Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samweli Sitta ameanza vibaya kazi yake siku ya kwanza kwa kukiuka kanuni za Bunge la katiba.
Sitta alitangaza kwamba Jaji Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba mpya kabla ya Rais Kikwete kuhutubia, jambo ambalo ni uvunjaji wa kanuni za Bunge hilo, maana kanuni inasema wazi Rais Kikwete atahutubia Bunge hilo kabla ya Warioba kuwasilisha rasimu hiyo.
Tundu Lisu mjumbe wa Bunge hilo akitaka mwongozo alimtahadharisha Sitta juu ya ukiukwaji huo, na kwamba sababu ya kuwekwa sheria hiyo ni kuondoa kile ambacho kingeonekana Kikwete kumjibu Mwenyekiti anayewasilisha mswada, hivyo ilikubaliwa Rais ahutubie kwanza Bunge ndipo mwenyekiti Warioba awasilishe rasimu.
Hali halisi inaonekana CCM wanaendelea kucheza faulo kwenye Bunge hili.

