Sarkozy: Ulaya ndilo bara lenye ukatili na unyama mkubwa zaidi

Sarkozy: Ulaya ndilo bara lenye ukatili na unyama mkubwa zaidi

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Rais wa zamani wa Ufaransa ameitaja Ulaya kuwa bara lenye unyama mkubwa zaidi duniani, ambako vita vya kikatili zaidi hufanyika.

Nicolas Sarkozy, ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Baraza la Katiba la Ufaransa, amesema: "Hatuko katika Zama za Kati, bali katika karne ya 21. Tuko katika bara la Ulaya ambako mauaji ya kwanza ya umati yalifanyika; Ulaya ambako nchi zilipigana."

Sarkozy ameongeza kusema kuwa: Bara la Ulaya limekumbwa na ukatili, unyama na ushenzi. Ni ujinga kuona watu wakivitaja vita vya Ukraine kuwa ni janga, labda wamesahau vita vya Bosnia.

Mwaka mmoja umepita tangu vianze vita kati ya Russia na Ukraine, na nchi zinazoiunga mkono Ukraine, tofauti na madai yao ya eti kujali ubinadamu, bado zinaendeleza vita hivyo vya umwagaji wa damu kwa kuendelea kumimina misaada ya silaha na zana za kivita kwa serikali ya Kiev na kupuuza mapendekezo yote ya kusitisha vita hivyo.

Siku chache zilizopita Wizara ya Mambo ya Nje ya China iliwasilisha pendekezo lenye vifungu 12 vya mpango wa kurejesha amani nchini Ukraine, ambalo limekaribishwa na serikali ya Moscow, na kukabiliwa na majibu baridi kutoka kwa Marekani na Umoja wa Ulaya.

4bk38bcf4b7b6755ry_800C450.jpg
 
Achukue hatua aache kelele.
Huyu kipindi yupo Rais mwaka 2008 alikataa pendekezo la Bush kuwa Ukraine iingie NATO, Yeye na Angel Merker walipinga moango uo kwakuwaambia wenzao kabisa kitendo tunachofanya kuendelea kuingatia Urusi kitaondoa hali ya utulivu na Aman nchini Ukraine pamoja na mashariki yote ya ulaya, kwaneno hilo alilolitoa 2008 ndicho kinachotokea leo hii nchini Ukraine.
Screenshot_2023-03-19-09-26-19-31_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Madhalimu wa Dunia hii wanatoka Ulaya. Nenda nchi yeyote ile, unakuta wavamiaji katika nchi hizo au bara hizo walitokea Ulaya. Piga ua Ufalme wa Uingereza ndio namba moja!

Sarkozy hajakosea hata kidogo.
 
Back
Top Bottom