Uchaguzi wa mwaka 1995,Hapo Dar wanaposema pameshindikana mbona walihairisha ukarudiwa mara ya pili kwa kuwa NCCR-Mageuzi ilionekana kuchukua majimbo karibu yote,Wakasingizia vifaa vya kupigia kura vimechelewa na mawakala hawakuwa vituoni kwa mda uliotajwa,ndipo baba wa Taifa akaingilia kati na hata kule Zanzibar.Mara ya pili wakaacha kiti cha Ubungo kwa Masumbuko Lamwai.Pia mara ya pili mandagu walitapakaa hadi wananchi wakaogopa maana hawakuwahi kuona askari wamejaa mitaani hivo.
Mwaka huo huo Kule alikozaliwa baba wa Taifa MKOANI MARA wapinzani walishinda majimbo manne ( 4).
Wananchi wakiamua kukataa vikofia,fulana na pilau mbona inawezekana.Sisiem haijashuka toka mbinguni,imeanzia hapa hapa duniani.Washindani wanaweza kabisa kwa kushirikiana na wananchi.