Sasa ninaamini ya kuwa ni kweli mlandizi husahau lakini mtupa maganda..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Yabidi nikiri bila ya kificho
ya kuwa haya ni kweli kabisa..
na hili situngi na ya kwamba yamenikuta kiukweli ukweli.
ni kweli mlandizi husahau bali mtupa maganda hasahau..

Hivi yawaje baada ya miaka kibao kupita
bado samahani yangu yakataliwa?
sababu sipewi bali kukunjiwa "X" tu
ni kweli mla ndizi husahau bali mtupa maganda hasahau...

Kuna siku nilikutana naye ghafla
mwandani wangu wa madongo kuinama
naye kuniona akaniangalia kwa dharau kisigino hadi utosini
ni kweli mla ndizi husahau bali mtupa maganda hasahau..

salamu nilimtupia lakini ni walakini niliambulia
nilitupiwa korosi na alinifyonya kwa ufedhuli
nikamwomba yaishe yeye ngumu akatia..
ni kweli mla ndizi husahau bali mtupa maganda hasahau..

makosa niliuliza na nikaambiwa yabidi nijaze mwenyewe!
sasa nimehukumiwa kwa makosa ambayo hata siyajui
nilichoambulia ni kujuzwa hakuna msamaha hata akiingia kaburini..
ni kweli mla ndizi husahahu bali mtupa maganda hasahau..

kosa langu ni lipi ambalo halina cha ubani?
kama ni bikira yake mbona na yangu aliitafuna bila ya huruma?
mie sina kinyongo naye, sasa yeye mbona purukshani hivyo?
ni kweli mla ndizi husahau lakini mtupa maganda hasahau..

ndizi yangu ni kweli aliimung'unya mung'unya bila cha msalie..
miye nilimvumilia lakini sasa mlalamishi ni yeye yawaje hivyo?
Sukari tulilambishana na sote kufurahiana sasa kejeli na dharau zatoka wapi?
ni kweli mla ndizi husahau lakini mtupa maganda hasahau...

alikula ndizi yangu nami sijasahau lakini yeye hakumbuki hilo
anachokumbuka ni kunisigina kila mahali, hivi yawaje hivyo?
mwafaka nautafuta lakini sioni wa kutusuluhisha..
AMA kwa hakika ni kweli mla ndizi husahau lakini mtupa maganda hasahau...
 
Uombe msamaha iweje...halafu lazima uchuniwe, mwanaume haulizwi bikra its the woman kama huamini check thread za bikira zote JF ni wanawake....
 
Uombe msamaha iweje...halafu lazima uchuniwe, mwanaume haulizwi bikra its the woman kama huamini check thread za bikira zote JF ni wanawake....

Madamex.it is time to call bygones bygones.....................maumivu ni hata kwa yule aliyechunwa huku yuko hai.....................na maziwa yake ukayanyonya bila hata ya huruma halafu bado unamwangushia lawama na dharau kibao.....lol.

usiziamini sana nyuzi za humu JF...................kwani nasi tunazikumbuka bikira zetu tulizodhulumiwa bila hata ya chembe ya huruma....lol
 
Nini kilio jamani mapema hii?
I will be back after...................................................
 
Nini kilio jamani mapema hii?
I will be back after......................... ..........................

smile unajua unyama ulionifanyia na sasa wataka kunikimbia ..........lol
 
ha ha ha. ta ruta walila...., kileke kigende urambona ondijo.

Zimwimtu hawa walandizi hata utamu hawataki kukumbuka....lol kama siyo laana hii sasa ni nini? kazi lawama tu ambazo hazina hata ncha.lol
 
mimi mtu peace sana
siwezi mfanyia myu yeyote unyama especialy you the king of my heart

my love to u has never been requited......so it as good as this thankless gal.....
 
Si "mtupa maganda" bali "mtupiwa maganda"

Kimantiki mla ndizi na mtupa maganda ni huyo huyo mmoja

catch-22 tafakari tena.....................haiwezekani wawe ni yuleyule....................kwa sababu itakuwaje anapokula ndizi asahau khalafu anapotupa maganda asisahau.lazima wawe ni watu wawili tofauti........kuhusu kutupiwa maganda na kutupa maganda yanafanana kiasi ingawaje kutupiwa maganda nilikuwa silijui hadi leo...........na yaelekea kuwa baya zaidi ya hata nilivyokusudia kwenye shairi hili............lol
 


Mtu anaekula ndizi ndie huwa na maganda ambayo anaweza kuyatupa. Kwa hiyo mla ndizi ndo mtupa maganda. Huyu husahau kuwa alikula na kutupa maganda.

Anaetupiwa maganda ndie hasahau kwa sababu ganda hilo alilotupiwa huenda limemkwaza kwa kumtofoa jicho na kumpa chongo, kwa kuvunjika mguu baada ya kulikanyaga, kuteleza na kuanguka au kwa sababu nyenginr

Mla ndizi husahau lakini mtupiwa maganda hasahau kamwe

Nataraji tumeelewana
 
Nimekumiss Smile, how was your Easter na majonzi ya Kanumba?
 

umeleweka kama mlandizi ndiye aliyeimenya hiyo ndizi lakini kama ilimenywa na mwingineo yule aliyeimenya ndiya aliyatupa maganda..............na mwenzie kuimung'unya...........................lol
 
mimi nipo na yesuuu sidanganyiki .............................

Hata miye n vivyo hivyo..........................Kristu Yesu ni wetu sote.........usinibague ...............lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…