Sasa ni wakati wa kupata katiba mpya

Mr002

New Member
Joined
Jan 24, 2025
Posts
3
Reaction score
3
Ni kweli kabisa kwa sasa tunahitaji KATIBA MPYA mambo mengi sana ndani ya KATIBA ya MWAKA 1977, yameshapitwa na wakati na yanahitaji kufanyiwa marekebishi.hasa kuhusu huu mgawanyo wa serikali na madaraka kwenye muungano , kwann Zanzibar Ina serikali yake lakini tanganyika Haina? Tuna serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na neno Tanzania limetokana na muungano wa pande mbili tanganyika ilienda wapi? Kwann tusingekuwa na serikali moja? Au basi , ingekuwepo serikali ya tanganyika pia

Pia Kuna hii ibara inayotaka , ili uwe na vigezo VYA kuwa waziri lazima uwe mbunge, hii sio sawa mtu MMOJA atawezaje kutimiza majukumu ya uwaziri pia na kuwakilisha Jimbo lake ipasavyo? Lazima hizi nafasi zitenganishwe waziri abaki kuwa waziri na mbunge abaki kuwa mbunge .time to work up..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…