SANAMU YA MNYAMA SASA INAPUMUA

SANAMU YA MNYAMA SASA INAPUMUA

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Je unajua kuwa mwaka 321BK mfalme Constantine alipitisha sheria ya kwanza ya jumapili huko Roma? Halafu miaka michache baadaye katika mwaka 325BK hasa 366BK kanisa la Roma likaifanya “jumapili” kuwa siku ya ibada badala ya Jumamosi.

Ilipitishwa sheria ya jumapili mwaka 321bk na Constantine, itapitishwa sheria ya jumapili hivi karibuni na nchi ya marekani.

Ufunuo 13:15 “Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.”

Je sanamu ya mnyama ni nini? Je ni nani amepewa uwezo wa kutia pumzi katika sanamu hiyo? Wengi hudhani sanamu hiyo ni sanamu halisi kama ile iliyosimamishwa wakati wa Danieli, lakini sio, kwa sababu kitabu cha ufunuo kimejaa ishara zinazotumika kuashiria tu vitu vingine tofauti. Sasa Je sanamu ya mnyama ni nini? na ni kwa jinsi gani itatiwa pumzi hata iongee na kutenda? Ili kujua sanamu ya mnyama ni nini kwanza tunatakiwa kujua mmnyama mwenyewe ni nani, ndipo tutajua sanamu au sura yake ikoje.

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mnyama katika unabii huwakilisha ‘taifa’ au ‘ufalme’ (Danieli 7:17,23), na mwanamke huwakilisha ‘kanisa’ (Ufunuo 21:2,9). Hivyo Ufunuo 17:3 inasemea kanisa ambalo limekaa juu ya serikali/taifa (mwanamke juu ya mnyama). Na ni kanisa la Romani pekee ambalo lina uwezo wa kanisa na serikali kwa wakati mmoja. Hivyo mnyama ni utawala wa Upapa wa kanisa na serikali; nguvu za kisiasa na kidini kwamba mfumo wa Upapa kwa hakika ni mnyama.

Kama ungelitaka kutengeneza sanamu/sura ya kitu flani lazima ungelitumia sifa zile zile za kitu hicho ambacho unataka kutengeneza sanamu yake, vivyo hivyo kutengeneza sanamu ya Upapa ni lazima kanisa jingine liunganishwe na serikali, liwe na uwezo wa kidini na kisiasa; au liwe chombo kinachomilikiwa na serikali kama vile kanisa Katoliki lilivyo chombo kinachomilikiwa na serikali ya Vatikani, hapo ndipo sanamu ya mnyama inakuwa imeundwa kikamilifu kwa jinsi kama hiyo.

Ufunuo 13:11 “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.”

Mnyama huyu mwingine anayepanda kutoka katika ‘nchi’ ni Marekani, bahari; sehemu yenye maji, katika unabii huwakilisha ‘watu wengi wa aina mbalimbali’ (Ufunuo 17:15), hivyo nchi; sehemu kavu, itawakilisha ‘sehemu yenye watu wachache’. Pia Ufunuo 13:11 inasema mnyama huyu mwingine ana pembe kama za mwana-kondo; pembe za mwana-kondoo zinawakilisha kuwa mnyama huyo angekuwa na sifa za Ukristo na kutetea amani. Na hii ni kweli kwa taifa la Marekani, liliinuka sehemu isiyo na watu wengi, na lilitetea uhuru wa dini kwa Wakristo waliokuwa wanateswa na Upapa. kwamba mnyama mwingine ni nchi ya Marekani.

Ufunuo 13:14 “Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.”

mnyama wa pili Marekani alikuwa na sifa za kudumisha amani na uhuru wa dini, lakini Ufunuo 13:14 inasema, atawakosesha wakaao juu ya nchi, na kuwadanganya wamfanyie sanamu mnyama wa kwanza; ambaye ni Upapa wa Romani Katoliki.

Hapa inaonyesha kuwa Marekani inawakosesha watu na makanisa na kuwadanganya wajiunge na serikali, na hivyo Marekani inakuwa imefanikiwa kuwakosesha watu na makanisa, na kuwafanya waunde sanamu ya Upapa ya kanisa na serikali.

Lakini wengine watajiuliza kwamba Marekani itawezaje kuwakosesha watu hata makanisa yaunganishwe na serikali na kutengeneza sanamu ya mnyama?

Ni urafi mkubwa wa viongozi wa madhehebu ndio uliosababisha sanamu ya mnyama itengenezwe, viongozi wa madhehebu ambao wanafanya kazi kwa ajili ya pesa tu, ni walafi wakubwa, na wameyasajili makanisa yao serikalini ili wajipatie kuongeza pesa wanazotafuta.

Madhehebu yote yameunganishwa na 501(c)3 free status, ambayo inamwezesha mchungaji wa dhehebu lililojiunga kwenda dukani na kuchukua mahitaji yake bila kulipia pesa. Na sheria za IRS (Internal Revenue Service) ya Romani Katoliki zinasema, mara tu kanisa limesajiliwa katika 501C3 free status, papo hapo linakuwa limeunganishwa na serikali ya Marekani, na pia linakuwa limeunganishwa na IRS ya Romani Katoliki kama mali yao. Na kanisa likishajiunga tu na 501C3 haiwezekani kulitoa huko mpaka zilipwe fidia zote zilizotumiwa na kanisa tangu kujiunga, hii inamaanisha kama kanisa lina miaka 20 limejiunga na 501C3 likijitoa litafirisika kabisa hata kuangamia.

THE TRUMPET vol. IX – Issue 6 NOV/DEC 2001 ambayo pia inapatikana mtandaoni inatuambia kuwa, kanisa ambalo limejiunga na 501C3 hata kama likijitoa na kuendelea kufanya kazi kama kanisa la kawaida, bado tu linakuwa kwenye mtego wa IRS. Wengi wamejaribu kuyatoa makanisa yao katika mfumo wa 501C3 lakini wameshindwa kwa sababu ya mashariti, na faini zilizopo kwa wale wanaotaka kujitoa. Hivyo, kwanini wachungaji na viongozi wa makanisa wamejiingiza katika mtego kama huu? Ni kwa sababu ya urafi wa pesa!

Ufunuo 13:15 “Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.”

Mach 7, 2006 Uongozi wa George Bush uliweka kwenye sheria utaratibu mpya ambao uliondoa tofauti kati ya kanisa na serikali na kuyafunga makanisa yote yenye 501C3 status kuwa VYOMBO VYA SERIKALI, na hii ndio sanamu ya mnyama. kutafuta kama kanisa lako linashiriki 501C3.ingia website ya MUUNGANO WA MAKANISA DUNIANI www.eucumenism.com


Makanisa yote yenye 501C3 yako chini ya uangalizi wa serikali, ndio maana tunaona madhehebu yanaweka wanawake kama wachungaji au wazee wa makanisa, na tunaona wachungaji wa madhehebu wakisema wazi kuwa Allah ni Mungu yule yule kama Mungu wa Wakristona Qran ni kitabu kilichobarikiwa kama vile Biblia. Wachungaji wote wenye 501C3 hawaruhusiwi kuhubiri ujumbe ambao serikali ya Marekani imepiga marufuku usihubiriwe, na ni lazima wafanye kila kitu ambacho serikali inatamka, vinginevyo watafutiwa sanamu yao ya 501C3 pamoja na kulipishwa faini itakayowaghalimu kufirisika kabisa. Hivyo, wakati wowote ambao serikali ya marekani itakaposema, “tunataka watu wote wapumzike siku ya Jumapili”, viongozi hawa wa madhehebu ambayo yamenaswa kwenye mtego huu wa 501C3 hawatakuwa na lolote la kufanya isipokuwa ni kuwalazimisha washiriki wa makanisa yao wasali Jumapili, la sivyo watafutiwa sanamu yao ya 501c3, na kupigwa faini ya kulipa pesa zote walizotumia tangu kujiunga na mfumo huu wa 501C3 kitu ambacho kitapelekea dhehebu lote kufirisika kabisa.

Na haya yote yanasababishwa na urafi wa pesa wa wachungaji na viongozi wa makanisa. Yesu alituonya kuwa.

Mathayo 6:24 “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Unabii ulisema kuwa Marekani itatia pumzi katika sanamu ya mnyama na kuifanya sanamu hiyo inene na kuwua wote wasioisujudia.

Ufunuo 13:15 “Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.”

Ni kwa jinsi hii ya mfumo wa 501C3 kwamba Marekani imetia pumzi katika sanamu ya mnyama (Marekani na makanisa yaliyoungana na serikali yake), na hivi karibuni Marekani itakapopitisha sheria ya jumapili, sanamu hiyo itaanza kunena na kuwafanya wote wasioisujudu wauwawe.

Ufunuo 13:16 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;”

Marekani itakapopitisha sheria ya jumapili ndipo makanisa yote yenye 501C3 yanayounda sanamu ya mnyama pamoja na serikali yao ya Marekani, watashirikiana ili kuwalazimisha watu wapokee alama ya mnyama[jumapili]. Na wale wote ambao hawatakubali kupokea jumapili amri ya mwanadamu watazuiliwa kuuza na kununua, watafungwa magerezani na kuteswa, na hata kuuwawa.

Ufunuo 13:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

“Kama tunaamini dini kuwa ni kweli, lazima tutambulishe tena adhabu ya uhalifu kwa wale wanaoshindwa kuhudhulia kanisani siku ya Jumapili.” -Daily Independent4-11-98-Sara Maitland “On the issues of belief”

Je njia hii ya kulazimishwa kusujudia sanamu ilishafanyika pia huko nyuma? Ndio!

Danieli 3:4-6 “Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.”

Danieli 3:7-8 “Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi.”

Serikali ya kipindi cha Danieli iliweka sheria ya kusujudu sanamu, na kama mtu asingeisujudu sanamu angeuwawa. Na kama tunavyoona marafiki watatu wa Danieli; Shadraka, na Meshaki, na Abednego, walikataa kuvunja sheria ya Mungu wao kwa sababu ya sheria ya mwanadamu. Hii ilimkasilisha mfalme wa siku hizo kama itakavyowakasilisha watawala watakaopitisha sheria ya jumapili, watakapoona Wakristo wanakataa kutii amri ya mwanadamu kuliko amri ya Mungu.

Danieli 3:14-15 “Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?”

Watu hawa watatu walikutana na jaribu la kifo kwa jinsi ya maumivu makali mbele ya adui yao, kama wasingekubali kusujudu sanamu. Je walifanya nini?

Danieli 3:16-18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”

Wakati huohuo mfalme aliamuru watu hao watu warushwe kwenye tanuri ya moto. Lakini Mungu alikuwa pamoja nao kuwasaidia kama vile atakavyokuwa pamoja na wale watakaochagua kutii amri yake kuliko ya mwanadamu wakati sheria ya jumapili itakapopitishwa. Baada ya kuwatupa waaminifu hao motoni, hiki ndicho mfalme aliona…

Danieli 3:24-25 “Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.”

Hadithi hii iliishia pazuri, wale waliochagua kumtii Mungu kuliko mwanadamu waliokolewa na tanuru ya moto. Petro anatuambia kwamba…

1Petro 4:12-13 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.”

Hivyo, na katika siku zetu pia vilevile kama siku za Danieli watakuwepo watu ambao watavumilia mpaka mwisho wasiisujudu sanamu ya mnyama, wala kupokea chapa au alama yake. Hao pia wataokolewa na watatawala pamoja na Kristo mbinguni.

Ufunuo 20:4 “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”


Ukweli ni:

313B.K., Vatican ikawa kanisa na serikali (mnyama)

na Machi 7, 2006 Marekani ikawa kanisa na serikali (sanamu ya mnyama).

Yesu hakuruhusu muungano wa kanisa na serikali, alisema…

Luka 20:25 “Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu.”

Serikali inatafuta kodi ambayo kiukweli ni pesa, na Mungu kwa hakika hatafuti pesa. Hivyo, serikali na Mungu ni vitu viwili tofauti, na haiwezekani kumtumikia Mungu na serikali kwa wakati mmoja.

Mathayo 6:24 “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Yohana 18:36 ”Yesu akajibu, falme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa nikatiwa mikononi mwa Wayahudi.”

Kuhusu sisi Yesu anasema…
Yohana 17:14 “Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.”

Je imekuwaje makanisa yanaungana na serikali dunia na kuvunja amri ya Kristo? Kanisa kuungana na serikali ni kufanya uzinzi na kuvunja amri ya 7 ya Mungu.

Yakobo 4:4 “Enyi wanzinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure?…”

1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Mungu hakumo ndani yake.”

Luka 6:26 “Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.”

Kama kanisa lako limeungana na serikali, au na dunia, au katika Baraza la makanisa duniani, linavunja amri ya 7 na limekuwa sanamu ya mnyama. Na Je unajua Mungu anataka nini kwa wale ambao wako kwenye makanisa yaliyoungana na serikali na kuwa sanamu ya mnyama?

Ufunuo 14:9-10. “Na mwingine, malaika wa tatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Kwa hiyo kama mtu ameunganika na sanamu ya mnyama, ni hakika ataadhibiwa na kupokea mapigo ya hasira ya Mungu. Hivyo sauti ya upendo ya Mungu inasikika ikisema…

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amemkumbuka maovu yake…Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemuhukumu ni mwenye nguvu.”

FB_IMG_1540123764463.jpeg
FB_IMG_1541586090838.jpeg
IMG-20181106-WA0031.jpeg
FB_IMG_1540123502299.jpeg
FB_IMG_1541730119811.jpeg
 
Wakatoliki na wanaofata mafundisho ya kikatoliki watakuja kubisha ,wakati ukweli umewekwa wazi
 
Kwanini Mungu apite kwenye mapito makali namna hii wakati anaweza kutamka tu mambo yakawa shwari?

Je, yupo kweli huyu Mungu au hadithi za kijinga tu zisizo na mbele wala nyuma?

Kama yupo basi anaelekea kushindwa na mwanadamu aliyemuumba yeye
 
Write your reply...Hapo allah kaingiaje naona umezungukaaaa sijui Yesu mara matayo mara roma naona ghafla umechomekea Qur an mara uislamu ...uzushi wenu hukohuko kwenye usabato na ukatoliki sie msituhusishe
 
Write your reply...Hapo allah kaingiaje naona umezungukaaaa sijui Yesu mara matayo mara roma naona ghafla umechomekea Qur an mara uislamu ...uzushi wenu hukohuko kwenye usabato na ukatoliki sie msituhusishe
Labda kama hujui

Ila tambua uislamu ni dhehebu la katoliki
 
Write your reply...Jifariji ivoivo ....mi naona mmengemalizana wenyewe tu hukohuko kwenye Yesu huku tuache kabisa ...ugomvi wenu sie hautuhusu
 
Teh teh teh....bila shaka wewe ni wa Bwn. Mudy wa Mecca.
Write your reply...Hapo allah kaingiaje naona umezungukaaaa sijui Yesu mara matayo mara roma naona ghafla umechomekea Qur an mara uislamu ...uzushi wenu hukohuko kwenye usabato na ukatoliki sie msituhusishe
 
Labda kama hujui

Ila tambua uislamu ni dhehebu la katoliki

Zama Basi mkuu, ukipata muda anzisha uzi ambao utafichua hilo ili nasi tupate nuru..... Ahsante, usisahau kuni tag
 
Back
Top Bottom