LGE2024 Sarakasi za Chaguzi za Serikali za Mitaa: Je, Nani Alaumiwe?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Inasikitisha sana kuona nchi inayofuata utawala wa kidemokrasia inakumbwa na mambo yasiyofuata sheria, taratibu, na kanuni kila inapofika wakati wa uchaguzi. Wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani wameenguliwa kwa sababu zisizo za msingi, kama vile herufi moja kwenye jina kukosekana, fomu kutokuwa na muhuri, au makosa madogo ya umri.

Makosa kama haya yanaweza kurekebishwa na hayapaswi kuwa sababu ya kumzuia mgombea kuendelea na uchaguzi. Uchaguzi huu unaonekana kama "witch hunt" au kuwashikilia wagombea kwa sababu zisizo na msingi. Waziri anayesimamia uchaguzi yupo, lakini mambo kama haya yanaendelea. Namshauri Mheshimiwa Waziri achukue hatua za haraka ili kuepusha hisia kwamba kuna upendeleo kwa chama fulani.

Soma: LGE2024 - Uchaguzi serikali za mitaa: Mamia ya wagombea wa upinzani waenguliwa, waapa 'kutosusia shamba'
 
Chura kiziwi ,Delila wa 4R
 
Back
Top Bottom