sarafu yetu vs ukuaji wa uchumi

kaluu

Member
Joined
Oct 5, 2011
Posts
17
Reaction score
1
hivi kweli kwa jinsi sarafu yetu inavyo poromoka dhidi ya dolar inashabiana na yanayosemwa kuwa uchumi wetu unakuwa kwa kasi?wenye euelewa juu ya hili naomba ufafanuzi
 
Hivi dora ni kiasi gani cha shilingi kwa sasa, maana kila siku kuna mabadiliko!!
 
haijafika huko !! Ni 1783.20 now!!

HEbu jamani wanauchumi niambieni hili lina maana gani kwa uchumi wetu maana mi na shindwa kuelewa.

Je effects zake kwa sisi walala hoi ni zipi?

Na ni nani wa kulaumiwa Raisi, waziri wa fedha,au wote na kama yupo mwingine naomba msaada wenu.
 
Thamani ya fedha ina mahusiano na ukuaji wa uchumi lakini sio kigezo pekee cha kupima ukuaji wa uchumi, fedha inaweza kushuka dhamani lakini uchumi usiwe umedondoka ,
 
Thamani ya fedha ina mahusiano na ukuaji wa uchumi lakini sio kigezo pekee cha kupima ukuaji wa uchumi, fedha inaweza kushuka dhamani lakini uchumi usiwe umedondoka ,

Mfano ni japan...lakini hata wao yen imeanza kupanda thamani dhidi ya dola
 
Leo dola kwa bei ya BOT ilikuwa 1690. Kwanini commercial banks na beureal de change wanauza 1850? Do we need something like Ewura or Tcra to regulate them?
 
Leo dola kwa bei ya BOT ilikuwa 1690. Kwanini commercial banks na beureal de change wanauza 1850? Do we need something like Ewura or Tcra to regulate them?

Exchange rates za BoT ni indicative rates lakini sokoni hali ndiyo hiyo. Fedha imeshuka thamani huwezi kuamini kwa mwendo huu hadi Oktoba 30 lazima itafika 1950 kama siyo 2000. Madhara yake ni makubwa mno kwa walala hoi kwa vile bidhaa na huduma zote lazima zipande bei huku kipato kikibaki pale pale kwa mfano anayepata mshahara wa TZS 200,000/= ataendelea kupata mshahara huo huo huku nauli ya basi kutoka Musoma hadi Dar ikiwa imepanda kutoka TZS 50,000/= hadi 80,000/= sasa angalia looser hapa si mwenye gari bali ni yule msafiri anayetumia huduma. Anayeagiza gari la USD 2000 sasa atalazimika kulipa TZS 3,700,000/= (Kwa rate ya 1850) badala ya TZS 3,200,000/= (Kwa rate ya 1600), kwa mifano hii miwili yatosha kuonesha maumivu ya sarafu yetu kushuka thamani yake dhidi ya Dola na sarafu za mataifa mengine.

Wakati umefika viongozi wasio na tija kama Bw. Mkullo na Bw. Ndullu waachie ngazi kama EL alivyofanya kwa maslahi ya walio wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…