Sasa hizi selection za kidato cha tano (form five) na vyuo zitatoka mwezi wa sita au?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Inashangaza mpaka sasa tukiwa tunauendea mwezi wa tano bado tu wakati inafahamika fika kuwa kunakuwa na gharama kibao.

Pamoja na kufuta ada, lakini kwa utitiri wa michango iliyopo advance mzazi itamgharimu si chini ya laki tatu (300,000/=) kuweza kumpeleka mtoto shule. Kiasi hiki ni kichekesho kwa wengi wenu humu lakini, amini nawaambia, ni kiasi kikubwa sana kwa wazazi wengi waliopo huko vijijini.

Kukipata hicho kiasi, inamlazimu mzazi kulima kibarua cha ekari kibao tu. Ikumbukwe pia, hiko ndo kipato cha juu cha mwaka kwa wakulima wengi tu.........Mungu mkubwa na wa ajabu, sote tunaishi na tunakutana kwa Mangi kukopa unga.

Kuwasaidia hawa, infekuwa busara kutoa hizo selection mapema zaidi kwa nafasi ya kutosha zaidi ya kujiandaa........mwezi wa nne ingependeza zaidi. Nasikia shule zinafungwa tarehe 31.05.2023, maana yake ni kwamba tayari muhula umeshaisha na ikumbukwe kuwa zinapofunguliwa basi na haaa form 5 inabidi wakafungue pamoja.
 
Kwanza sio utitili wa michango, ukiona ni mingi mpeleke private, wa Tz hatuna shukran na tunaongoza kwa kuzaana pia tunapenda kitonga ,
We andaa ela weka kibundoni, kama itakua tofaut unaitumia kwa matumizi mengine
 
Kwa vile sio suala la ghafla wazazi wajiandae kabisa waweke kwenye tigo pesa
 
We
Kwanza sio utitili wa michango, ukiona ni mingi mpeleke private, wa Tz hatuna shukran na tunaongoza kwa kuzaana pia tunapenda kitonga ,
We andaa ela weka kibundoni, kama itakua tofaut unaitumia kwa matumizi mengine
Boya acha ujinga watu wako village hawana hata elfu hamsini alafu unaandika ujinga
 
Inashangaza mpaka sasa tukiwa tunauendea mwezi wa tano bado tu wakati inafahamika fika kuwa kunakuwa na gharama kibao.

Pamoja na kufuta ada, lakini kwa utitiri wa michango iliyopo advance mzazi itamgharimu si chini ya laki tatu (300,000/=) kuweza kumpeleka mtoto shule. Kiasi hiki ni kichekesho kwa wengi wenu humu lakini, amini nawaambia, ni kiasi kikubwa sana kwa wazazi wengi waliopo huko vijijini.

Kukipata hicho kiasi, inamlazimu mzazi kulima kibarua cha ekari kibao tu. Ikumbukwe pia, hiko ndo kipato cha juu cha mwaka kwa wakulima wengi tu.........Mungu mkubwa na wa ajabu, sote tunaishi na tunakutana kwa Mangi kukopa unga.

Kuwasaidia hawa, infekuwa busara kutoa hizo selection mapema zaidi kwa nafasi ya kutosha zaidi ya kujiandaa........mwezi wa nne ingependeza zaidi. Nasikia shule zinafungwa tarehe 31.05.2023, maana yake ni kwamba tayari muhula umeshaisha na ikumbukwe kuwa zinapofunguliwa basi na haaa form 5 inabidi wakafungue pamoja.
Ndugu yangu hili taifa Lina watendaji wapumbavu mpaka ukiwaza unachanganyikiwa !!! Leo tunaenda mwezi wa sita hakuna selection shule zinafunguliwa mwezi wa Saba hatujui watapangiwa wapi!! Gharama za maisha zipo juu!!! Wao wanadhani tuna mishahara kama wao!!
 
Back
Top Bottom