Sasa ni muda muafaka wa maridhiano Tanzania

Sasa ni muda muafaka wa maridhiano Tanzania

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
3,337
Reaction score
5,876
Maridhiano ni muhimu sana baada ya zile vurugu za Oktoba 29.

Mjumbe wa Jumuiya ya madola-Chakwera yupo nchini kutafuta maridhiano. Isije kutokea upande wowote ukakwamisha maridhino kwa tamaa ya madaraka. Pia, isije kutokea Lisu akabezwa kukubali maridhiano.

Hii ni kwa sababu huu mkwamo hauwezi kuisha bila maridhiano kutokana na asili ya upande wa pili kutokuwa tayari kujiuzulu.

Kupitia maridhiano chini ya usimamizi wa jumuiya ya madola angalau tunaweza kupiga hatua hata chache kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli chanya katika uendeshaji wa siasa zetu.

Ni bora kuridhiana chini ya usimamizi wa jumuiya hii ya madola angalau inaweza kusaidia yale mapungufu yanayopigiwa kelele kufanyiwa kazi kwa sababu hata hao kina Chakwera wataona hoja za wapinzani zina mashiko na labda upande wa chama tawala wataona aibu.

Maridhiano yana faida sana kwa sababu tutaweza kuishi kwa umoja na mshikamano kama taifa.

Kule Kenya walivurugana sana mwaka 2007 na baadae wakafanya maridhiano. Itakuwa maajabu Tanzania tushindwe kufanya maridhiano ikiwemo kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kama ilivyo Malawi. Watu wanapiga kura chini ya mti peupe pee kila mtu anayaona maboksi na uhesabuji wa kura.

Nchi zilizostaarabika hakuna machafuko baada ya uchaguzi kwa sababu kunakuwa na mazingira mazuri ya ushindani kwa kila upande. Kwa nini huku Afrika tunapenda kufanyiana wizi na figisu katika uchaguzi?

Tafadhali, wanasiasa msitangulize maslahi yenu ya kulinda ulaji wenu na kupuuza maslahi ya wananchi.
 
Maandamano hayakua ya chadema maridhiano hayawahusu
Unajua tukiendelea kuficha tatizo wakati lipo hatutafika. Ukweli ni kwamba, hauwezi kufanya maridhiano Tanzania bila kuihusisha CCM na CHADEMA. Watanzania wengi wapo CCM kimaslahi lakini Watanzania wanaotaka mabadiliko wapo CHADEMA.
 
Watanzania wengi wapo CCM kimaslahi lakini Watanzania wanaotaka mabadiliko wapo CHADEMA.
 
Back
Top Bottom