Sasa unaweza kufuga Nyuki nyumbani kwako

Sasa unaweza kufuga Nyuki nyumbani kwako

Nimewahi kusikia kuna aina mbili za nyuki.

1. Nyuki wakubwa ambao ni hatari na wanashambulia.

2. Nyuki wadogo ambao hawashambulii.

Inasemekana nyuki wakubwa wanatoa asali nyingi kuliko nyuki wadogo.

Pia inasemekana asali ya nyuki wadogo ni nzuri na ina virutubisho kuliko asali ya nyuki wakubwa.

Naomba unisaidie mimi pamoja na wasomaji wako ktk jukwaa letu kuhusu ukweli wa maelezo hayo hapo juu.

Natanguliza shukrani.


Ndiyo ni kweli kuna Nyuki an mbili Kama ulivyozitaja.

Nyuki wakubwa ndiyo wazalishaji wakubwa wa asali kuliko wadogo. Lakini Nyuki wadogo (wasiouma) wanachangamoto kubwa kufugika na uzalishaji wake asali ni kidogo Sana hii ndiyo sababu pia asali yake haipatikani kwa wingi na kwa vile inahitajika pia hivyo demand yake imeifanya kuuzwa Bei kubwa mfano Sh 30,000/ -50,000/ kwa kilo (sokoni wanaita Lita).
 
Hii ni possible hata majirani wanafanya
mkuu, project bado unaendelea nayo
 
Jambo hili nimekuwa nikiulizwa sana na watu wengi iwapo mtu anaweza kufuga Nyuki wanaoudunga mwiba, (wengi wamezowea kusema Nyuki wanaouma) nyumbani, jibu lake ni ndiyo inawezekana.

Kivipi, hapa ndipo inabidi nikupe shule maana Nyuki ni hatari sana wanaweza kusababisha madhara makubwa kwa watu hata vifo.

Hatua ya Kwanza: Ili uweze kufuga Nyuki nyumbani ni lazima uwe na mizinga wa kufugia nyuki, lakini sababu ni nyumbani mimi nakushauri uwe na mzinga maalum kwa nyumbani ambao utapendezesha makazi yako na kukufugia Nyuki pia.

Mizinga aina hii Kwanza huwa ni pambo na mingi in vioo ambavyo hukuwezesha kuwaona Nyuki ndani yake hivyo kugeuka kuwa kivutio kwako.

Huu ni mmoja wa mzinga wa kufugia Nyuki nyumbani.

Tunaendekea........>>>
Kawaida Nyuki wakubwa tunaofuga ambao wanazalisha asali no hatari sana katika makazi yetu, lakini Nyuki Hawa wanaweza kufugwa na wakafunzwa kuzowea binadamu na ukaishi nao wasikushambulie. Hiki ndicho namaanisha.
Kwani Sasa Nyuki Farming tumeanzisha mradi wa ufugaji Nyuki msinga mmoja au miwili majumbani kwa lengo la kuwalinda wasitoweke lakini pia kuwapatia asali na kuwatumia Kama kuvutio kwa watu.

Wengi huliona Jambo hili Kama gumu, lakini wanafunzwa kuwazowea binadamu na unaweza kuweka mkono kwenye mzinga wait au kuwa katibu yao kabisa wakatoka kuendelea na maisha shughuli zao za Kila siku na wasikushambulie isipokuwa, ukiwachokoza watakushambulia tu.

Kwa Sasa tunayo mizinga aina 2 ambayo mtu anaweza kutumia kufugia Nyuki nyumbani lakini sharti tumpatie mbegu ya Nyuki ambao wamezowea hata waking katika makazi hawawezi kuwasumbua kwa kuwadunga na mwimba.
View attachment 2375339
Mzinga I: Kama picha inavyoonekana hapo juu huu ni aina ambayo unakuwa na miti ya mapambo mingi ubavunu kwake. Aina hii unaweza kuzalisha asali Kg 30 kwa mwaka au zaidi ikitegemea. Una kioo ambacho kinakuwezesha kuwaangalia Nyuki ndani ya mzinga. Na juu unayo chupa bayo unaweza kutoa masega yenye asali kwenye hiyo chupa na ukawatumia watu zawadi ya asali ikiwa kwenye masega.

View attachment 2375337
Mzinga II: Aina hi unawezwa kutundikwa ukitani. Sehemu ya mbele unacho kioo kidogo ambacho kitakusaidia kuwaangalia Nyuki ndani. Huu uzalisha asali Kg. 3-5 kwa mwaka.

View attachment 2375341
Mzinga III: Aina nyingine ni Kama wa Kwanza lakini huu mfuniko wake upo kwa muundo wa paa ambao unaweza kuliwekea udingo na kupanda may juu ambayo pia husaidia kuwalisha Nyuki na kupendezesha Nyumba yako au mazimgira. Huu pia unaweza kuvuna Kg 30 za asali.

Angalizo! Mteja akichukua mizinga kwetu sisi humuzia na Nyuki ambao wamekusha fundishwa na kuwazowea binadamu hivyo unaweza kyishi nao. Lakini lazima pia tumpatie mafunzo anayechukua mzinga huo yeye na familia yake namba ya kuuhudumia mzinga huo ili asije kudhurika na Nyuki.
Mnapatikana wapi mkuu?
 
Je, ni kweli kwamba nyuki wadogo wana tabia ya kuua nyuki wakubwa?

Je, nyuki wadogo hawawezi kufugwa kitaalamu wakatoa asali nyingi kwa ajili ya biashara?
Ukweli ni kinyume chake yaani nyuki wadogo ndiyo wanaoumwa na wakubwa hiyo huwezi wafuga karibu. Hii pia ni sababu ya nyuki wadogo kueneleza lutoweka zaidi.

Nyuki wadogo wanafugw lakini uzalisha wao siyo mkubwa na hii ndiyo sababu asali yake inakuwa aghali sokoni
 
Back
Top Bottom