Sare zaendelea kuiandama Yanga

Sare zaendelea kuiandama Yanga

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
20210217_211416.jpg


Michezo mitatu ya Kigi Kuu ya Soka Tanzania Bara imechezwa hii leo katika viwanja tofauti

Baada ya kuondoka na alama 1 katika mchezo dhidi ya Mbeya City juma lililopita, Yanga hii leo wameambulia alama moja pia baada ya mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kumalizika kwa sare ya 3-3

Magoli ya Yanga yamefungwa T. Kisinda 14', D. Kaseke 30' na M. Tonombe 61' huku magoli ya Kagera Sugar yakifungwa na P. Mwalyanzi 11', H. Mwaterema 24' na Y. Mhilu 45'+2

Mchezo huo umehusisha magoli mengi zaidi kuliko michezo mingine iliyopigwa hii leo

Aidha, baada ya kumlazimisha Azam kichapo cha goli 2-1 katika Dimba la Mkwakwani, Coastal Union hii leo wamerejeshewa adhabu ya goli 2-1 na Dodoma Jiji katika Dimba la Jamhuri huko Dodoma

Magoli ya Dodoma Jiji yamefungwa na A Jabir 57' na J Mtegeta 66' , huku goli la Wagosi wa Kaya likifungwa na R Hafidh 83'

Mchezo mwingine uliopigwa hii ni leo ni kati ya Mtibwa Sugar ambao walikuwa nyumbani kwenye uwanja wa Jamhuri kuumana na Ihefu FC. Si Mtibwa wala Ihefu ambaye alionyesha ubabe wake baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1

Goli la Mtibwa limefungwa na K Sabato kunako dakika ya 38, huku goli la Ihefu likifungwa na I Ngoah dakika ya 13
 
Ligi tunaongoza,
Ndo timu pekee hatujafungwa,
Kombe la Mapinduzi tumechukua.... Sasa nini tena.
Wacha tuVIMBE... msemaji Kasema
 
Yanga ni waungwana sana huwezi kumfunga mtu wakati kuna maombolezo
Sema utelembwe kwao wanaona ni big deal kwa yanga kutoa droo
 
Sare zitaendelea kuiandama yanga kama vile kwenye ushindi wa moja bila ulivyowaandama. Sasa ni mwendo wa kushangilia sare tu.
 
Ligi tunaongoza,
Ndo timu pekee hatujafungwa,
Kombe la Mapinduzi tumechukua.... Sasa nini tena.
Wacha tuVIMBE... msemaji Kasema
Umesahau mtaweka historia pia ya kumaliza ligi bila kufungwa lkn hamtachukua ubingwa.uto km uto
 
Soma hiyoooo
 
Kweli
 

Attachments

  • VID-20210214-WA0007.mp4
    2.1 MB
Back
Top Bottom