Sarafu mpya ya BRICS ina umiliki wa Nchi moja wapo au ni mfano wa Sarafu ya EURO ya Ulaya? Itashindana vipi na Dollar isiyo na mipaka wanachama?

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Dollar ni sarafu ya Marekani na inayotumiwa na Dunia nzima licha ya kuwepo sarafu mbali mbali zinazoundwa na baadhi ya umoja wa nchi mbalimbali kama Africa Mashariki, Umoja wa Ulaya n.k na lengo moja wapo ni sarafu hiyo itumike kibiashara kwenye nchi hizo

Sarafu mpya ya mataifa ya BRICS, ni vigumu na haitawezekana kushindana na Dollar ya marekani

Sababu za kushindwa ni moja tu na hii hapa

Sarafu ile ndio itakuwa ni sarafu ya umoja wa mataifa hayo yanayoundwa na China,Russia, Brazil na SA n.k ambapo nchi hizo nazo zina sarafu za ndani ya nchi zao

Tofauti na Dollar inayomilikiwa na Marekani, inatumika kama sarafu ya Marekani na duniani kote

Baada ya umoja wa Ulaya kuundwa, walikubaliana kuunda sarafu yao itakayotumika kibiashara katika mataifa hayo n.k

Hata hivyo, Dollar iliendelea na imeendelea kutumika pia katika mataifa hayo licha ya kuwepo sarafu yao pendwa

Akili yangu inanituma kuwa, ushindani wa sarafu unaoendelea sasa kwa nia ya kuiondoa Dollar kwenye mzunguko wa Dunia nzima, ni lazima pia iwepo sarafu ya nchi mojawapo yenye nguvu kiuchumi na itumie ushawishi wa kutosha ili kuzishawishi nchi zote kwanza zinazounda BRICS ziikubali na kisha zianze kuitumia kitu ambacho ni kigumu kwao, China atakubali Russia sarafu yake itumike kushindana na Dollar? Hali kadhalika Russia atakubali sarafu ya China ndio iwe mbadala wa Dollar?

Wakikubaliana kwenye hilo, hapo ndipo mchakamcaka wa kiushindani na Dollar itakuwa imeanza rasimi

Mpaka hapa, bado sjaona mchakato wa ushindani wa sarafu ya Dollar na sarafu nyingine yeyote

Kuiondoa Dollar kwenye mzunguko yahitaji utulivu wa akili na kazi ifanywe haswa pia ushawishi wa nguvu za uchumi, Dola n.k
 
Kwani nani alisema hiyo sarafu ya brics inakuja sababu ya kushindana na Dollar? Watu wameunda sarafu yao ili wafanye biashara kwa sarafu yao, wakopeshane kwa sarafu yao etc Brics currency itakuwa na thaman kubwa tu ila yamkini isiwe maarufu zaidi ya Dollar kama vile Paund ya UK ilivyo na thaman zaidi ya USD ila sio maarufu ila umaarufi utategemea na uhitaji hasa wa pesa hiyo katika nchi husika.

Tanzania kama tunanunua vitu vingi toka China, UAE na Russia basi ujue wafanyabiashara wakitanzania watalazimika Brics currency na nchi itaona itakuwa na uhitaji wa kuweka reserve ya sarafu ya brics ili iweze kulipia mikopo utakayoichukua katika Bank ya Brics.
 
Hivi baada ya kuwepo USD basi hakuna ruhusa Tena ya nchi zenye malengo na mitazamo inayofanana kuunda sarafu Yao?
Mbona Europe waliunda fedha Yao euro lkn haikusemwa kua wanataka kushindana na USD.
Nchi za BRICS zimeunda umoja wao kulingana na mahitaji Yao imeonekana wanataka kushindana na G7 na USD.
Kwa hiyo kuwepo kwa G7 kunaondoa ruhusa kwa nchi nyingine kuunda umoja wao?
Habu fikiria Kuna miungano mingi TU na yenye malengo tofauti,mfano EU,AU,EA,Saddc, ECOWAS, Shanghai Cooperation, OPEC NATO n.k
Lakini kuundwa kwa BRICS TU imekua maneno ya kuipinga Kila Kona.
Hebu fikiria nchi ambazo zimetengwa au kuwekewa vikwazo na kikundi Cha nchi TU,Tena sio na Umoja wa mataifa,je nchi hizi hazina haki ya kujiundia umoja wao wa kusaidiana kiuchumi?
Ukiangalia Kwa jicho la utulivu utaona nchi za ulaya Magharibi ni kama umoja usio rasmi kwa sababu nchi moja ikikuwekea vikwazo zote zinakuwelea mfano USA.
Mfano Cuba, Korea kaskazini,Iran,Urusi, Venezuela na nchi zisizopendwa kama Syria N.k
Sasa hizi nchi zenye mrengo tofauti na west haziruhusiwi kua na umoja wao?
Jamani eeeh Dunia ni Mali ya mwenyezi Mungu Kila mtu ana haki ya kuishi na kujifanyia mambo yake bila kuumiza wengine.

BRICS currency itakua na itaweza kuiupunguzia nguvu USD kwa sababu zifuatazo.
Nchi zote ambazo zimetengwa na USA na marafiki zake zitaachana na matumizi ya USD kwa biashara baina Yao .
Mafano Sasa hivi sio Siri nchi karibu zote hapa duniani zimekua zikiitumia USD kama fedha ya kufanyaia biashara,mfano ukitaka kununua machine china utalipa kwa USD au kununua gari Japan utalipa kwa USD au ukitaka kununua mafuta said Arabia utalipa kwa USD .
USD imekua ikitumika Kwa miaka mingi.
Sasa itakapokuja fedha ya BRICS nchi zisizopenda kua chini ya USA zitahamia kwenye BRICS currency katika kufanya biashara.
Mfano itakua hivi na ndio itakua anguko la USD kimataifa na kubaki kua pedha ya USA pekee.
Nchi kadhaa zikitaka kununua mafuta soud Arbia,itaziambia zilipe kwa BRICS currency,
Nchi nchi zikitaka kununua machines china,china itaziambia zilipe kwa fedha ya BRICS,
Nchi zikitaka kununua silaha Kwa Urusi Urusi itaziambia zilipe kwa BRICS currency.
Hapo ni Kwa uchache TU,kumbuka bidhaa ziko nyingi sana,sio bidhaa TU Bali pia na huduma.
Sasa hebu fikiria nchi kama china,India, Urusi,Iran,soud Arbia,Misri, UAE,nchi kadhaa za afrika,latin American,far east,Arabs na baadhi ya nchi za ulaya zikahamia kufanya biashara zao kwa kutumia fedha ya BRICS je umaarufu wa USD haitashuka?
Je thamani ya USD itabaki vile Ile licha ya nchi nyingi kuacha kuitumia katika biashara zao?
Kwa hakika USD haitabaki kama ilivyokua mwanzo.
Itabaki na thamani sawa lakini sio thamani kubwa kama ilivyo hivi Sasa Kwa sababu inatumika Dunia nzima kama fedha ya Dunia,Sasa tufanye robo nusu ya nchi za Dunia zikaachana nayo hakika thamani yake itashuka.
Kumbuka kuna nchi hazita itumia USD wala hazitaitumia BRICS currency bala nazo zitaamua kutumia fedha zao binafsi ama fedha nyingine mfano euro na fedha nyingine.
USA itabaki na USD yake nayo ukitaka kununua kitu kwao nao itabidi tuendelee kununua kwa USD kama vile Leo hii ukitaka kununua bidhaa UK utalipan kwa Pound ama ukitaka kununua bidhaa ulaya utalipa kwa euro.
USD itabaki kama fedha yenye nguvu ya USA lakini itapoteza nguvu yake kimataifa baada ya kua nchi nyingi zitakua zimekwisha iacha.
Ndugu zangu zaidi ya nusu ya nchi za Dunia zikiiacha USD itaendeelaje kua na nguvu?
 
Mchambu kutoka mchamba wima katika ubora wako
 
Marekani alibugi sana kuchochea vita ya Urusi na Ukraine na kutumia mfumo wake wa dollah kunyanyasa nchi nyingine kwa kuziwekea vikwazo. Sasa yanamtokea puani, BRICS wamemkalia kooni, uchumi wake unaenda kuyumba sana sababu ya sarafu yake ya dollah inaenda kupoteza ushawishi duniani
 
Ni hivi karibuni kulikuwa na makubaliano ya mpango wa kupitisha SARAFU ya MUUNGANO wa nchi 5 zenye UCHUMI mkubwa ktk G-20, KUBUNI SARAFU ili kuto tegemea SARAFU ya marekani( dollar)
*Je wataweza kupambana na vikwazo kutoka kwa marekani?.
* itakuwaje Kama mpango ukifanikiwa Kuna faida yyte tutayo nufaika Africa.
 
Watajaribu lakini hawatashinda
 
Back
Top Bottom