magharibi mwa Namibia. Eneo alilozaliwa linaitwa "Ovambo" likimaanisha ardhi.Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 11 wa mkulima na mfugaji Daniel Utoni Nujoma na kwa mkewe Helvi Mpingana Kondombolo.Alisoma shule ya Okahao mpaka darasa la sita kwa wakati huo ilikua elimu ya juu sana.

Jina lake la "Shafiihuna"ambalo si maarufu sana kama Nujoma lina maana ya wakati wa matatizo,linakaribiana na majina wanaopewa watoto wa kitanzania kama "Shida",Matatizo".Jina hili alipewa kutokana na wakati anazaliwa nchini humo kilikua ni kipindi ambacho nchi hiyo ilikua chini kipindi cha ukoloni mpya wa Uingireza toka kwa Mjerumani baada ya vita vya kwanza vya dunia.

Mwaka 1949 Nujoma alikwenda kuishi Windhoek kwa mjomba wake Hiskia Kondombolo.Akiwa Windhoek alianza kufanya kazi katika shirika la reli la Afrika ya kusini (South African Railway-SAR).Alifanya kazi mchana usiku anaingia darasani kusoma St .Barnabas hapo hapo Windhoek.

Mwaka 1957 alifukuzwa kazini kutokana na harakati zake za kupigania haki za wafanyakazi wa shirika la reli alilokua akifanyika kazi lakini pia kulichangiwa na kustukiwa kwa mpango wake wa kutaka kuanzisha umoja wa wafanyakazi wa reli

Baada ya kufukuzwa kazi, alijitumbukiza rasmi kwenye siasa, kwa kushirikiana na Chief Hosea Kutako,Samuel Witbooi,Theophilus Hamutumbangela, Toivo ya Toivo na wengine walianzisha chama cha Ovamboland People's Congres .

Mwaka mwaka 1959 walianzisha chama kingine tena cha Ovamboland People's Organization na kuchaguliwa kua kiongozi wa chama hiko, mwaka 1960 alishiriki kuanzisha chama kilichoipa uhuru nchi hiyo cha Ukombozi wa Umma wa Afrika ya kusini Magharibi,SWAPO na kuchaguliwa kua mwenyekiti wa chama hiko.Akiwa kiongozi wa SWAPO alifanikisha Namibia kujitenga kutoka Afrika kusini na kua nchi huru mwaka 1990.

Nujoma aliyeungwa mkono na mataifa mbalimbali pamoja taaisisi kikiwemo chama cha kikomunisti cha china na jeshi la ukombozi wa umma wa china chini ya Mao Zedong na Bw.Zhou Enlai.

Alifika Tanganyika mara ya kwanza mwaka 1960 akiwakimbia wakoloni.
Alitoroka toka Namibia hadi Tanganyika kutafuta hifadhi baada ya kushtakiwa kusababisha vurugu.Safari hii iliyomgharimu zaidi ya siku sitini(miezi miwili) ilikua ni jumla ya mateso mengi na shida, akitumia usafiri wa ndege,treni,magari na hata kwa miguu akipita Botwsana ya leo(Zamani Bechuana land),Zimbabwe ya leo(zamani Rhodesia ya kusini),kisha Zambia ya leo(zamani Rhodesi ya kaskazini,Kongo Tanganyika

Akiwa Tanganyika watu wa TANU walimficha mjini Mbeya ili asikamatwe,kisha alisafirishwa kwa siri hadi Dar -es-Salaam alipokutana na Nyerere.Akiwa Dar es-Salaam kwa msaada wa Nyerere alipata nafasi ya kuzungumza na kamati maalum ya umoja wa mataifa New York nchini Marekani.

Ilipoundwa kamati ya ukombozi wa ilikua umoja wa nchi huru Afrika (OAU)mwaka 1963,Tanzania ikawa kituo cha wapigania Uhuru na mafunzo ya kijeshi. Alikua miongoni mwa wapigania uhuru waliojiunga na jeshi lilioweka kambi Kongwa mkoani Dodoma.Akiwa Kongwa alijifunza tamaduni mbali mbali za kabila la kigogo ikiwemo lugha ya kabila hilo.

Agusti 26, 1966 Nujoma alifanikiwa kuingiza mzigo wa kwanza wa silaha Namibia zilizotoka Algeria kupitia Misri,Sudan,Tanzania Zambia na kisha kuingiza nchini humo katika mji wa Uukwaluudhi mkoa wa Umusati na kua mwanzo rasmi wa mapigano ya ukombozi wa nchi hiyo.Tukio hilo la kuingiza silaha kwa mara ya kwanza nchini humo ni moja ya kumbukumbu za kihistoria ikiwa imepewa heshma ya peake na kubatizwa rasmi kama siku ya mashujaa (Heros'Day Agust 26).

Mapigano yalianza baada ya askari wa kikoloni kuwavamia bywanaharakati wa SWAPO siku hiyohiyo silaha zilipoingia nchini humo wakiwa kwenye kambi yao ya Omugulugwombashe. Yalidumu kwa miaka 25 hadi mwaka 1971 Nujoma alipohutubia baraza kuu la Usalama la Umoja wa mataifa mjini New York Marekani.Kupitia hotuba hiyo Swapo ilitambulika rasmi na baraza hilo na ukawa mwisho wa vita hivyo ingawa hakurudi nchini kwake.

September 1989 alirudi nchini Namibia rasmi baada ya miaka 29 ya kuishi uhamishoni.Na machi 21 alitangazwa rasmi kua rais wa nchi hiyo kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini humo.Nujoma alistaafu rasmi urasi wa Namibia machi 21,2005 na limpisha rais Hifikepunye Pohamba na kisha kuachia nafasi yake ya uongozi wa chama cha SWAPO Novemba 30,2007

Noel Nguzo.R.
 
Uzi mzuuuriii wachangiaji wachache watanzania bwana wajinga Sana sasa anzisha uzi wa simba na yanga au kichuya ndio utawaona
 
Mimi maishani sijawahi mkubali mandela

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina hakika sana, ila nahisi kwa sasa hata kwake wengi watakuwa hawamkubali kama zamani, hii sera ya kusamehe na kuleta usawa kwa watu walio wakandamiza kwa muda mrefu, kwa sasa haikubaliki. Nahisi moja ya sababu ya kutorudiana na mkewe ilikua hii ya kuwasamehe weupe, huku wakiachiwa fursa zote na neema za nchi na wazawa kuachwa mikono mitupu. Sasa kumekuwa na uhasama baina ya weupe na wazawa, ambao wachache miaka hiyo walishauona.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom