Sasa ni wakati wa wafanyabiashara wakubwa (Wawekezaji) kutajirika kwa ukwasi wa mabilioni ya wajinga

Sasa ni wakati wa wafanyabiashara wakubwa (Wawekezaji) kutajirika kwa ukwasi wa mabilioni ya wajinga

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Neno mjinga halina uhusiano na matusi. Ni mtu asiyejua kitu kuhusu jambo husika.

Kwahiyo kwakuwa Watanzania wengi hawajui yanayoendelea katika nchi yao kutokana na kukosekana kwa uwazi ndani ya shughuli za kiserikali basi ni vyema tutumie msamiati huu wa WAJINGA.

Walipopiga hesabu na kupata watumiaji wengi wa smartphone na ndio wanunuzi wakubwa wa vocha basi wakubwa wa nchi na Wawekezaji wakaweka mtego papo hapo. Ni sawa na kuweka mtego langoni wanaponywea maji ndege. Lazima tu utamnasa

Leo hii vocha ya elfu moja ukinunua bando la internet kisha uzame mtandaoni ukitazama video dk 20 tu habari yako imeisha.

Huu ni wizi, ujambazi na ulanguzi kwa wajinga wasiojua namna ya kujikomboa.

Bidhaa zingine zimeongezeka bei kwa asilimia 40- 60 bila maelezo.

Leo hii wauzaji wa cement au mabati wakiamua kukaa kikao cha siri na kupanga bei mpya kisha kumpa bahasha waziri husika mchezo umeisha.
 
Cha kushangaza zaidi vijana kutwa wapo online, sijui nani anawawekea hizo vocha maana kila siku wanalalamika ajira hakuna
 
Back
Top Bottom