chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Mrisho Gambo sasa anatakiwa kula chakula alichowalisha wenzake kwa muda mrefu sana, chakula chenye sumu ya fitna. Katika foleni, hakuna aliyebaki isipokuwa ni yeye, na mgawa chakula anamuangalia usoni kwa macho pima akiwa na upawa uliojaa chakula, gambo akiwa na sahani yake mbele ya mgawa chakula.
Katika utumishi wake Gambo kaumiza watu kwa staili yale ya siasa za uongo na fitna. Katika barabara ambayo hakujua kama ataelekezwa arudi kuipitia, alijaza miiba mingi ambayo sasa analazimika kuikanyaga ili apite.
Kakutana na Mkuu wa Mkoa-Makonda ambaye pia fitna ni sehemu ya siasa zake, na anaweza kumchekecha vilivyo na asikemewe. Je kama Mkuu anajua mambo ya ndani ya mpango wa chama kwamba kinaweza na kiliweza kuishi bila Arusha, wakamuachia yule mkimbizi ajiponye kiuchumi? Mbona chama kiliishi bila Mbeya, Iringa na Arusha? Seuze 2025-2030
Ila kwanza Gambo akionje kikombe alichowaonjesha wenzake enzi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, na baadae Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na baadae mbunge wa Arusha.
Ushauri wangu kwake, aanze kuondoa vitu vyake binafsi pale ofisi ya mbunge, na aanze safari rasmi ya kuwaaga wana Arusha.