Pauline, hebu ongezea ugali hapo, bamia/mchicha na samaki wa kukaanga 🙂 ili wengine tuweze kujisikia sikia kama tumepata mlo wa uhakika
Chapati haina kazi??Chapati gani unaongelea wewe!??
Mkate wa kusukuma bana, ule unauzungusha layer kwa layer,...! Sio chapati ilimradi imesukumwa tu :becky:
hapo pamejaa vilivyokaangwa tu. Kwa meza hiyo, nampa mpishi maksi 6/10...tena sababu ya chapati tu.
The rest sijui ni uvivu wa kupika, amekaanga tu kila kitu! Na hiyo nyama ya mchuzi wala haina mvuto kiviiile!
ha ha ha, anaongelea mkate wa maji huyo, sio ule kule unguja tunaouita mkate wa kusukuma.
Wakati wa kula unauchambua layer after layer...
Sio chapati ikishachomwa dakika tano baadae inakauka utadhani 'kipepeo cha mkono!'
Menu yako nimeipata ila hiyo juisi ya Embe mbichi,parachichi na tangawizi???!!Mhn!:confused2:...mkate wa kumimina, vitumbua, kaimati, vipoo poo, visheti, faluda, mzuu wa nazi, mseto, samaki wa kupaka, kisamvu, Pilau ya mboga mboga...
Bro BaK we acha tu...raha ya 'mahanjumati' hayo uyavalie msuli huku ukisukumia na juice ya Bungo ilochonganywa na syrup ya Iliki au mdalasini, ...au Juice ya Embe mbichi na parachichi iliyochanganywa na tangawizi mbichi
halafu unamalizia na chai ya viungo (masala tea)
Sio tiba mbadala kweli hiyo,nahisi kama tumbo litageuka kuwa kiwanda cha tindikali a.k.a nyongo?Kama lengo ni hilo basi ulisahau pilipili kichaa na mbilimbi
ha ha ha, anaongelea mkate wa maji huyo, sio ule kule unguja tunaouita mkate wa kusukuma.
Wakati wa kula unauchambua layer after layer...
Sio chapati ikishachomwa dakika tano baadae inakauka utadhani 'kipepeo cha mkono!'
Yani hizi ndo unataka???Kula huko huko kwa mama ntilie nisije nikachekwa mie!:becky::becky::becky:
Hizi ndo nilikuwa nataka Lizzy azijue
Dah, MBU nisaidie,bibi yako naumbuka hapa.Nashindwa namna ya kuquote somoene's point then chini yake niendeleze mjadala kama ulivyofanya juu hapo.Naomba nielekeze,si unajua "ndio tumetoka usingizini wakati ni saa 8 mchana tayari"
Dah, MBU nisaidie,bibi yako naumbuka hapa.Nashindwa namna ya kuquote somoene's point then chini yake niendeleze mjadala kama ulivyofanya juu hapo.Naomba nielekeze,si unajua "ndio tumetoka usingizini wakati ni saa 8 mchana tayari"
hii ni mojawapo ya sectors za malavi davi inakyokuwa overlooked ila aparently inasababisha matatizo.....sasa wenye uzoefu tupeane maujuzi humu,tusije tukaachika bure lol.....tufundishane namna nyengine za kupika nyama,wali,mboga za majani na vile vyakula vya asili.....kujua aina moja tu ya upishi inachosha tufundishane varieties jamani..................
NB.....na wale wengine wenye recipe rahisi rahisi na fupi mnaweza kuongezea hata wakaka wanaoishi kibachela napo wapate maujuzi........mie mpaka leo sijui kupika wali wa nazi ingawa kila siku najitahidi kujaribu lol....nawish by the time naolewa niwe nimejuwa lol...........
najua siko peke yangu wadada tuzungumze kikike mambo yasiharibike:becky::becky::mwaaah:...naombeni kwa kuanzia mnaojua zile sambusa ile nyama ya ndani ya kusaga wanatia viungo gani/wanapikaje?..........karibuni.
mimi naweza nikapika,ila mambo ya vipimo,sijui.vyakula ambavyo napika kwa kupima ni keki,mkate wa mayai,na mkate wa kumimina.kwa leo nitawafahamisha kupika mkate wa kumimina{mkate wa mchele}
-kikombe kimoja cha mchele
-yai moja
-tui la nazi
-sukari
-hiliki
-hamira.
usiku unaroweka mchele mpaka asubuhi{kikombe kimoja}tui nzito ya nazi unapima na kile kile kikombe kimoja.unavitia kwenye blenda,tui la nazi,mchele,na hiliki nusu kijiko cha chai na sukari unapimia kwenye kile kikombe.ila sukari inakuwa haijai{sukari ni nusu na robo ya kile kikombe}.yai ni ute wa yai tu.vitu vyote unasaga kwenye blenda.vikishalainika unaweka kwenye bakuli.unatia hamira kijiko 1 cha chai unakoroga ili vichanganyike.hamira usiisage kwenye blenda{ukiisaga mkate hauwi na rangi ya kuvutia}ukimaliza vyote unafunika na kusubiri mpaka viumuke.vikishaumuka unachukua sufuria lako,unatia mafuta kidogo unapaka kwenye sufuria{inasaidia mkate haugandi}unatia mchanganyiko wote,unaweka kwenye oven,kwenye moto wa kawaida,kila baada ya muda unacheki,{mimi huwa napenda mkate uwe na rangi ya kama ya ukoko wa wali}ukitaka kujua mkate umeiva ndani,unatafuta kijiti chako,kisafi,fanya kama unakiingiza kwenye mkate,kijiti kikitoka kisafi bila ugando wa mkate,ujue mkate wako uko tayari.ila kijiti kikitoka na ugando wa mkate,ujue mkate wako haujaiva}mkate ni mzuri kwa kunywea chai[/QUOTE
sina blenda jamani,ningependa kujaribu hii kitu...inshalah ngoja niprint out nijaribu siku nyengine,thanks for sharing mamito.....:mwaaah:
Pauline, asante kwa "kunijaza mate mdomoni".
Huo msosi unavutia, mpaka nimekumbuka nyumbani. Natamani kurudi leo.
Ila kitu ninachoona, ni upungufu tulionao katika ulaji wa mboga.
Kwa kweli ingependeza kama tungekuwa tunakula mboga za majani nyingi na za aina mbalimbali kwa ajili ya afya zetu.
Ni bahati mbaya kwamba kwa familia nyingi tunapenda nyama nyama ndio ziwe kibao. Halafu ka-mchicha kanakuwepo kiduchu kama vile kwa ajili ya kupamba sahani tu.
Wajuzi wasisahau kutuletea na mapishi ya matembele, swischard, sukuma wiki, cabbage, brocolli, majani ya maharage, mnavu, mchunga, chinese cabbage, mboga za maboga, majani ya magimbi, njegere, matango, maboga, maharagwe, kunde, choroko, n.k.
...ooohhh, pole sana, wengi wetu tumetokea huko huko.
1. Bonyeza kitufe cha "Reply With Quote", itakupeleka hapa;
2. Anzia ku type nje ya mabano haya;[quote] ......[/quote]..kisha unabonyeza kitufe cha "SAVE." Job done!
Angalizo.
kwa masahihisho, ni rahisi wewe mwenyewe kwa kutumia keyboard yako ukaweka hayo mabano
na kuandika hayo maneno [QUOTE] ....kisha [/QUOTE]
Nifundishe chapati navozipendaaa!! hee!! nadhani ntafunga nazo ndoa!! hasa nene laini!! maweee!! yaani naweza kuishi kwa chakula hiki tu!! nikawa na furaha! nakulaga na Beans, mchuzi, nyama, Pepsi, mboga zooote nakula na chapati!I opened my teeth now
:becky::becky::becky:
Mkuu chapati haina kazi sana, labda chapati za kuwekea makorombwezo mpaka zionekane kama mayai ya Spanish