GE2025 Sasa CCM kipi kimewazuia kuzitimiza hizo ahadi zenu kipindi kilichopita mnakuja kuziahidi leo?

GE2025 Sasa CCM kipi kimewazuia kuzitimiza hizo ahadi zenu kipindi kilichopita mnakuja kuziahidi leo?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Kwa utashi tu wa kawaida, hizo ahadi mnazozitoa sasa hivi kipi kimewazuia kuzitimiza kipindi cha uongozi wenu kilichopita? Mnaanza kuahidi siku 100 za mwanzo baada ya kupita uchaguzi mtatoa ajira 7,000, sasa hizo ajira kipi kimewazuia kuzitoa kipindi kilichopita au kwanini msizitoa hata sasa hivi?

Au ndio hamna hoja mkaamua msitoe kwanza hizo ajira ili ndio mje mzitumie kama hoja kwenye hizi kampeni? Mnatutafakarisha sana, licha ya kuwa hamna wapinzani lakini nguvu mnayoitumia kwenye hizi kampeni mnasikitisha sana.

Kwako mtanzania anaekuambia siasa ni ,mchezo mchafu, mara kwenye siasa hamna kitu, basi wasingekuwa wanang'ang'ania kubaki huko, mpaka wanang'ang'ana kubaki huko basi kaa ujue huko ndiko kuna maisha.
 
Singida wataongezewa usikivu wa TBC.
Mbeya watapata taa barabarani.
Huku Dar sijasikia wakiongea lolote kuhusu mwendo kasi. Mabasi hakuna, miundo mbinu ipo ila uongozi umelala fofofo.
Kigoma wao wanasema hawamdai mama kwa hivyo hata wasichague mbunge sawa tu, au wanaweza kuteua hata mtoto wa darasa la nane akasinzie bungeni.
 
Back
Top Bottom