Sasa unaweza kufuga Nyuki nyumbani kwako

Sasa unaweza kufuga Nyuki nyumbani kwako

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
380
Reaction score
550
Jambo hili nimekuwa nikiulizwa sana na watu wengi iwapo mtu anaweza kufuga Nyuki wanaoudunga mwiba, (wengi wamezowea kusema Nyuki wanaouma) nyumbani, jibu lake ni ndiyo inawezekana.

Kivipi, hapa ndipo inabidi nikupe shule maana Nyuki ni hatari sana wanaweza kusababisha madhara makubwa kwa watu hata vifo.

Hatua ya Kwanza: Ili uweze kufuga Nyuki nyumbani ni lazima uwe na mizinga wa kufugia nyuki, lakini sababu ni nyumbani mimi nakushauri uwe na mzinga maalum kwa nyumbani ambao utapendezesha makazi yako na kukufugia Nyuki pia.

Mizinga aina hii Kwanza huwa ni pambo na mingi in vioo ambavyo hukuwezesha kuwaona Nyuki ndani yake hivyo kugeuka kuwa kivutio kwako.

Screenshot_20220930-004551~2.png
Huu ni mmoja wa mzinga wa kufugia Nyuki nyumbani.

Tunaendekea........>>>
Kawaida Nyuki wakubwa tunaofuga ambao wanazalisha asali no hatari sana katika makazi yetu, lakini Nyuki Hawa wanaweza kufugwa na wakafunzwa kuzowea binadamu na ukaishi nao wasikushambulie. Hiki ndicho namaanisha.
Kwani Sasa Nyuki Farming tumeanzisha mradi wa ufugaji Nyuki msinga mmoja au miwili majumbani kwa lengo la kuwalinda wasitoweke lakini pia kuwapatia asali na kuwatumia Kama kuvutio kwa watu.

Wengi huliona Jambo hili Kama gumu, lakini wanafunzwa kuwazowea binadamu na unaweza kuweka mkono kwenye mzinga wait au kuwa katibu yao kabisa wakatoka kuendelea na maisha shughuli zao za Kila siku na wasikushambulie isipokuwa, ukiwachokoza watakushambulia tu.

Kwa Sasa tunayo mizinga aina 2 ambayo mtu anaweza kutumia kufugia Nyuki nyumbani lakini sharti tumpatie mbegu ya Nyuki ambao wamezowea hata waking katika makazi hawawezi kuwasumbua kwa kuwadunga na mwimba.
Screenshot_20221003-004757~2.png

Mzinga I: Kama picha inavyoonekana hapo juu huu ni aina ambayo unakuwa na miti ya mapambo mingi ubavunu kwake. Aina hii unaweza kuzalisha asali Kg 30 kwa mwaka au zaidi ikitegemea. Una kioo ambacho kinakuwezesha kuwaangalia Nyuki ndani ya mzinga. Na juu unayo chupa bayo unaweza kutoa masega yenye asali kwenye hiyo chupa na ukawatumia watu zawadi ya asali ikiwa kwenye masega.

Screenshot_20220930-004635~2.png

Mzinga II: Aina hi unawezwa kutundikwa ukitani. Sehemu ya mbele unacho kioo kidogo ambacho kitakusaidia kuwaangalia Nyuki ndani. Huu uzalisha asali Kg. 3-5 kwa mwaka.

Screenshot_20221003-004802~2.png

Mzinga III: Aina nyingine ni Kama wa Kwanza lakini huu mfuniko wake upo kwa muundo wa paa ambao unaweza kuliwekea udingo na kupanda may juu ambayo pia husaidia kuwalisha Nyuki na kupendezesha Nyumba yako au mazimgira. Huu pia unaweza kuvuna Kg 30 za asali.

Angalizo! Mteja akichukua mizinga kwetu sisi humuzia na Nyuki ambao wamekusha fundishwa na kuwazowea binadamu hivyo unaweza kyishi nao. Lakini lazima pia tumpatie mafunzo anayechukua mzinga huo yeye na familia yake namba ya kuuhudumia mzinga huo ili asije kudhurika na Nyuki.
 
Shukrani mkuu ila ongeza taarifa like mzinga utatoa lita ngapi kwa muda gani, msinga mmoja bei gani, je ni nyuki wadogo au wakubwa, masoko yakoje nk
 
Nakuja na taarifa baadaye.
Kwann umeanzisha uzi bila taarifa kamili?! Huoni kwamba unatukosea heshima wanaJF?!

Yaani watu tumeacha shughuli zetu tumekuja kusikilizana na wewe unatuambia unakuja na taarifa baadae.

Haya nirudishie mafuta yangu haraka maana nimetoka posta kule hadi hapa kwaajiri yako.
 
Jambo hili nimekuwa nikiulizwa sana na watu wengi iwapo mtu anaweza kufuga Nyuki wanaoudunga mwiba, (wengi wamezowea kusema Nyuki wanaouma) nyumbani, jibu lake ni ndiyo inawezekana.

Kivipi, hapa ndipo inabidi nikupe shule maana Nyuki ni hatari sana wanaweza kusababisha madhara makubwa kwa watu hata vifo.

Hatua ya Kwanza: Ili uweze kufuga Nyuki nyumbani ni lazima uwe na mizinga wa kufugia nyuki, lakini sababu ni nyumbani mimi nakushauri uwe na mzinga maalum kwa nyumbani ambao utapendezesha makazi yako na kukufugia Nyuki pia.

Mizinga aina hii Kwanza huwa ni pambo na mingi in vioo ambavyo hukuwezesha kuwaona Nyuki ndani yake hivyo kugeuka kuwa kivutio kwako.

Huu ni mmoja wa mzinga wa kufugia Nyuki nyumbani.
Hao nyuki nitawaletaje nyumbani?
 
Nyuki tuwafuge hukoo nyumbani na hawa kina junior hapana
 
Muhimu ufugaji huu. Sasa eleza mkwapi tuje tujifunze zaidi
 
Kwann umeanzisha uzi bila taarifa kamili?! Huoni kwamba unatukosea heshima wanaJF?!

Yaani watu tumeacha shughuli zetu tumekuja kusikilizana na wewe unatuambia unakuja na taarifa baadae.

Haya nirudishie mafuta yangu haraka maana nimetoka posta kule hadi hapa kwaajiri yako.
Samahani mambo tayari
 
Hao nyuki nitawaletaje nyumbani?
Tunakuletea mzinga ukiwa na Nyuki ambao tumewafunza utaishi nao wakiingia na kutoka katika mzinga bila madhara kwako. Ila usiende kuwachokonoa na kijiti au mti. Ila kabla ya happy sisi tunaanza kuwatega waingie kwenye mzinga wako Kisha tukishawafunza tulajiridhisha hawawezi kukushambulia hata ukienda mbele yao ukiwa na harufu ya Manukato tunakuletea.

Katika video hii hapa tumekwisha watega Nyuki wanaingia kwenye mzinga lakini eneo la makazi na Kisha tutawafunza kuzowea watu.
 
Tatizo sisi tuna jamii ya nyuki wanaitwa "African Killer Bees"
Hapo sasa.....Attack...
Hawana shida. Kuna watu wanaishu na Nyuki ndani ya Nyumba wakiamini wamekuja kwa ajili ya mizimu ndiyo maana hawawaumi, lakini siyo kweli Nyuki wanaweza kuishi nawe na wakakuzowea wasikuume ukiwa naomndani ya Nyumba.
 
Kioo kiko wapi mbona naona kuni tu hapo.
Screenshot_20221003-010135~3.png

Ukiangalia hapo nilipozungushia rangi, ni kioo lakini huwa tunaweka mlango wa kufunga ili isije kutokea mtu aponda kioo na kuvunja, hivyo itagungua mlango kubakiza kioo oale unapohitaji kuangalia na Kisha ugafunga.
 
Nimewahi kusikia kuna aina mbili za nyuki.

1. Nyuki wakubwa ambao ni hatari na wanashambulia.

2. Nyuki wadogo ambao hawashambulii.

Inasemekana nyuki wakubwa wanatoa asali nyingi kuliko nyuki wadogo.

Pia inasemekana asali ya nyuki wadogo ni nzuri na ina virutubisho kuliko asali ya nyuki wakubwa.

Naomba unisaidie mimi pamoja na wasomaji wako ktk jukwaa letu kuhusu ukweli wa maelezo hayo hapo juu.

Natanguliza shukrani.
 
Yes yes asali ya nyuki wadogo ni nyeusi hivi

Tunao nyumbani , hawanaga habari na mtu kabisa

Ila asali yake ni kidooogo na inapatikana kwa mwaka mara moja Kama sijasahau
 
Yes yes asali ya nyuki wadogo ni nyeusi hivi

Tunao nyumbani , hawanaga habari na mtu kabisa

Ila asali yake ni kidooogo na inapatikana kwa mwaka mara moja Kama sijasahau

Je, ni kweli kwamba nyuki wadogo wana tabia ya kuua nyuki wakubwa?

Je, nyuki wadogo hawawezi kufugwa kitaalamu wakatoa asali nyingi kwa ajili ya biashara?
 
Back
Top Bottom