Hayo ni maneno ya watu waliokuwa wamezoea kuishi kwa vipato vitokanavyo na shughuli za ujanja ujanja, ukwepa kodi, ufisadi, biashara haramu nk ambao awamu hii wameonja joto la jiwe na wako taabani. Mmoja wao ni mwenyekiti wenu ambaye amewakalilisha maneno hayo ambayo yamekuwa ndiyo sala yenu. Wamefyekelewa mbali na nchi yetu sasa uchumi unapaa kwa kasi ya ajabu. Ndani ya miaka mitano nchi yetu imetoka kutoka kuwa nchi masikini wa kutupwa duniani hadi nchi kuwa nchi tajiri za kati duniani sawa na nchi kama Afrika kusini na Nigeria. Sasa hivi sisi si omba omba tena. Tunatekeleza miradi mikubwa mikubwa ya mabillion ya dola kwa fedha zetu wenyewe, tena cash money!
Ni kanuni ya asili (the law of nature) kwamba matukio ya uhalifu (ulioutaja) kwenye nchi yo yote huongezeka jinsi utajiri unavyoongezeka (direct propotional). Hata kwa mtu mmoja mmoja wewe kama ni fukara hakuna jambazi lo lote litakalokuja nyumbani kwako usiku kukuvamia likiwa na silaha nzito nzito za moto. Ndiyo maana nchi kama ya Marekani ndiyo inayoongoza duniani katika matukio ya uhalifu wa aina hiyo. Kwa bara la Afrika nchi za South Africa na Nigeria ndizo zinazoongoza. Tanzania ndiyo inaongoza barani Afrika kwenye orodha ya the most peaceful countries. Hayo matukio ya uhalifu uliyokaririshwa yalishadhibitiwa kwa kiwango kikubwa na mengi yake yalikuwa na mkono wa chama chenu. Majambazi ya kutumia silaha hayatambi tena maana huwa tunayalaza haraka haraka. Maghaidi ya Al Shabah na washirika wao wa Upasho hawathubutu kuichezea nchi yetu kama ambavyo wanaichezea nchi ya Kenya. Jiwe huwa hajaribiwi na watu au makundi ya watu wa design hii!