SoC04 Sanduku la Mpiga kura liboreshwe

SoC04 Sanduku la Mpiga kura liboreshwe

Tanzania Tuitakayo competition threads

Berto Mdendemi

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Ili tuendelee tunahitaji watu, siasa Safi, ardhi na uongozi bora.

Hivi vinategemeana, kinara uongozi bora. Uongozi bora utatoa maono, mengine yachangie kuleta maendeleo.

Kiongozi anaongoza watu, Kazi zake; kupanga, kusimamia, kufundisha na kuhamasisha. Anapashwa awe na maono, mbunifu, na mboreshaji. Sifa zake; uaminifu, uadilifu, nidhamu, ubunifu, na kujituma.

Kutokana na dhana hii nafasi ya uongozi bora ni ya juu.
Kiongozi anaongoza watu, nafasi ya pili, watu.Watu wenye afya ya akili, mwili, wanaojitambua na wazalendo.

Siasa Safi ya tatu, uongozi bora na watu watatengeneza siasa safi zitakazozungusha gurudumu na kupata uongozi bora, watu sahihi,siasa safi , mwisho kutumia ardhi (rasilimali), kuleta maendeleo.
Kwenye piramidi ya kuleta maendeleo; uongozi bora uko juu, watu wanafuata, kisha siasa safi halafu ardhi.

Pasipo uongozi bora hatuwezi kupata watu sahihi. Tukikosa watu hatuwezi kupata viongozi bora miongoni mwao. Viongozi bora na watu sahihi wakikosekana hatupati siasa Safi. Tukikosa hayo tunashindwa kutumia ardhi (rasilimali)
Ukinara wa uongozi kuleta maendeleo si wa kupuuzia. Tunapataje viongozi wenye maono, wabunifu, waboreshaji, waaminifu, wanaojituma na wazalendo. Wakipatikana wanalindwaje?. Bahati mbaya wanashindwa wanatolewaje?.
Njia nzuri ni kuboresha sanduku la mpiga kura ili watu sahihi wachague viongozi bora miongoni mwao.

Sanduku bora lisaidie; kuchagua viongozi bora, kuwalinda na kutoa wabovu. Sanduku bora litalazimisha viongozi kuheshimu watu na kuwasikiliza.

Kupata sanduku bora tunahitaji uongozi bora utufikishe huko, wenye maono na uzalendo. Nyerere alionesha cha kufanya kuboresha sanduku la mpiga kura mageuzi ya vyama vingi yalipoanza, aliunga mkono uanzishwaji mfumo huu kama sehemu ya kuboresha sanduku. Nyerere alimpinga mgombea wa chama chake kule Mara kuonesha sanduku bora sio kama Ushabiki wa Yanga na Simba na haki lazima izingatiwe. Baba wa taifa alisema vyama vingi vinafanya serikali isinzie yaani kufanya uongozi bora. Mwishowe alishauri Chama tawala kujenga upinzani Imara. Hii yote kuboresha sanduku la mpiga kura.
Nyerere alitufikisha hapo, nini kifanyike kuboresha sanduku ili kupata uongozi bora?

Sanduku bora litoe majibu stahiki (haki). Mazingira Yatengenezwe kura zitoe jibu linalokubalika sasa kuna kutokuaminika hali inayopelekea hamasa ya kupiga kura kushuka, kwenye chaguzi zote serikali na vyama. Haki ni muhimu katika kuwa na sanduku bora. Vipengele vya kufanyia kazi usimamizi, upigaji kura, uhesabuji na uangalizi.

Katika kuboresha Kutanua wigo wa wapiga kura ni muhimu,hili lifanikiwe haki lazima izingatiwe, watu hawawezi shiriki iwapo hawauamini uchaguzi.Wigo utanuliwe Hadi ngazi za vyama kwa wanachama wote kushiriki kuchagua. Sio kupitia wawakilishi ambapo mizengwe, rushwa na makundi hujitokeza. Imetokea wawakilishi wanachagua halafu vikao vya juu vinabadilisha hii inadhihiri si mfumo mzuri. Wanachama kuchagua linafaa hata Kwa vyama vingine kama wafanyakazi. Mfano kunatakiwa mgombea ubunge wanachama wote jimboni wachague wa kuwawakilisha.
Utanuaji wigo wapigaji uendane na utanuaji wigo wa wagombeaji. CCM imepiga hatua hapa, wanajitokeza wagombea wengi kisha mmoja anapita Lau imesaidia. Labda waangalie Kutanua wigo wa wapigaji. Kuna shida Kutanua wigo wa wagombea labda kutokana na maslahi binafsi na ukosefu siasa safi. Tumekosa siasa safi mpaka tunaona wa chama kingine ni adui. Tulipashwa kukubaliana kutokubaliana, ilipashwa kumuona wa chama kingine si adui labda afanye vitendo vya uadui. Wengi wenye uwezo wa kuongoza hawagombei sababu ya changamoto za uvyama. Ugombea binafsi ungeongeza wigo wa wagombea Hasa wasiopenda shida za vyama. Nyerere aliwahi kulizungumza lakini halijafanyiwa Kazi.

Lingine la kufanya kuboresha sanduku la mpiga kura ni kuongeza nafasi za viongozi wanaochaguliwa na wananchi. Wananchi walitoa maoni Kwa mzee Warioba kwamba viongozi gani wachaguliwe na wananchi ili kuongeza ubora wa uongozi, kuna nafasi ilipendekezwa zifutwe na nyingine ziunganishwe, kikubwa wanaochaguliwa wawe na sifa. Mfano kwenye wilaya tukiachana na mbunge (mwakilishi), yupo mkuu wa wilaya, mwenyekiti na mkurugenzi.
Njia ni nyingi, za uboreshaji kikubwa viongozi watuongoze ili njia hizo zisilente sintofahamu. Mwalimu alishauri mabadiliko yasisubiri fujo kama Romania.

Faida ni nyingi za uboreshaji kubwa kufanya uongozi kuwa bora kama alivyosema Nyerere; kwamba vyama vingi vinasaidia serikali isilale kama njia ya uboreshaji.
Sanduku bora hufanya viongozi kujituma kwa matarajio ya siku zijazo. JPM alipenya utendaji wake ulimbeba na ubora wa sanduku chamani.

Sanduku bora linapunguza tuhuma za upendeleo, tuhuma za upendeleo huleta shida. Sanduku bora tuhuma za upendeleo hazina nguvu.Marekani sanduku lina nguvu kuanzia kwenye vyama. Licha ya nguvu ya kina Bush, Jeb Bush hakufua dafu kwa Trump. Mshindi asilimia kubwa anapatikana kwa haki mazingira ya upendeleo yanakosa nguvu.
Sanduku bora linapunguza unafiki,ni miongoni mwa mambo yanayotudondosha. Kuna mnyororo wa unafiki kuanzia kwa viongozi hadi watu.Unafiki unafanya sera isieleweke ni safi au chafu, inaangaliwa sura ya mkuu. Sanduku bora litasema kwa vitendo siasa hii ni safi au chafu.
Faida ni nyingi za sanduku bora ili kupata uongozi bora lakini katika utengenezaji tuepuke serikali za umoja wa kitaifa mara nyingi hazibadili kitu, wezi wanaungana na ni dhaifu. Tunapo boresha daftari la mpiga kura tufikirie kuboresha na sanduku.
Berto Mdendemi
mdendemiberto@gmail.com
 
Upvote 2
Back
Top Bottom