Samweli Sitta aanza kazi kwa kukiuka kanuni za bunge la katiba

Ni mara Mia moja Pandu Kificho angakaa kwenye kiti hichi hakika angefanya makubwa kwa hekima na Busara zake ila Sitta anaendesha Bunge kibabe akifikiri ni kile kipindi chake ambacho wabunge lile lisilojitambua.......Leo hii ajue kuna watu wanasoma kanuni na kulala nazonhivyo kuwaburuza hakutakuwa na mwisho mzuri.

mchezaji namba 6 ni mpummbaaavu kabisa, anahitaji super sub ya kuaminika
 
Mbona kitu kidogo sana hiki jamani??? Alipitiwa tu kidogo!!!! Mwacheni mzee wa standards and speed aliongoze bunge hili ili mwisho wa siku tupate katiba nzuri Kwa manufaa ya taifa letu.
 
hadi nimecheka....................kweli kazi ipo ila naamini pale Bungeni pataeleweka tu

Kusipotokea mtifuano bunge movie kati ya wiki hii na wiki ijayo basi tutavuka salama kwa mtindo wa funika kombe mwanaharamu apite.
 
Mpwa usibishane nao
Povu lote la nini. Jadili mada iliyo letwa, kwa kawaida asiye na upeo mkubwa katika kujadili mada huja kwa speed ya mipasho.

Kwa taarifa yako mie si mponea dezo za kisiasa, naponea jasho langu, na katu siwezi kushinda majukwaani nikishupaza mishipa kama sina akili timamu, bora nikalime tuta la mbatata na hakuna mwenye kunisuta au kuja kunikagua ilivyo mfanyiwavyo vinavyotokana na dezo.
 
Ndugu Wana-Jamii,

Nadhani tunachanganya mambo.

Kama Sita amekiuka kanuni hilo ni kosa. Hakuna sababu watu watuimie mwezi mzima kuandaa kanuni halafu siku ya kwanza zinavunjwa tena na Mwenyekiti.

Hata hivyo sikubaliani a wanaosema kuwa ni lazima Warioba awasilishe kwanza kama kwamba kuna Mtanzania aneyefuatilia mchakato wa Katiba ambaye hadi leo hana rasimu hiyo. Kama yupo tena ni Mjumbe wa Bunge la Katiba basi umakini wake kwenye kazi aliyotumwa au tunayomtegemea kuifanya unatia shaka.

Sambamba na hilo sidhani kama Rais atataka kumjibu Waroba (Au Kamati ya kukusanya maoni) au kushawishi hoja yake atashindwa eti kwa sababu hajui kilichoma ndani ya Rasimu mpaka Warioba aseme. Tunasahau kuwa Rais alishakabidhiwa rasimu na yeye na Watanzania wote wanaofatilia mchakato huu tunajua Warioba atasema nini kwa kiasi kikubwa
 
Kipi kina nguvu mkuu; kanuni (za sheria) au logic?

Mkuu nakubaliana na wewe kuwa kanuni zina nguvu lakini lazima busara na logic zitumike pale kanuni zinakinzana na hali halisi. Otherwise, kama kungekuwa na muda wa kutosha wangebadili kanuni.
 
Ilikuwaje hao 'wengi' wakapitisha kanuni zinazokinzana kiasi cha kuonekana mbovu hata kabla hazijaanza kutumika? Huoni ni kutokana na uzembe wa kuitikia "Ndioooooo"? Hawajajifunza kwa kosa la kupitisha sheria ya kodi ya line za simu mwaka jana?
 
View attachment 145334 Sitta ajue bunge la sasa lina wanasheria mahiri View attachment 145335

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samweli Sitta ameanza vibaya kazi yake siku ya kwanza kwa kukiuka kanuni za Bunge la katiba.

Sitta alitangaza kwamba Jaji Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba mpya kabla ya Rais Kikwete kuhutubia, jambo ambalo ni uvunjaji wa kanuni za Bunge hilo, maana kanuni inasema wazi Rais Kikwete atahutubia Bunge hilo kabla ya Warioba kuwasilisha rasimu hiyo.

Tundu Lisu mjumbe wa Bunge hilo akitaka mwongozo alimtahadharisha Sitta juu ya ukiukwaji huo, na kwamba sababu ya kuwekwa sheria hiyo ni kuondoa kile ambacho kingeonekana Kikwete kumjibu Mwenyekiti anayewasilisha mswada, hivyo ilikubaliwa Rais ahutubie kwanza Bunge ndipo mwenyekiti Warioba awasilishe rasimu.

Hali halisi inaonekana CCM wanaendelea kucheza faulo kwenye Bunge hili.

Amekiuka kanuni gani? Umezisoma hizo kanuni wewe au unakuja tu hapa kubwabwaja ili upotoshe watu kwa malengo yako unayoyajua!!! Maelezo aliyotoa SITTA ni ya msingi na Kanuni ya 85 inaruhusu hoja kwa ajili ya kutengua kanuni yoyote kwa madhumuni fulani. Hoja ya kutenguliwa Kanuni ya 7 ilitolewa ili Rais azindue Bunge Ijumaa kwakua ana ratiba zingine. Hivyo ni busara tu kwamba Warioba awasilishe rasimu hii leo kama anavyotakiwa na sheria ya mabadiliko ya katiba then aondoke zake!!!! Wewe na wenzako mna wasiwasi gani Mkuu wa Nchi [RAIS] akizindua Bunge baada ya uwasilishaji wa Warioba???? Acha UPOTOSHAJI. SHAME ON YOU!!!
 
Ungekuwa unajua sheria hizo kuliko mimi uneleta hoja zako hapa kutetea hilo badala ya kuanza na mashambulizi ya matusi, sina muda wa kubishana na watu wa aina yako kwa vile hamko kwa masilahi ya taifa bali ya kikundi cha viongozi
 
Hapo kwenye bold ---Hatuko hapa kubishana nani anajua sheria zaidi kati yako na mimi kwakua hata wewe hujui mimi ni nani na cv yangu na hakuna haja ya kujua hayo maana hayatakusaidia lolote. Aidha, sihitaji kujua una elimu gani ya sheria ila ninachoangalia ni hoja yako. Nikuambie tu kwa ufupi kwamba mimi nina shahada ya uzamivu katika sheria kutoka chuo kikuu cha HUMBOLDT kilichopo Berlin Ujerumani. Katika andiko lako hapakua na hoja ya msingi na kama umesoma kanuni za bunge maalum kwa ufasaha basi ungeelewa kwamba SITTA hajakiuka KANUNI YOYOTE. Nakusihi tu kwamba si afya kupotosha watu hapa hasa katika kipindi hichi muhimu ambacho taifa letu liko katika mchakato wa mabadiliko ya katiba. Tanzania Kwanza, Tanzania Milele!!!!!!!!!!!!
 
NEVIOT, kama ni kweli umesoma sheria kama unavyodai hungeandika point ya kipuuzi kama ulivyoandika katika jibu lako la awali, eti;
...hoja ya kutenguliwa Kanuni ya 7 ilitolewa ili Rais azindue Bunge Ijumaa kwakua ana ratiba zingine!
My God, are you serious? Unaelewa jukumu la bunge la Katiba? Hizo ratiba zingine anazoweza kuwa nazo Raisi zikawa na umuhimu kupita kuzindua Bunge la Katiba ni zipi? Kwa mtu anayedai eti kasomea sheria, this logic is more than ridiculous...it is stupid. Je ilitokea ghafla tu akatakiwa kuzindua hilo Bunge au ni jambo limepangwa kwa muda mrefu, hii hasa ndio thinking ya usanii/uswahili uliotufikisha Watanzania hapa tulipo, it is pitiful...na nakuapia kitu kama hiki kinaweza kutokea tu katika nchi yenye watu kama NEVIOT, anayesemekana kusomea sheria chuo kikuu cha HUMBOLDT Ujerumani. Samahani mods kwa lugha kali lakini ni vigumu kwangu kuuita ujinga werevu.
 
Last edited by a moderator:
Kusipotokea mtifuano bunge movie kati ya wiki hii na wiki ijayo basi tutavuka salama kwa mtindo wa funika kombe mwanaharamu apite.

Skype hayo ni ya kweli.......Sitta aacheza sana na akili za watu
 
Amekiuka kanuni gani? Umezisoma hizo kanuni wewe au unakuja tu hapa kubwabwaja ili upotoshe watu kwa malengo yako unayoyajua!!! Maelezo aliyotoa SITTA ni ya msingi na Kanuni ya 85 inaruhusu hoja kwa ajili ya kutengua kanuni yoyote kwa madhumuni fulani. Hoja ya kutenguliwa Kanuni ya 7 ilitolewa ili Rais azindue Bunge Ijumaa kwakua ana ratiba zingine. Hivyo ni busara tu kwamba Warioba awasilishe rasimu hii leo kama anavyotakiwa na sheria ya mabadiliko ya katiba then aondoke zake!!!! Wewe na wenzako mna wasiwasi gani Mkuu wa Nchi [RAIS] akizindua Bunge baada ya uwasilishaji wa Warioba???? Acha UPOTOSHAJI. SHAME ON YOU!!!

Shame on You: kwa kujifanya uajua kanuni
 
Amekiuka kanuni gani? Umezisoma hizo kanuni wewe au unakuja tu hapa kubwabwaja ili upotoshe watu kwa malengo yako unayoyajua!!! Maelezo aliyotoa SITTA ni ya msingi na Kanuni ya 85 inaruhusu hoja kwa ajili ya kutengua kanuni yoyote kwa
madhumuni fulani. Hoja ya kutenguliwa Kanuni ya 7 ilitolewa ili Rais azindue Bunge Ijumaa kwakua ana ratiba zingine. Hivyo ni busara tu kwamba Warioba awasilishe rasimu hii leo kama anavyotakiwa na sheria ya mabadiliko ya katiba then aondoke zake!!!! Wewe na wenzako mna wasiwasi gani Mkuu wa Nchi [RAIS] akizindua Bunge baada ya uwasilishaji wa Warioba???? Acha UPOTOSHAJI. SHAME ON YOU!!!

We acha ujinga rais hata awe na shughuli gani angehairisha katiba ndio kila kitu asilete ujanja ujanja wake au anataka kwenda malaysia kujiunga na rescue team
 
NEVIOT, kama ni kweli umesoma sheria kama unavyodai hungeandika point ya kipuuzi kama ulivyoandika katika jibu lako la awali, eti;

My God, are you serious? Unaelewa jukumu la bunge la Katiba? Hizo ratiba zingine anazoweza kuwa nazo Raisi zikawa na umuhimu kupita kuzindua Bunge la Katiba ni zipi? Kwa mtu anayedai eti kasomea sheria, this logic is more than ridiculous...it is stupid. Je ilitokea ghafla tu akatakiwa kuzindua hilo Bunge au ni jambo limepangwa kwa muda mrefu, hii hasa ndio thinking ya usanii/uswahili uliotufikisha Watanzania hapa tulipo, it is pitiful...na nakuapia kitu kama hiki kinaweza kutokea tu katika nchi yenye watu kama NEVIOT, anayesemekana kusomea sheria chuo kikuu cha HUMBOLDT Ujerumani. Samahani mods kwa lugha kali lakini ni vigumu kwangu kuuita ujinga werevu.

Kafka nakuunga mkono eti ana shughuli nyingine ipi ina umuhimi kuliko katiba watu wenye akili wameweka akili zao mfukoni sasa wanafikiria kwa makalio
 
Last edited by a moderator:
Mambo mengine ni suala la logic, huwezi kuzindua bunge wakati watakachojadili hapo hawanacho.

siyo kila mahali unaposeama logic itumike, kinachotumika ni logic. Logic ni kitu kitukufu sana na kinapotumika hakunaga maswali ya kijinga. Kwa hiyo wakati rais anaunda bunge hilo alikuwa hajui anaunda bunge la kwenda kufanya nini? Je walipokuwa wanaapa hawakujua wanaapa kwa kazi gani ? Je wakati uchaguzi unapokamilika na rais kuapishwa anafupofuguaga bunge huwa kuna muswada au agenda mezani? Ni Logic gani bwana unayozungumza! Sasa tuangalie logic yako, Sheria inamtaka Mwenyekiti wa tume ya katiba kuwasilisha rasimu kwenye bunge maalumu la katiba. Ili liwe tayari ni bunge maalumu kimsingi linapaswa liwe limezinduliwa rasmi na kuwa bunge maalumu la katiba. Uzinduzi wa bunge hilo unapaswa kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mantiki hiyo bunge hilo la katiba litakuwa bunge maalum baada ya kuzinduliwa. Kama Warioba anawasilisha rasimu katika bunge ambalo halijazinduliwa ina maana anavunja kanuni na sheria kwa kuwasilisha rasimu kwenye kundi la watu waliokusanyika na ambao hawajaundwa kuwa bunge rasmi la katiba. Hapo unaweza kuona kuwa hata katika kuwaza kilogic Warioba anapswa kuwasilisha rasimu hiyo kwenye bunge baada ya bunge hilo kuzinduliwa rasmi na Rais.
 
Amekiuka kanuni gani? Umezisoma hizo kanuni wewe au unakuja tu hapa kubwabwaja ili upotoshe watu kwa malengo yako unayoyajua!!! Maelezo aliyotoa SITTA ni ya msingi na Kanuni ya 85 inaruhusu hoja kwa ajili ya kutengua kanuni yoyote kwa madhumuni fulani. Hoja ya kutenguliwa Kanuni ya 7 ilitolewa ili Rais azindue Bunge Ijumaa kwakua ana ratiba zingine. Hivyo ni busara tu kwamba Warioba awasilishe rasimu hii leo kama anavyotakiwa na sheria ya mabadiliko ya katiba then aondoke zake!!!! Wewe na wenzako mna wasiwasi gani Mkuu wa Nchi [RAIS] akizindua Bunge baada ya uwasilishaji wa Warioba???? Acha UPOTOSHAJI. SHAME ON YOU!!!

Nevioti kama wewe ni msomi wa sheria tafadhali jibu swali kwa kufuta kanuni za kisheria. Nadhani mie ambaye sijasoma kabisa sheria na wala sijui sheria ninadhani ungepaswa kwanza kunukuu hiyo kanuni ya 85 uonyeshe inampa mwenyekiti mamlaka kiasi gani. Pili unukuu kanuni ya saba na vipengele vyake ndipo uonyeshe jinsi kanuni ya 85 ilivyotumika kutengeua kanuni ya 7 na vipengele vyake. Baada ya hapo ndipo uonyeshe jinsi hoja ya Samwel Sita iliyoenea au kutokuenea kwa hoja husika. Lakini unapojibu hoja kama muuzaji wa nyanya na kudai kuwa unayo CV nzito ya shahada ya uzamili hapo unanipa kutilia wasiwasi elimu yako hiyo.
 
Back
Top Bottom