Sanamu la Rais wa zamani wa Ghana Akufo Addo labomolewa, majigambo na kujitukuza zatajwa kama sababu

Sanamu la Rais wa zamani wa Ghana Akufo Addo labomolewa, majigambo na kujitukuza zatajwa kama sababu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Huko nchini Ghana sanamu ya kumbukumbu ya Rais wa zamani wa Ghana, Nana Akufo-Addo, iliyojengwa mwishoni mwa mwaka jana, imeangushwa.

Wakati Akufo-Addo akizindua sanamu hilo Januari (11) katika Mkoa wa Magharibi alikumbana na mapokezi mabaya sana kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakikashifu kuwa ni majigambo

Sanamu hilo lilitengenezwa kwa ajili ya kutambua mchango wa maendeleo uliotekelezwa katika kipindi cha uongozi wake.

Hata hivyo, video zilizosambaa mtandaoni siku ya Jumatatu zilionyesha sanamu hilo likiwa limeharibika, na kichwa chake kikiwa kimeporomoka baada ya watu kulibomoa

Soma pia: Raia Ghana walalamika baada ya Rais wao Nana Akufo-addo kuzindua sanamu yake ilinokshiwa na rangi ya shaba!

Kufikia sasa Polisi bado hawajaweka wazi sababu gani hasa zilizochagiza kubomoa sanamu hilo lakini watu wengi kupitia mitandao ya kijamii wamedokeza kutokupendezwa na kitendo cha kujengwa kwa sanamu hilo


Akufo 1.png
William Nana Akuffo Ado ni nani?

William Nana Addo Dankwa Akufo-Addo ni mwanasiasa kutoka Ghana ambaye alihudumu kama rais wa 13 wa Ghana kutoka 2017 hadi 2025.

Aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia 2001 hadi 2003 na pia Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 2003 hadi 2007 chini ya utawala wa rais John Kufuor.

Katika uchaguzi wa 2016, alichaguliwa tena kuwa mgombea wa urais wa NPP na alishinda kwa kura nyingi dhidi ya rais aliyekuwepo, John Dramani Mahama, kwa kupata asilimia 53.85 ya kura, na hivyo kuwa mgombea wa upinzani wa kwanza kushinda uchaguzi wa urais nchini Ghana

==============================================

The controversial statue of Ghana’s immediate past President, Nana Akufo-Addo, has been destroyed, sparking a wave of reactions across the country.

The statue, unveiled in November in the Western Region to honor Akufo-Addo’s development initiatives, had faced heavy criticism since its installation.

Many citizens and critics derided the move as an act of “self-glorification” amid widespread economic challenges.

Images circulating in the media on Monday showed the statue in ruins, its severed head lying on the ground. The torso was also destroyed, leaving behind only a damaged pedestal.

The motives behind the destruction remain unclear, with police yet to comment on the incident.

This is not the first time the statue had been targeted; one of its legs was partially vandalized last month. Despite local authorities pledging to repair it, the statue has now been completely reduced to rubbl

Source: Maravipost
 
Sanamu la Rais wa Ghana aliyemaliza muda wake Nana Akufo Addo limebomolewa ikiwa ni siku chache tangu kuapishwa kwa Rais mpya John Mahama.
Uzinduzi wa sanamu hilo uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2024 ulikutana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa raia wa Ghana kutokana na raia wengi kutopendezwa na uongozi wa Rais Addo hasa sera zake za kiuchumi.
 

Attachments

  • 20250115_130842.jpg
    20250115_130842.jpg
    47.4 KB · Views: 2
  • 20250115_130850.jpg
    20250115_130850.jpg
    50.4 KB · Views: 3
  • 20250115_130846.jpg
    20250115_130846.jpg
    20.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom