Sasa huyu Bashe kamsaidia mkulima au kamuangamiza? Huu mchele wa Ruzuku unaweza kuuzwa 1,500/- kwa kilo

Sasa huyu Bashe kamsaidia mkulima au kamuangamiza? Huu mchele wa Ruzuku unaweza kuuzwa 1,500/- kwa kilo

Wabongo tuna tabu sana. Maana hata hatujui tunataka nini hasa...

Mchele ukipanda bei tunalalamika, na ukishuka bei tunalalamika...
Mkuu
Mbona Umekigeuka Chama Sasa Hivi, Unapingana Na Ilani Iliyosema Kilogram Iwe Tshs 10000/=
Tatizo siyo mtoa mada bali akili yake imeshindwa kuchambua hadha ya kufichwa chakula, ugumu wa kupata mlo na wepesi wa kupata mlo.

Huyo huyo anaanzisha uzi 'mchele shs 3800kg bashe hafai' leo anaanzisha uzi 'Bashe anaangamiza mkulima' yaani ni hajui au anajifanya kusimama kati asionekane mpinzani.

Anang'ata na kupuliza!.
 
Tulikokuwa tunaelekea mchele Kg ilikuwa ufike 5K kwa sababu matumizi home huwa nanunua kila baada ya wiki mbili ila ndani ya hii miezi miwili nilikuwa kila nikienda imeongezeka Tsh 300/700.

Ila vizuri zaidi wangewawezesha wakulima walime kwa wingi kila mkoa hali ingetulia.
 
Tatizo siyo mtoa mada bali akili yake imeshindwa kuchambua hadha ya kufichwa chakula, ugumu wa kupata mlo na wepesi wa kupata mlo.

Huyo huyo anaanzisha uzi 'mchele shs 3800kg bashe hafai' leo anaanzisha uzi 'Bashe anaangamiza mkulima' yaani ni hajui au anajifanya kusimama kati asionekane mpinzani.

Anang'ata na kupuliza!.
Wewe ndio huelewi

Bashe kashindwa kutengeneza Win Win situation kwa mkulima na Mlaji
 
Ninavyowajua Watanzania wanapenda vitu vya bei rahisi Bila kuzingatia ubora

Hiyo michele iliyofichwa na Wakulima soon inaenda kuwadodea

Bashe ajipime kama anatosha!
Watawauzia walanguzi nao watauza nje Kama wanavyofanya sasa
 
Kilichotokea Zanzibar siku chache baada ya raisi Mwinyi kukutana na wafanyabiashara na kuwataka waagize mchele mwingi.

Siku chache baadae walioficha stock wakaanza kutafuta mbinu za kuuleta bara, maana wanajua soon shehena zikianza kuingia huko ndio mwisho wa biashara yao ya ulanguzi.

Na hapa soon watu wanaohodhi bidhaa za chakula watakiachia tu. Hawa ndio watu Bashe alikuwa anawalinda sio wakulima.
 
Back
Top Bottom