CCM kubalini yaishe japo mnasema Mapinduzi daima, kubalini kwa roho safi kabisa wala msiwe na kinyongo.
Ukiangalia CCM haina tena mvuto kiukweli huku mitaani achana na majukwaa, huku mitaani kila mtu ni CHADEMA mwaka huu.
Ona sasa CCM wamebaki na wasanii kwa kuwavalisha kofia kama kumbukumbu na agano, CCM wanajua bila ya wasanii hawatachua zaidi ya wiki mikutano yao itaanza kusinyaa na kuonekana ya ajabu, na wajaribu kufanya kampeni bila ya tamasha la bure, tuone kama wenyeviti nakuhakikishia watabakia na meza tu.
Mziki wa Chadema sasa unazidi kutapakaa nchi nzima kwa kasi ya ajabu, tunaona tume ya uchaguzi NEC inavyoanza kuwa kwenye taharuki kubwa kwani upepo umewabadilikia wanaona wazi kabisa CCM wanazidi kutengwa ikiwa ndio kwanza thekuthi moja ya kampeni inamaliza na wao weshafanya manyago.
Kampeni za Tundu Lissu zimeshaiteka nusu narobo ya ya Watanzania na kila anapokanyaga CCM wanazamishwa hilo lipo wazi,hatumii elimu ya wakata viuno wanaoletwa kwa makundi kwenye kampeni za Mgombea uraisi wa CCM wala hatumii malori mabasi na bodaboda wala hatoi petroli na dizeli bure kwa vyombo vya aina hio vinavyohudhuria, bali matumaini ya WaTanzania na kutaka kumsikiliza Rais mtarajiwa.
Tayari na ni wazi kabisa waTanzania wameshawekeza matumaini yao kwa Tundu Lissu, wamebakia wananchi wachache tu waliopo CCM ambao nao hawachezi tena mbali na matumaini yanayohubiriwa na kujengwa na CHADEMA
CCM kwa sasa mnajihangaisha bure tu tunaona nguvu mlizobaki nazo ni kuwavalisha kofia wakata viuno ambao hata wao wanajua wapi pa kuipeleka kura yao, hilo lipo wazi kwani nao wanawachukia kuliko maelezo, msizani wana maradhi ya kusahau, wasanii endeleeni na kuwatumbuiza CCM tupo pamoja kuimaliza kwenye sanduku la kura.
Ukijazia tena na kashfa kama hizi hapa ndio kwaheri CCM:
Steven Makigo ni Swahiba wa Rais John Pombe Magufuli... hawakukutana barabarani!! Hawa wamesoma pamoja Lake Secondary School.
Akiwa kama waziri wa ujenzi, mwaka 2012 JPM alimteua Steven Makigo kuwa Mjumbe wa TEMESA. TEMESA hii ni ile ile ambayo ilinunua boti kwa mabilioni ya pesa huku boti yenyewe ikiwa na speed sawa na mtumbwi!!
Ni boti ile ile ambayo, ili kuwakata watu midomo wasiijadili, JPM yule yule akaipeleka boti hiyo jeshini! Yaani, Jeshi linapewa boti yenyewe mwendo wa kinyonga!!!
REMEMBER: Zabuni ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato iliweka sharti kwamba Contractor
LAZIMA awe ni wa Kanda ya Ziwa!!
Yaani "National Project" inaweka condition ya ku-eliminate Watanzania wengine!!!!
Tena hapa tukumbushane kwamba, hiyo ni aina moja wapo ya Grand Corruption! YES, I mean it... a type of the GRAND CORRUPTION ambayo kwa makusudi watu wanaweka
baseless conditions only to eliminate other competitors in favor of their guy!!!
SO, Kuna atakayeshangaa tukisema Mradi wa ujenzi wa Chato International Airport uliletwa maalumu ili tenda apewe Mayanga Construction Ltd, and ONLY Mayanga?!
Halafu ngoja, nimekumbuka!!
Hivi mnakumbuka JPM enzi zake akiwa Waziri wa Ujenzi akaja na "Wakandarasi Wazalendo"?!
Hoja tamu kweli kweli ambayo mtu ukiitia doa utaonekana unapingana na mtu anayekusudia kuwainua Wakandarasi Wazalendo lakini ukweli ni kwamba hiyo ilikuwa ni janja janja nyingine ya kui-favor Mayanga Construction!!
Wakati Wizara ya Ujenzi chini ya Magu ilipokuwa na mpango wa kujenga Daraja la Mbutu, Magu alijua kabisa Mayanga hatakuwa na ubavu wa kushindana na kampuni za kigeni na ndipo likaja suala la Wakandarasi Wazalendo, na Mayanga Construction akala shavu akiwa na "wazalendo" wengine!!