sasa ni rasmi: babu wa samunge ni bilionea!!

Ms Judith

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2010
Posts
2,563
Reaction score
929
Hesaabu zenyewe ziko hivi:

Hadi leo amehudumia watu 3,000,000/- x 500 = 1,500,000,000/-!!

Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo

Na Mwandishi wetu

ZAIDI ya wagonjwa milioni 3 wamepata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila ‘Babu’ katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro tangu aanze kutoa huduma hiyo Agosti mwaka jana.

Takwimu zilizotolewa jana na mmoja wa wasaidizi wa Babu, Jackson Dudui, zinaonyesha bado wanategemea idadi kubwa ya wagonjwa kuendelea kumiminika kijijini hapo kufuata kikombe hicho kinachotibu magonjwa sugu na kwamba juzi pekee wagonjwa 17,065 walipata huduma hiyo.

Magonjwa sugu yanayodaiwa kutibiwa na kikombe hicho kinachokwenda na imani zaidi ni kisukari, shinikizo la damu, pumu, saratani na ukimwi.

Alisema jana magari zaidi ya 400 yenye wagonjwa zaidi ya 3000 yalikuwa yakimsubiri Mchungaji Mwasapila atoke kanisani, ili awapatie tiba hiyo mbadala ambapo alieleza raia kutoka Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi kijijini hapo.

“Foleni ya magari si kubwa sana kwa siku ya leo kwani hivi tunavyozungumza yapo magari zaidi ya 400 yakimsubiri Babu atoke kanisani na kuanza kuwahudumia kuanzia saa 8 mchana na hakika atawamaliza leo hii,” alisema.

Msaidizi huyo alisema kuwa katikati ya wiki iliyopita walipata ugeni wa wachungaji zaidi ya 10 kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati waliokuwa kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano wao mkuu wa mwaka wakiongozwa na Mkuu wa Jimbo aliyetajwa kwa jina moja la Nangole.

Alisema mbali na wachungaji hao kushiriki mkutano huo waliungana na Babu kutoa vikombe kwa wagonjwa waliokuwepo kijijini hapo kupata tiba hiyo.

Habari zaidi zilizopatikana zimeeleza kuwa Babu amepiga marufuku wagonjwa kutoka Kenya wanaosafirishwa kutumia magari yasiyoruhusiwa kama malori na gari ndogo ‘saloon’ wakiwa wamejazana hali aliyosema ni mateso kwa wagonjwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alieleza kuwa utoaji tiba unaendelea vizuri kijiji hapo, na alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa ukusanyaji ushuru wa magari na helikopta alisema hayo ni mambo ya kisiasa zaidi na kumtaka mwandishi wa habari hizi kusubiri maamuzi ya kikao halali kitakachofanyika leo kijijini hapo.

Alisema bado maamuzi hayajafikiwa kujua ni mamlaka ipi itakayokuwa ikikusanya ushuru huo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngoromngoro na serikali ya kijiji cha Samunge.

“Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuzungumzia suala hilo naomba usiandike chochote kwani kesho kutakuwa na kikao kitakachozungumzia suala hilo na tutawapeni taarifa,” alisema.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mgogoro wa kugombea ushuru wa magari na helikopta kati ya pande hizo na wakati fulani iliripotiwa kuwa serikali ya kijiji iliwafukuza watoza ushuru toka halmashauri.

source: Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo
 
Hongera babu....atajenga kijiji kiwe mji!
 
kama sii yeye vodaacom na airtell wangetinga humo? wilaya ingepata mapato? samunge ingejulikana? nani anafaidi zaidi?
 
Subiri wakati wa mgao!hapa ndio tutasikia babu kaua wangapi!
 
Dah kwa sasa hivi nikisia habari za babu nasikia uchungu kweli. Anko wangu akiuguliwa na figo ,yupo nachingwea,alivyoona hali si shwari ikabidi aanze safari ya muhimbili. Wakati yupo mtwara kabla hajapanda ndege kwenda daslam, habari za bau zikamkuta hapa,akashawishika,akakata tiket nyiingine hadi Arusha-samunge...baada ya kupata kikombe akarudi zake na amani kabisa kajua kwamba kapona. mwezi na ushehe umepita sasa anataabika kweli hadi juzi nimepata simu ananiomba nimpe details za matibabu India, hali yake si mzuri kabisa na sasa anafanya utaratibu aende india akafanye matibabu ya figo.
Najua watu watasema mambo ya imani n.k lakini tiba yake hadi hivi leo ni kizungumkuti, na magumashi. yaani haieleweki kabisa.!!
 
pole zake anko na familia yake na nyie nduguze wa karibu mnaomuuguza.

hapa JF,

ukipona=tiba ya babu ni ya kweli
usipopona=huna imani
ukifa kwa ugonjwa uleule uliotibwa na babu=babu hazuii kifo
gharama ya 500/=hizo ni ndogo sana ukilinganisha na akina ndodi (ingawa zimemfanya bilionaire ndani ya miezi michache)
nk
nk

mmh, ngoja niishie hapa wapenzi wake wasije wakanivamia hapa nikaharibu maombi yangu bure.

amani iwe kwenu

Glory to God
 
Jambo lilijema kwa binadamu ni kifo chake tu.
Sijasikia mtu akilalamika baada ya kufa.
 
pole zake anko na familia yake na nyie nduguze wa karibu mnaomuuguza.

hapa JF,

ukipona=tiba ya babu ni ya kweli
usipopona=huna imani
ukifa kwa ugonjwa uleule uliotibwa na babu=babu hazuii kifo
gharama ya 500/=hizo ni ndogo sana ukilinganisha na akina ndodi (ingawa zimemfanya bilionaire ndani ya miezi michache)
nk
nk

mmh, ngoja niishie hapa wapenzi wake wasije wakanivamia hapa nikaharibu maombi yangu bure.

amani iwe kwenu

Glory to God

Dah umenena vema sana Miss Judith...we subiri akina pakaJimmy waje..utawasikia tu!!
 
Yaani Miss alivyomshupalia Babu we acha tu. Kanisa lile waumini wake wangetoa sadaka ya mia 500 kila wakienda kusali saa hii wasingepiga kelele.
Poleni kwa hilo lakini hakuna wa kumzuia tena ndo imetoka hivyo.
Yule DJ wa pale temeke mbona alipofungua kanisa na kuwaambia dhahabu ni za kishetani hamkumhoji. Mbona hamhoji mapato yake!
Unajua mke wa mganga wa kienyeji kazoea kula kuku wa kijani! wa bluu nk sasa hakuna wenyekupeleka kuku shida kweli kweli!
 
pole zake anko na familia yake na nyie nduguze wa karibu mnaomuuguza.

hapa JF,

ukipona=tiba ya babu ni ya kweli
usipopona=huna imani
ukifa kwa ugonjwa uleule uliotibwa na babu=babu hazuii kifo
gharama ya 500/=hizo ni ndogo sana ukilinganisha na akina ndodi (ingawa zimemfanya bilionaire ndani ya miezi michache)
nk
nk

mmh, ngoja niishie hapa wapenzi wake wasije wakanivamia hapa nikaharibu maombi yangu bure.

amani iwe kwenu

Glory to God
Ishu zako za kuolewa vp?
 
Dah kwa sasa hivi nikisia habari za babu nasikia uchungu kweli. Anko wangu akiuguliwa na figo ,yupo nachingwea,alivyoona hali si shwari ikabidi aanze safari ya muhimbili. Wakati yupo mtwara kabla hajapanda ndege kwenda daslam, habari za bau zikamkuta hapa,akashawishika,akakata tiket nyiingine hadi Arusha-samunge...baada ya kupata kikombe akarudi zake na amani kabisa kajua kwamba kapona. mwezi na ushehe umepita sasa anataabika kweli hadi juzi nimepata simu ananiomba nimpe details za matibabu India, hali yake si mzuri kabisa na sasa anafanya utaratibu aende india akafanye matibabu ya figo.
Najua watu watasema mambo ya imani n.k lakini tiba yake hadi hivi leo ni kizungumkuti, na magumashi. yaani haieleweki kabisa.!!
Hata dawa ya malaria mseto(ambayo inadaiwa kuwa ya kisasa kabisa) kuna baadhi ya watu inawadhuru, wengine haiwaponyi kabisa, wengine inaweza kuwasababishia kifo!
Kwahiyo kwa kulinganisha tu, mjomba wako ni percentage ni 0.0000000000001 ya watu WALIOTIBIWA na babu na kupata complication hiyo!
Na huenda kuna masharrti alikiuka!
kWAHIYO bWANA sizinga, acha upotoshaji, acha watu wasafiri kwenda SAMUNGE, dawa ya babu inaponya, na hii ni kwa mujibu wa HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI!
Hata hivyo namtakia MJOMBA wetu AFYA NJEMA!
 
Dah umenena vema sana Miss Judith...we subiri akina pakaJimmy waje..utawasikia tu!!

Judith hana jipya, na kilichobaki sasa anatafuta umaarufu kwa kushika mashati watu!
Sijui ishu yake ya kumuoa yule kijana imeishia wapi, mshauri amalizane kwanza na ile!

Actually kwa habari hii amemtangaza sana babu kuwa tiba yake ni ya uhakika, ndiyo maana watu hawataacha kwenda huko!
NAMSHUKURU mISS jUDITH KWAHILO!

Ila hesabu za kitoto alizofanya pale kwenye orijino thread yake zinachekesha, maana haikuwa na sababu ya kuziweka, ni uzushi wake tu na kukuza bifu lake na babu, kitu ambacho hawezi kufanikiwa!
POLE ZAKE!
 
hesaabu zenyewe ziko hivi:

hadi leo amehudumia watu 3,000,000/- x 500 = 1,500,000,000/-!!

Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo

na Mwandishi wetu

ZAIDI ya wagonjwa milioni 3 wamepata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila ‘Babu' katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro tangu aanze kutoa huduma hiyo Agosti mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa jana na mmoja wa wasaidizi wa Babu, Jackson Dudui, zinaonyesha bado wanategemea idadi kubwa ya wagonjwa kuendelea kumiminika kijijini hapo kufuata kikombe hicho kinachotibu magonjwa sugu na kwamba juzi pekee wagonjwa 17,065 walipata huduma hiyo.
Magonjwa sugu yanayodaiwa kutibiwa na kikombe hicho kinachokwenda na imani zaidi ni kisukari, shinikizo la damu, pumu, saratani na ukimwi.
Alisema jana magari zaidi ya 400 yenye wagonjwa zaidi ya 3000 yalikuwa yakimsubiri Mchungaji Mwasapila atoke kanisani, ili awapatie tiba hiyo mbadala ambapo alieleza raia kutoka Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi kijijini hapo.
"Foleni ya magari si kubwa sana kwa siku ya leo kwani hivi tunavyozungumza yapo magari zaidi ya 400 yakimsubiri Babu atoke kanisani na kuanza kuwahudumia kuanzia saa 8 mchana na hakika atawamaliza leo hii," alisema.
Msaidizi huyo alisema kuwa katikati ya wiki iliyopita walipata ugeni wa wachungaji zaidi ya 10 kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati waliokuwa kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano wao mkuu wa mwaka wakiongozwa na Mkuu wa Jimbo aliyetajwa kwa jina moja la Nangole.
Alisema mbali na wachungaji hao kushiriki mkutano huo waliungana na Babu kutoa vikombe kwa wagonjwa waliokuwepo kijijini hapo kupata ti
source: Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo
So kama ni bilionea whats new on Earth?..Ni wa kwanza?
Hata kindergatten hawawezi kukubaliana na magazijuto uliyofanya hapo juu...kama kichwa chako huwa kinaelewa, ulitakiwa kumaliza homework yako kwa kumalizia hesabu hiyo, maana haiishii hapo!
Mpotoshaji mkubwa sana wewe mdada!
Kuna mgawa standard kabisa ambao babu anaufanya, hujauweka kwenye hisabati zako za jumlisha toa!

BTW, hoja yako ninini...Unataka kumwibia au?
 
Habari zaidi zilizopatikana zimeeleza kuwa Babu amepiga marufuku wagonjwa kutoka Kenya wanaosafirishwa kutumia magari yasiyoruhusiwa kama malori na gari ndogo ‘saloon' wakiwa wamejazana hali aliyosema ni mateso kwa wagonjwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alieleza kuwa utoaji tiba unaendelea vizuri kijiji hapo, na alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa ukusanyaji ushuru wa magari na helikopta alisema hayo ni mambo ya kisiasa zaidi na kumtaka mwandishi wa habari hizi kusubiri maamuzi ya kikao halali kitakachofanyika leo kijijini hapo.
Alisema bado maamuzi hayajafikiwa kujua ni mamlaka ipi itakayokuwa ikikusanya ushuru huo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngoromngoro na serikali ya kijiji cha Samunge.
"Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuzungumzia suala hilo naomba usiandike chochote kwani kesho kutakuwa na kikao kitakachozungumzia suala hilo na tutawapeni taarifa," alisema.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mgogoro wa kugombea ushuru wa magari na helikopta kati ya pande hizo na wakati fulani iliripotiwa kuwa serikali ya kijiji iliwafukuza watoza ushuru toka halmashauri.

source: Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo
Jamani mkiandika tumieni ubongo, Haingii kichwani watu millioni Tatu, huo uwezo umetoka wapi wa yeye kunywesha watu 15,000 daily say kwa siku 200 labda kama ni mkono wa Mungu ndiyo umefanya kazi hiyo, Hebu jaribuni kuchakachua hizo hesabu na mimi niridhike or else sikubaliani na hiyo Idadi
 
So kama ni bilionea whats new on Earth?..Ni wa kwanza?
Hata kindergatten hawawezi kukubaliana na magazijuto uliyofanya hapo juu...kama kichwa chako huwa kinaelewa, ulitakiwa kumaliza homework yako kwa kumalizia hesabu hiyo, maana haiishii hapo!
Mpotoshaji mkubwa sana wewe mdada!
Kuna mgawa standard kabisa ambao babu anaufanya, hujauweka kwenye hisabati zako za jumlisha toa!

BTW, hoja yako ninini...Unataka kumwibia au?

Ha ha haaaaaaaaaaa! Anataka kuwa mshika mafao mkuu! Anajiuliza saa hii angekuwa mrs Asapile angekuwa ana ngapi kama babu anazo hizo!
 
Back
Top Bottom