Sasa Wanasiasa wameachwa Watupu. Wananchi wamegundua wanachezwa Shere.

Sasa Wanasiasa wameachwa Watupu. Wananchi wamegundua wanachezwa Shere.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Ile ya kutushauri twendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini... Wananchi wameanza kukataa.

Wananchi wengi wamekuja gundua wao wanasiasa WANAKULA NYAMA MTORI WANAUACHA JUU.

Wananchi wengi wamejikuta wakimaliza Mtori na kukuta chini patupu. Wachache wanasema kila wanapokaribia kufika chini ya bakuli wanaongezewa tena Mtori. Hawajawahi kuachwa wakutane na nyama.

But wananchi wamekuja kugundua Dhana hii ya KULA MTORI NYAMA UTAZIKUTA CHINI. Haitumiki kwa Viongozi. Wao mara zote wameonekana WAKILA NYAMA NA MTORI kutegemea kuukuta ikiwa watakuja fika chini. Jambo ambalo limekuwa ni Nadra sana kwao kutokea.

Maana huwa wanajua kuinuana...na kukumbukana.

Wananchi wengi wameanza kuonesha kutokubaliana na hali hiyo ya miaka yote na kuona wanafanywa watoto wadogo. Wamechoka wanataka katika kipindi hiki kigumu wote tunywe mtori na ikitokea kufika huko chini tu weze share Nyama pia.
 
Mtori hauongezwi, nyama hakuna (zinaliwa na wanasiasa)... Na hakuna kitu mtawafanya.
 
Spika atasema kwamba hajapata barua rasmi kutoka chadema inayo mtaarifu kwamba wamefukuzwa uanachama.
Ama kama amepata barua kutoka chadema, atasema kwamba hana taarifa rasmi kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa.
Baada ya hapo bunge litalipuka kwa shangwe na kisha spika atatangaza kwamba yeye anawatambua kama wabunge halali wa chadema....teh😜
 
Back
Top Bottom