Pre GE2025 Sare za bodaboda kuwekwa picha ya Rais Samia na Mchengerwa kuagiza madereva bodaboda waache kusumbuliwa halitaongeza uvunjifu wa sheria?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mchengerwa atoe tafsiri ya usumbufu ni ipi.
Je akivunja sheria barabarani aachwetu kwakua kavaa hicho kizibao?
Vipi akiwa hana leseni? Je chombo kama hakina namba ya usajili. Ikiwa akipakia watu washeli hata niwatoto wa chekechea asiulizwe?
Kwanini mambo yanayomhusu waziri wa mambo ya ndani na jeshi la polisi tena mambo muhimu na mazito unayazungumzia kirahisi?
Hapo Mchengerwa anachezea usalama wa watanzania.
 
Mchengerwa na Abdul hawa jamaa wanaongoza kuchezea pesa za nchi kwa sasa, wanavuna wapendavyo.
 
EEEEEeeeeeeeNnnHEEEEeeee!
Mambo mengine ni kucheka tu.
Hizi sare bodaboda watagawiwa bure au watanunua? Sheria inawataka bodaboda wavae hizi sare kazini, vinginevyo hawaruhusiwi kufanya kazi?

Huko maofisini kwenye mawizara yote na mashirika ya umma, sare za aina hii watapewa lini?

Hawa bodaboda wanamfanyia kazi huyo mwenye picha yake kwenye sare hizo?

Sasa viongozi hawa wameingia kwenye upumbavu, halafu wanataka kila mtu awe mpumbavu kama walivyo wao.
 
ni kosa kwa askari wa usalama barabarani kuwagombanisha madereva wa bodaboda na mama Samia, uvunjifu wa sheria si uvunjifu wa amani.
Sijui haya maneno yalisemwa na nani, huko CCM, mkuu 'Hismastersvoice'?
"... uvunjifu wa sheria si uvunjifu wa amani."!
Ukitaka kujua ulaghai wa hawa watu, tazama na uelewe hadaa ya misemo yao kama huu hapa.
 
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa jana alikuwepo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijiji Dar es Salam wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa Madereva bodaboda na Bajaji wa Jiji la Dar es salaam.

Sare hizi zina picha ya Rais Samia kama zinavyooneka hapo, lakini pia Mchengerwa alitoa maagizo kwa madereva wa bodaboda kuacha kusumbuliwa kwakuwa wanashiriki vizuri kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.

“Kuanzia sasa sitaki kusikia kamata kamata ya hovyo, inayotokana na wakati fulani kuwepo na sintofahamu baina yenu na Maafisa wa Serikali, mchango wenu ni mkubwa sana hivyo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inawathamini sana ninyi Maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji, na ndio maana ninataka kuona ushirikiano mzuri unakuwepo baina yenu na Serikali"

Wakuu tunajua bodaboda ndio wanaongoza kwa uvunjifu wa sheria barabarani, na wengi hawana leseni, mtu anajifunzia zake mtaani siku mbili tatu huyo mtaani, kwa agizo hili hatuoni kama ni uvunjifu wa sheria utazidi kuongezeka?

Kwanini sare hizo zimewekwa picha ya Rais? Ukijumlisha na agizo la Mchengerwa si ni kampeni hiyo kabisa ya waziwazi, kila kitu mama atenda, tuanze kuuliza kama yule Mchungaji alivyosema, kama vyote amefanya Rais, nyie Wabunge na Mawaziri mnafanya kazi gani?

====

Pia soma: Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa wote simamieni mfumo wa Kidijitali wa kuwatambua Madereva Bodaboda na Bajaji

#KataaMachawa
#KataaUozo2025
Kampeni zimeaanza mapema sana..Halafu wangeweka rangi zenye high visibilty kama njano kuwasaidia kuonekana mbali, hizo reflctive stripes hazitoshi.
 
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa jana alikuwepo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijiji Dar es Salam wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa Madereva bodaboda na Bajaji wa Jiji la Dar es salaam.

Sare hizi zina picha ya Rais Samia kama zinavyooneka hapo, lakini pia Mchengerwa alitoa maagizo kwa madereva wa bodaboda kuacha kusumbuliwa kwakuwa wanashiriki vizuri kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.

“Kuanzia sasa sitaki kusikia kamata kamata ya hovyo, inayotokana na wakati fulani kuwepo na sintofahamu baina yenu na Maafisa wa Serikali, mchango wenu ni mkubwa sana hivyo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inawathamini sana ninyi Maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji, na ndio maana ninataka kuona ushirikiano mzuri unakuwepo baina yenu na Serikali"

Wakuu tunajua bodaboda ndio wanaongoza kwa uvunjifu wa sheria barabarani, na wengi hawana leseni, mtu anajifunzia zake mtaani siku mbili tatu huyo mtaani, kwa agizo hili hatuoni kama ni uvunjifu wa sheria utazidi kuongezeka?

Kwanini sare hizo zimewekwa picha ya Rais? Ukijumlisha na agizo la Mchengerwa si ni kampeni hiyo kabisa ya waziwazi, kila kitu mama atenda, tuanze kuuliza kama yule Mchungaji alivyosema, kama vyote amefanya Rais, nyie Wabunge na Mawaziri mnafanya kazi gani?

====

Pia soma: Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa wote simamieni mfumo wa Kidijitali wa kuwatambua Madereva Bodaboda na Bajaji

#KataaMachawa
#KataaUozo2025
BODA BODA HANA TOFAUTI NA MWANAMKE MALAYA KUTUMIKA NI WAJIBU
 
Sijui haya maneno yalisemwa na nani, huko CCM, mkuu 'Hismastersvoice'?
"... uvunjifu wa sheria si uvunjifu wa amani."!
Ukitaka kujua ulaghai wa hawa watu, tazama na uelewe hadaa ya misemo yao kama huu hapa.
Viongozi wa CCM ndio wanaongoza kwa kuwalinda wahalifu lakini amani haijawahi kutetereka.
 
AAhaaaa!
Kwa hiyo huu msemo ni ubunifu toka kwako na siyo hao niliodhani wanautumia?
Wewe ni 'chawa'?

Kwa hiyo unawahimiza CCM waendelee "kuvunja sheria", kwa vile "amani haivunjiki"?
Inakukera sana amani kutovunjika?

Haihitaji kuvunja amani kuwatia adabu CCM. Vuta subira kidogo utauona moto wa waTanzania.

Hii nchi ni tofauti sana na hizo takataka nyingine mnazotaka tufuate mifano yao.
 
Back
Top Bottom