Sasa rasmi Tanzania kupeleka timu nne

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
➡️Baada ya klabu ya Simba kufanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup) rasmi sasa Tanzania tutapeleka timu nne kwenye mashindano ya CAF msimu ujao (2022/23) baada ya kuwa miongoni mwa maitaifa 12 yayopeleka timu 4 msimu ujao.

➡️ Kabla ya mchezo wa jana Tanzania kama nchi tulikuwa nafasi ya 13 tukiwa na pointi zetu 23 tu ila baada ya Simba kufuzu robo fainali tukaongeza pointi 7.5 na kufikisha pointi 30.5 na kuwa nafasi ya 10 huku pointi zetu zikiwa na uwezo wa kuongezeka iwapo timu ya Simba itafuzu nusu fainali.

➡️ Nafasi ya 8 yupo Sudani akiwa na pointi 33.5 na pointi zake haziwezi kuongezeka kwa sababu hana timu yoyote kwenye mashindano ya CAF nafasi ya 9 yupo Guinea ana pointi 31 akiwa anatuzidi pointi 0.5 na pointi zake haziwezi kuongezeka tena kwa sababu hana kwenye mashindano ya CAF.

➡️ Nafasi ya 11 yupo Libya ana pointi 28 na pointi zake zinaweza kuongezeka kwani ana timu 2 (Ahli Tripoli na Al-Attihad) zimefuzu robo fainali ya kombe la shirikisho hivyo anaweza kutuzidi iwapo timu zake zitafanya vizuri kwa kufuzu nusu fainali na timu yetu ya Simba isifuzu nusu fainali.

➡️ Nafasi ya 12 yupo Nigeria akiwa na pointi 26 ambazo haziwezi kuongezeka tena kwa hana timu tena kwenye mashindano ya CAF na kuanzia nafasi ya 13 hadi 30 nchi zote zilizopo kwenye nafasi hizo hamna nchi ambayo imebaki na timu kwenye mashindano ya CAF hivyo pointi zao nao haziwezi kuongezeka.

Credit: Yossima Sports
 
Mkuu timu ya simba mashindano yajayo atacheza shirikisho au Cl endapo hatachukua kombe la ligi kuu bara? na ataanzia hatua ipi?
 
Timu nne maana yake nini?

2 ligi ya mabingwa na 2 shirikisho
Au 4 ligi ya mabingwa? Na wanaanzia hatua gani?
 
Mkuu timu ya simba mashindano yajayo atacheza shirikisho au Cl endapo hatachukua kombe la ligi kuu bara? na ataanzia hatua ipi?
1.Atacheza CL ikiwa atachukua ubingwa wa ligi au nafasi ya pili
2. Atacheza CC ikiwa atakuwa mshindi wa wa FA au atashikia nafasi ya tatu kwenye ligi
Na ikiwa atachukua ubingwa, au kushika nafasi ya pili wkt huohuo akawa bingwa wa FA atacheza CL
Kwa point alizonazo kwenye caf club ranking hataanzia hatua ya awali kama ilivyokuwa kwa msimu huu unaondelea

I stand to be corrected
 
Mkuu timu ya simba mashindano yajayo atacheza shirikisho au Cl endapo hatachukua kombe la ligi kuu bara? na ataanzia hatua ipi?
Umeuliza swal zuru San jamaa atolee ufafanuzi
 
Mkuu timu ya simba mashindano yajayo atacheza shirikisho au Cl endapo hatachukua kombe la ligi kuu bara? na ataanzia hatua ipi?
a. Atacheza Cl endapo atakuwa mshindi wa kwanza au pili, pia ataanzaia hatua ya kwanza sio ile ya awali maana atakuwa kwenye orodha ya timu 10 za juu zenye points nyingi.

b. Atacheza shirikisho endapo atakuwa nafasi ya 3, pia ikitokea aliyechukua ubingwa wa FA yuko nafasi ya 1 au 2 kwenye msimamo wa NBC league basi Simba akiwa nafasi ya 4 kwenye NBC league bado ataenda shirikisho.
 
Mkuu timu ya simba mashindano yajayo atacheza shirikisho au Cl endapo hatachukua kombe la ligi kuu bara? na ataanzia hatua ipi?
ataenda ligi ya mabingwa na ataanzia roundi ya kwanza na si round ya awali
 
Hongera sa Simba kwa kujibeba na kujikatia tiketi ya Kimataifa...N.B Yanga ataenda kama Bingwa wa NBC League.Kila mtu atakula kwa jasho lake.
 
Kwahiyo unataka kusema utopolo wanabebwa lakini awabebeki kwa namna yoyote ile
Wanufaika hapo ni Azam na nyinyi wenyewe. Yanga ina asilimia zaidi ya 80 ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu msimu huu! Hivyo inajibeba yenyewe.
 
Wanufaika hapo ni Azam na nyinyi wenyewe. Yanga ina asilimia zaidi ya 80 ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu msimu huu! Hivyo inajibeba yenyewe.
Kabla haijachukua huo ubingwa tayari tumeshaihakikishia kuwa itacheza CL, kwahiyo tumeibeba hata kama haikuwa tayari kubebwa.
 
Kabla haijachukua huo ubingwa tayari tumeshaihakikishia kuwa itacheza CL, kwahiyo tumeibeba hata kama haikuwa tayari kubebwa.
Yanga tangu msimu unaanza tayari ilisha jihakikishia ubingwa. Hivyo wanufaika bado mtabakia nyinyi wenyewe, wadogo zenu Azam, na katimu kengine ka kimaskini katakako shika hiyo nafasi ya 4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…