Sasa CHADEMA ni Chama Tawala, ni suala la muda tu - ukweli ndio huo

Yaani hili jamaa limeaminishwa kwamba nenda tutakuja kukusaidia,linaongea kama lina majeshi mpe salam yeye ni kama punje ya sukari kwenye ndoo ya maji.
Sisi watanzania tutamchagua!Na kama sanduku la kura halitaheshimiwa basi tuko tayari kwa lolote!
 
Hahaha ni nchi ipi itakayokabidhiwa kwa chama kilichoshindwa kujenga ofisi ya chama kwa miaka 30 sasa.

Kwa shida za watanzania ni ofisi mbona CCM inazo ofisi nchi nzima na inawaletea wananchi umasikini tu kama maendeleo ya wananchi yangekuwa yanaletwa na uwepo wa ofisi nzuri za chama makaburu wasingeondolewa na ANC
 
Hata mimi nimeota kama niko kwenye starehe fulani Maisha ni bomba, Lisu na JPM wananipigia magoti, ilekuamka nikajikuta bado nipo bado kwenye utawala wa JPM na kazi zinaendelea, na Lisu naambiwa kaenda kusoma ulaya political science, na jinsi ya kuwasikiliza wenzake
 
Kofia zimevaliwa toka 1995 mfumo wa vyama vingi ulipoanza na CCM imeendelea kushinda kwa ushindi mnono. Mwaka huu kofia zinavaliwa na ushindi ni wa kimbunga.

Kama mme kuwa mnashinda kwa mazoea mwaka huu mnakwenda kupigwa za uso maana hata kwenye mikutano yenu mara wewe ni profesa nitakuteua kama nilivyomteua balozi masilingi kumbe ni sound tu balozi aliteuliwa na mtangulizi wake. Mgombea anaishiwa cha kujisifia hadi anapiga sound subirini 28/10 mwisho wenu nyie mbogamboga
 
Mazuri Maelfu Kwa kosa moja?

Tutazingatia wingi wa mazuri yake, nendeni mkamwambie mwenye urai Pacha kwamba, hatumtaki mtu ambaye anamashaka na nchi yake!

Kwamba haiamini? Kwamba anaweza kufanya atakavyo na kisha kukimbilia nchi yake mpaya siyo?

Watanzania tunataka haki uhuru na maendeleo ya wananchi siyo orodha ya mazuri ambayo hayagusi maisha yetu huku tunanyanyaswa tunatishwa hatuwezi kusema chochote sababu ya vitisho kila mahali hiyo orodha yenu ya mazuri iwasaifie kwenyebkumbukumbu zenu watanzania tumewachoka
 
Ukweli mtupu
 
Nani alikulazimisha uwe na cheti feki?
 

Ukijazia tena na kashfa kama hizi hapa ndio kwaheri CCM:

Steven Makigo ni Swahiba wa Rais John Pombe Magufuli... hawakukutana barabarani!! Hawa wamesoma pamoja Lake Secondary School.

Akiwa kama waziri wa ujenzi, mwaka 2012 JPM alimteua Steven Makigo kuwa Mjumbe wa TEMESA. TEMESA hii ni ile ile ambayo ilinunua boti kwa mabilioni ya pesa huku boti yenyewe ikiwa na speed sawa na mtumbwi!!

Ni boti ile ile ambayo, ili kuwakata watu midomo wasiijadili, JPM yule yule akaipeleka boti hiyo jeshini! Yaani, Jeshi linapewa boti yenyewe mwendo wa kinyonga!!!

REMEMBER: Zabuni ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato iliweka sharti kwamba Contractor LAZIMA awe ni wa Kanda ya Ziwa!!

Yaani "National Project" inaweka condition ya ku-eliminate Watanzania wengine!!!!

Tena hapa tukumbushane kwamba, hiyo ni aina moja wapo ya Grand Corruption! YES, I mean it... a type of the GRAND CORRUPTION ambayo kwa makusudi watu wanaweka baseless conditions only to eliminate other competitors in favor of their guy!!!

SO, Kuna atakayeshangaa tukisema Mradi wa ujenzi wa Chato International Airport uliletwa maalumu ili tenda apewe Mayanga Construction Ltd, and ONLY Mayanga?!

Halafu ngoja, nimekumbuka!!

Hivi mnakumbuka JPM enzi zake akiwa Waziri wa Ujenzi akaja na "Wakandarasi Wazalendo"?!

Hoja tamu kweli kweli ambayo mtu ukiitia doa utaonekana unapingana na mtu anayekusudia kuwainua Wakandarasi Wazalendo lakini ukweli ni kwamba hiyo ilikuwa ni janja janja nyingine ya kui-favor Mayanga Construction!!

Wakati Wizara ya Ujenzi chini ya Magu ilipokuwa na mpango wa kujenga Daraja la Mbutu, Magu alijua kabisa Mayanga hatakuwa na ubavu wa kushindana na kampuni za kigeni na ndipo likaja suala la Wakandarasi Wazalendo, na Mayanga Construction akala shavu akiwa na "wazalendo" wengine!!
 
Inatawala nini? Nyie endeleeni kujitoa ufahamu tu hakuna nchi ya kufanyia majaribio kwenye u ubunge tumeshawapima hamtoshi sasa urais tuwape kweli? Hapana jiimarisheni kwanza ndio pengine mtaweza kutushawishi lakini kwa sasa HAPANA.
 
Chadomo bana! Mnafikili kuchukua nchi ni kama kuokota dodo chini ya muembe!
 
Kawaida ya nyumbu kujiona salama mbele ya simba.

Pia sio vibaya kumpa moyo mgonjwa wa ukimwi so endeleeni kuota.
Hii ndio shida ya misukule ya lumumba akili zifuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…