Hata Tanzania serikali inajua kabila la kila mtu usijitie hamnazo , kwani wazawa wa Moshi Ni kabila gani? Wazawa wa morogoro Ni kabila gani, wazawa wa mtwara Ni kabila gani ? Mbona mnajifanya zuzu kwa Mambo ya hazarani? Leo hii ukatajwa tu kwa jina tayari unajulikana unatoka kabila lipi ,kwa mfano ukiniambia unaitwa kimaro najua wewe Ni mtu wa Moshi ,ukisema unaitwa mwakasitu najua unatoka mbeya ukisema unaitwa mkude najua anatoka uzaramoni ukisikia mtu anaitwa marwa unajua huko Ni ukuriani , mbona Leo unajifanya serikali ya Tanzania haijui watu kwa makabila yao ilihali hakuna mnyiramba anaejiita majina wa wasukuma au mnyaturu akajiita majina ya wanyamwezi kutoka huko tabora ,tuwe wakweli ndugu yangu maana hata serikali zote duniani zinaendeshwa na watu kutoka makabila ,Leo hii unajua speaker was bunge la muungano wa Tanzania Ni mnyakyusa, waziri mkuu majaliwa Kuna uwezekano Ni mngindo kutoka Lindi ,makamu wa rais mpango Ni mtu wa kigoma na watu wa kigoma wanajulikana kwa hivyo usilete ngonjera ndugu yangu,kila mtanzania anajulikana kwa kabila lake ,kwa mfano mtu hapa kenya akiniambia anatoka county flani Kuna uwezekano nijue kabila lake bila hata kutaja pengine Kuna mchanganyiko wa makabila lakini kwa kawaida kila mkoa una asili ya watu wa kabila flani,mfano ukisema unatoka nyanza nitajua wewe mkisii ,mjaluo au mkuria hao ndio wanapatikana nyanza lakini pia kwa lafudhi yako nitajua kabila lako hata usiposema, ukisema unatoka mkoa wa magharibi vilevile nitajua wewe Ni mluhya na ukisema unatoka mkoa wa Kati nitajua wewe Ni mkikuyu au mmeru na Tanzania pia Ni vilevile.