JERUSALEM 2006
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 527
- 596
Haujambo mwana Jf? Mimi ni mzima buheri wa afya, namshukuru Mungu kwa ulinzi wake na kunipa uhai mpaka sasa. Moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo.
Tangu kifo cha Rais wa awamu ya Tano , Hay. Dkt. John P. Magufuli, kama taifa tumepita kipindi kigumu sana hasa kwenye katiba yetu. Katiba yetu imejaribiwa na imejaribika. Kuna msemo unasema "acha inyeshe tuone panapo vuja". Hakika tangu kutungwa kwake mwaka 1977 na marekebisho yake mbalimbali bado kumekuwa na hitaji kubwa sana kutoka kwa wadau wengi waki 'demand' katiba mpya. Mhe, rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya M. Kikwete alijaribu kuanzisha mchakato huu wa katika katika awamu yake ya pili(2010-15) bila mafanikio yoyote, na kupelekea kelele hizo kuzimwa na mrithi wake.
Bila kumung`unya maneno, Hay. Dkt. Magufuli hakuwa muumini wa katiba mpya. Na wala hakuamini sana katika utawala wa sheria, yeye aliamini katika utashi binafsi na maamuzi ya kiimla huku akijitanabaisha kama mtu pekee anayeweza kusongesha mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Kwa sehemu kubwa alifanikiwa hasa kwenye ujenzi wa miundombinu ya nchi na kurudisha nidhamu ya kiutumishi na kijamii kwa ujumla. Katika kutekeleza majukumu yake, aliumiza kundi kubwa la watu kutokana na maamuzi aliyo yatekeleza kwa kutumia dhamira ya ndani kama mbadala wa sheria.
Kama taifa hatuwezi kuendelea kutegemea utashi wa mtu binafsi,kuna somo kubwa tumejifunza na tuko tayari kusonga mbele pamoja, ikiwezekana kuanza upya. Nashauri vuguvugu la kutaka katiba mpya lianze upya kwa nguvu ile ile ya mwaka 2010 baada ya uchaguzi mkuu. Natoa rai kwa wadau wote wa katiba mpya kushiriki katika kushinikiza mchakato huu. Tusiwaachie wanasiasa pekee, bali nyanja zote za taaluma zishiriki, makundi yote ya kijamii, makabila yote na watu wa rika zote.
Kuna mambo mengi sana tunaweza kuyajadili kuhusu katika katiba mpya, mimi nitajadili mambo matatu tu. Naomba tutumie uzi huu kuorodhesha mambo tunayodhani ni muhimu kuyaangalia upya ikiwezekana kuyabadili ili kuleta tija katika taifa letu. Hii iwe sehemu ya kushinikiza mamlaka ya Urais kukubali kuendeleza mchakato wa katiba mpya au kuanza upya.
Mambo ma(3) yafuatayo yamepitwa na wakati na nadhani ni muda sahihi kama taifa kuyaangalia upya.
1. Mamlaka ya Urais ni kubwa mno, apunguziwe majukumu hasa ya uteuzi.
Katiba yetu ya J.M.T ya 1977 kuanzia ibara ya 33 mpaka ibara ya 46 inazungumzia kwa mapana mamlaka ya urais wa taifa letu. Kwamba ndiye Amir Jeshi Mkuu, Mkuu wa nchi na Kiongozi Mkuu wa Serikali. Rais anamamlaka kubwa sana ya Uteuzi na utenguzi kuanzia kwa Mawaziri, majudge, wabungu(10), Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Wakuu wa taasisi zote za serikali, Wakuu wa kurugenzi nyeti za serikali, Wenyeviti wa bodi za taasisi zote za serikali, Wakuu wa mikoa, Makatibu wakuu, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa halmashari za kiutawala, Makatibu tawala wa mikoa , Mabalozi, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, Msajili wa vyama vya siasa, Katibu mkuu wa bunge, Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG), Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) , Mwanasheria Mkuu wa serikali, Wakili mkuu wa serikali n.k n.k.
Mamlaka ya uteuzi ya Rais ni kubwa mno. Hana tofauti na mfalme , hakuna sababu zozote kwa nini Rais apewe mamlaka kubwa hivi.
Ushauri wangu kwenye hili;
A. Viongozi wote wa kisiasa kama wakuu wa mikoa na wilaya, mamlaka ya uteuzi ibaki kwa wananchi. Yaani wachaguliwe moja kwa moja na wananchi, na wananchi wapewe mamlaka ya kuwaondoa pindi wasiporishwa na utendaji wao.
B. Viongozi wote wa Bunge na Mahakama wasichaguliwe na Rais hata kidogo. Wananchi wapewe mamlaka ya kuwachagua viongozi hawa kupitia kwa wawakilishi wao yaani wabunge.
C. Viongozi wote wa Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya siasa wachaguliwe moja kwa moja na wawakilishi wa wananchi kupitia utaratibu utakao wekwa na Bunge la katiba.
D. Wakurugenzi na Makatibu tawala wa mikoa wateuliwe moja kwa moja na waziri wa TAMISEMI ili kumpa waziri husuka mamlaka ya moja kwa moja kwa viongozi hawa.
2. Muungano wetu Kati ya Tanganyika na Zanzibar
Ibara ya 1 na ya 2(1) za katiba ya JMT ya mwaka 1977 inatamka wazi kwamba, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muungano wa nchi mbili za Tanganyika( Tanzania Bara) na Zanzibar. Lakini pia ibara ya 4(3) imeoroshesha mambo 21 ya muungano. Hapa ndugu zangu kuna shida, na kama taifa lazima tukubaliane yafuatayo.
A.Je, Bado tunahiji kuungana kwa sababu zile zile zilizotufanya tuungane 1964?
B.Na kama Jibu ni 'Ndio' ni aina gani ya muungano utatufaa kwa mazingira yetu ya sasa?
Hapa panahitajika mjadala mrefu na wawazi, ili kuondoa sintofahamu zote zilizopo kwenye muungano wetu na kuuboresha zaidi kama tutakubaliana kuendelea kuungana.
3. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Ibara ya 74 ya katiba yetu ya mwaka 1977 inaeleza kuhusu tume ya taifa ya Uchaguzi. Kimsingi Rais amepewa mamlaka yote ya uteuzi na utenguzi kuanzia kwa mwenyekiti mpaka wajumbe wote wa tume hii. Rais pia amepewa mamlaka ya kumteua mkurugenzi wa tume ya uchaguzi. Hapa kuna shida kweli kweli.
Kama taifa tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Yaani, rais asiwe na uwezo wowote au ushawishi wowote juu ya watendaji wa tume hii. Wawakilishi wa wananchi na mahakama zihusike moja kwa moja kuteua mwenyekiti na wajumbe wake baada ya kupokea maombi ya kazi kutoka kwa wahusika.
Ndugu wana Jamvi, nimechokoza mada tu, natambua mjadala huu sio mgeni, lakini mpaka tutakapo ipa serikali shinikizo/pressure ya kutosha, hakuna atakaye jitingisha kuhusu katiba mpya. Katiba ya mwaka 1977 sio zao la wananchi, tuna demand katiba ya wananchi. Kuna watakao sema katika haileti maendeleo, msiwasikilize hao, tutumie mwanya huu wa sasa kuitaka katiba mpya kwa mbinu zote ikiwemo majadiliano kama haya.