Sasa tuwageukia upinzani- wajirekebishe na kujipanga mapema

Sasa tuwageukia upinzani- wajirekebishe na kujipanga mapema

Mkuu wangu kasheshe.

Kushinda kwa kishindo kwa ccm in the light ya upotevu wa pesa kule BoT kwa sasa uko tainted sana. Ni vigumu sana kusema kwa hakika kama ccm ilishinda kwa kishindo.

Ndugu wakike
Umenikumbusha manen ya JK mwenyewe siku wanatangaza matokeo na kuambiwa kashida kwa asilimia sijui ngapi wenyewe huwa wanaitaja lakini yeye akasema haamini kwamba alipata kura hizo maana aliona uhalisia wa Kampeni .Nakubaliana nawe kwamba ni EPA iliongea si kura za 80%
 
Kimbembe kipo katika hilo la kuachiana majimbo, maana hapo ndipo penye mtego wa kitu kinaitwa RUZUKU. Kila mmoja atadai yeye ndie anakubalika zaidi katika jimbo fulani ili aongeze asilimia ya ruzuku bila kujali kama kweli atashinda.

Tumeshuhudia hili kwenye ile "ndoa" ya CUF na Chadema mwaka 2000 mwisho wakakubaliana kutokubaliana na kila mmoja akaingia kivyake na wote wakaangukia poa!

Bado naamini kabla ya kulivalia njuga hilo la "kuachiana" majimbo na mgombea mmoja wa urais suala la mabadiliko ya katika ni muhimu zaidi. Katiba yetu hairuhusu mgombea wa "pamoja" na hilo kwa mtazamo wangu ndio nguzo kuu inayokwamisha upinzani. Sambamba na hilo kuanzisha chama cha "pamoja" ndani ya muda mfupi haiwezekani kwani kuna mlolongo wa urasimu kuanzia kutafuta saini za watu sijui mia ngapi kutoka mikoa zaidi ya kumi ikiwemo ya Zanzibar.

All said and done wakati tunapanga sijui Lipumba agombee Ilala, Mbatia Kinondoni nk nadhani ni muhimu kwanza tukasukuma mabadiliko ya katiba walau iwe kama ya jirani zetu wa Kenya.
 
Mi naona wapinzani wapo ila hawajajipanga. mimi ninachoshauri ni kwamba wajipange kwa hii miaka miwili watuonyeshe kwamba wanaweza kuchukua nchi na kufanya mabadiliko ya kimaendeleo,wawe na watu makini siyo vigeu geu na sisi wananchi tunatakiwa kuelewa kwamba hakuna njia ya mkato lazima tuwajibike kufanya haya mabadiliko kama tutashindwa kuwaweka wapinzani madarakani basi angalau hata asilimia 70 ya wabunge wawe wapinzani.
 
Uchaguzi wa mwaka 1995,Hapo Dar wanaposema pameshindikana mbona walihairisha ukarudiwa mara ya pili kwa kuwa NCCR-Mageuzi ilionekana kuchukua majimbo karibu yote,Wakasingizia vifaa vya kupigia kura vimechelewa na mawakala hawakuwa vituoni kwa mda uliotajwa,ndipo baba wa Taifa akaingilia kati na hata kule Zanzibar.Mara ya pili wakaacha kiti cha Ubungo kwa Masumbuko Lamwai.Pia mara ya pili mandagu walitapakaa hadi wananchi wakaogopa maana hawakuwahi kuona askari wamejaa mitaani hivo.

Mwaka huo huo Kule alikozaliwa baba wa Taifa MKOANI MARA wapinzani walishinda majimbo manne ( 4).
Wananchi wakiamua kukataa vikofia,fulana na pilau mbona inawezekana.Sisiem haijashuka toka mbinguni,imeanzia hapa hapa duniani.Washindani wanaweza kabisa kwa kushirikiana na wananchi.
 
Back
Top Bottom