Elections 2015 Sasa naanza kupata picha kwamba Apson Mwang'onda yupo kwa Lowassa kikazi zaidi...

Hapa nitoe pongezi kwa ndugu yetu Consigliere kwa maono ya mbali, naweza amini sasa upo ndani ya kampuni.

Mkuu nachelea kupokea pongezi zako sababu ya neno hili kwenye Kijani, ni taaluma na kazi za watu hizo. Mimi sijui hata 'a' yake inaandikwaje.
 
Aisee yametia kabisa watu ni mikakati yao tena wanatumia watu wa karibu yako.
 
Jieleze vizuri. Mara unaunga unga kiingereza, mara kiswahili. Nyoosha lugha yako na maneno yako.
 
Au wewe ndiyo Pacha wa Pasco wa JF? Sijui mlioteshwa sawa au imetokea tu kama ya Sheick Kipozeo?

Nilishaongea na jamaa mmoja ambaye na yeye aliachwa kwenye mataa ya Apson. Huyu jamaa ni hatari sana.

Ukiangalia alivyokuwa karibu na Lowassa, alikuwa anajua kila kitu na nadhani hili walilitumia kumtisha Edo.

Sasa hivi atatengwa na wote maana kila mtu ataogopa kushikamana naye. CCM kuna unafiki sana.
Sinyooshi!!
 
Last edited by a moderator:

huwezi ukabisha kuwa ww si sehemu ya hiyo Idara, nakumbuka nilikuwa mtu wa kwanza kusoma hii post nikiri niliona hili ni gumu kutokea kwa sababu ya nguvu alizokuwa nazo EL na mazingira halisi.
Ila kwa hali ilivyotokea DoDoma na hili andiko lako hakuna tofauti
na katika hili JK pamoja na mapungufu yake yote yaliyowahi tokea Watanzania wazalendo hawatamsahau kajijengea heshima kubwa sana kwa kitendo kile tu alichokifanya Juzi.
Ameonyesha kwamba yeyote yule atakaepewa cheo akafanya kazi kwa bidii, maarifa, na uzalendo bila ya kuwa na tamaa ya wizi,,, iko siku anaweza kuwa kiongozi mkubwa wa nchi hii.
 
Je mnaweza kutuambia kwa nini Wagombea Uraisi wa CCM kama ni Wakiristo basi wote ni Wakatoliki?
Je Jaji Augustino Ramadhani aliyesheheni ma CV kibao mchungaji wa Kanisa la Kiprotestanti imekuwaje amekatwa hata kwenye tano bora hayumo?
 

Mkuu, hayo mengine siyajui. Ila hili la juzi Kikwete alitaka awekee 'TV' yake pale Ikulu halafu astaafu na remort akiwa nayo yeye. Kikwete hana cha kujivunia, hata ukikutana naye ukampongeza atahisi unamng'ong'a tu na atakachokufanya hutataka kusimulia.
Ukweli ni kuwa Magufuli hakuwemo hata kwenye tano bora ya awali bali mashinikizo ya watu kuhoji na kutishia kuwang'oa wote wakianza na yeye ndipo Ben alipoicheza karata ya Magufuli. Kwa kifupi Kikwete anaondoka na machozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…