mimi naweza nikapika,ila mambo ya vipimo,sijui.vyakula ambavyo napika kwa kupima ni keki,mkate wa mayai,na mkate wa kumimina.kwa leo nitawafahamisha kupika mkate wa kumimina{mkate wa mchele}
-kikombe kimoja cha mchele
-yai moja
-tui la nazi
-sukari
-hiliki
-hamira.
usiku unaroweka mchele mpaka asubuhi{kikombe kimoja}tui nzito ya nazi unapima na kile kile kikombe kimoja.unavitia kwenye blenda,tui la nazi,mchele,na hiliki nusu kijiko cha chai na sukari unapimia kwenye kile kikombe.ila sukari inakuwa haijai{sukari ni nusu na robo ya kile kikombe}.yai ni ute wa yai tu.vitu vyote unasaga kwenye blenda.vikishalainika unaweka kwenye bakuli.unatia hamira kijiko 1 cha chai unakoroga ili vichanganyike.hamira usiisage kwenye blenda{ukiisaga mkate hauwi na rangi ya kuvutia}ukimaliza vyote unafunika na kusubiri mpaka viumuke.vikishaumuka unachukua sufuria lako,unatia mafuta kidogo unapaka kwenye sufuria{inasaidia mkate haugandi}unatia mchanganyiko wote,unaweka kwenye oven,kwenye moto wa kawaida,kila baada ya muda unacheki,{mimi huwa napenda mkate uwe na rangi ya kama ya ukoko wa wali}ukitaka kujua mkate umeiva ndani,unatafuta kijiti chako,kisafi,fanya kama unakiingiza kwenye mkate,kijiti kikitoka kisafi bila ugando wa mkate,ujue mkate wako uko tayari.ila kijiti kikitoka na ugando wa mkate,ujue mkate wako haujaiva}mkate ni mzuri kwa kunywea chai[/QUOTE
sina blenda jamani,ningependa kujaribu hii kitu...inshalah ngoja niprint out nijaribu siku nyengine,thanks for sharing mamito.....:mwaaah: