Sasa nataka kuoa.

Sasa nataka kuoa.

Unajua mi sijaweza kuelewa hii staili ya kutafuta wachumba kwenye mitandao mi nadhani kama muda wa kuoa au kuolewa unafika pale unapompata mtu mnaanza urafiki uchumba then unaoa lakini usikurupuke tuu kwa kutangaza unataka kuoa unaoa nini sasa maneno! muombe mungu wako akupe mke mume mwema...naboreka sana kuona thread watu wanatoa humu na kuweka masharti ya nataka hiki nataka kile...kwa hiyo wasio na hizo sifa hawataolewa au kuoa achen hizo bana...muda wako ukifika hutakuw na hata haja ya kuesma ni hayo tuu kwa leo...
mwenzi anapatikana popote,kanisani,masijid,bar,shuleni,kwenye mziki nk
 
Mwenye nia tuwasiliane.Si vizuri kufundishana namna ya kuchagua.
 
Nimekuwa mtazamaji na mchangiaji katika jukwaa kwa muda sasa.Lakini ombi langu kwa leo nadhani umefika muda niseme kwamba nahitaji mke.Sifa zifuatazo zinahitajika.Mzuri wa haja,mweusi(si kama Idd Amini),mwenye urefu wa wasitani,asiyependelea vileo,mwenye kiu ya maendeleo, MCHA MUNGU,asiwe ni ndiyo mzee(she must be critical),awe mfanyakazi kwa kujiajiri au kuajiriwa (lakini si mwanasheria),Umri walau kuanzia miaka 23 mpaka 25.La muhimu zaidi asiwe mwanasiasa.Karibuni.

hujataja awe amepitiwa na wanaume wagapi! au hiyo haipo?
 
Nimekuwa mtazamaji na mchangiaji katika jukwaa kwa muda sasa.Lakini ombi langu kwa leo nadhani umefika muda niseme kwamba nahitaji mke.Sifa zifuatazo zinahitajika.Mzuri wa haja,mweusi(si kama Idd Amini),mwenye urefu wa wasitani,asiyependelea vileo,mwenye kiu ya maendeleo, MCHA MUNGU,asiwe ni ndiyo mzee(she must be critical),awe mfanyakazi kwa kujiajiri au kuajiriwa (lakini si mwanasheria),Umri walau kuanzia miaka 23 mpaka 25.La muhimu zaidi asiwe mwanasiasa.Karibuni.

OKK....ila kaka inabidi upunguze masharti...au uwe flexible..
1. Kazi vs Umri : Ume-overlook fact ya kwamba wa-dada wengi katika hiyo age ndio either wapo chuo au wanatafuta kazi...au ndio wameanza....pengine ungesema mtu mwenye potential future.....
2. Criticism vs poltics : Mtu mwenye challenge lazima atakuwa anajua siasa kwa hiyo u either choose one...
3. Ulibwende vs Tabia??
4. Profile yako........naamini kuoa/kuolewa ni 2-way tarffic....so jichambue nawewe as weakness na sifa

Ushauri: Fanya mpango wa arranged marriage itakufaa zaidi....unaweza fanya over internet (cna hakika hapa nyumbani kama ni formal service) au kijijin kwenu ukawaambia wakutafutie mke...lol..
 
Kiukweli bado hujawa tayari kuoa mtu anayetaka kuoa unajulikana sababu mke ni zaidi ya vigezo vyako ulivyo vitaja, mke sio kama gari kusema nataka toyota nyeupe model fulani automatic milango 6 iwe na.................................... muda wako ukifika au utaita watu kwenye vikao au sherehe ya harusi na sio kututangazia vigezo kama unatafuta mfanyakazi wa kuajiri,
 
...Try the 'Missing Person' Department at a nearby Police Station.
 
Back
Top Bottom