Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
➡️Baada ya klabu ya Simba kufanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup) rasmi sasa Tanzania tutapeleka timu nne kwenye mashindano ya CAF msimu ujao (2022/23) baada ya kuwa miongoni mwa maitaifa 12 yayopeleka timu 4 msimu ujao.
➡️ Kabla ya mchezo wa jana Tanzania kama nchi tulikuwa nafasi ya 13 tukiwa na pointi zetu 23 tu ila baada ya Simba kufuzu robo fainali tukaongeza pointi 7.5 na kufikisha pointi 30.5 na kuwa nafasi ya 10 huku pointi zetu zikiwa na uwezo wa kuongezeka iwapo timu ya Simba itafuzu nusu fainali.
➡️ Nafasi ya 8 yupo Sudani akiwa na pointi 33.5 na pointi zake haziwezi kuongezeka kwa sababu hana timu yoyote kwenye mashindano ya CAF nafasi ya 9 yupo Guinea ana pointi 31 akiwa anatuzidi pointi 0.5 na pointi zake haziwezi kuongezeka tena kwa sababu hana kwenye mashindano ya CAF.
➡️ Nafasi ya 11 yupo Libya ana pointi 28 na pointi zake zinaweza kuongezeka kwani ana timu 2 (Ahli Tripoli na Al-Attihad) zimefuzu robo fainali ya kombe la shirikisho hivyo anaweza kutuzidi iwapo timu zake zitafanya vizuri kwa kufuzu nusu fainali na timu yetu ya Simba isifuzu nusu fainali.
➡️ Nafasi ya 12 yupo Nigeria akiwa na pointi 26 ambazo haziwezi kuongezeka tena kwa hana timu tena kwenye mashindano ya CAF na kuanzia nafasi ya 13 hadi 30 nchi zote zilizopo kwenye nafasi hizo hamna nchi ambayo imebaki na timu kwenye mashindano ya CAF hivyo pointi zao nao haziwezi kuongezeka.
Credit: Yossima Sports