Sasa wewe unataka Teuzi/ Umeteuliwa kisha unajifanya kutumia akili? Utaona sasa.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Haya maneno yamenifikirisha sana. Aliyekuwa ananiambia ni Katibu Wizara flan. Na ni sababu nimemuuliza mbona jina langu halipelekwi kwenye teuzi mbalimbali nami tayari nina uzoefu nshafiri sana na mama na Elimu inaruhusu.

Jamaa hakuuma uma maneno.kanichana live(watoto wa mjini mnasema hivyo) kanipa makavu hakuremba wala kupaka rangi maneno.

Sasa naelewa kuwa tatizo ni mimi kujifanya mjuaji, na ushamba wangu wa huu wa kijinga, kifala. Kujifanya sioni mema ya nchi anayofanya mama na serikali kwa ujumla. Kama Chidy Mkisu kapata teuzi. Tuliosoma miaka ile Ilala Boma mtakuwa mnamkumbuka. Alikuwa darasani hana akili. Anagezea mpaka analazimisha.ukikataa kumpa karatasi adese atakutukana sana baadaye.

Nakumbuka Jamaa alisaidiwa na wana kupata hata cheti cha degree ndani ya 2 days.. Elimu yake ilikomea fomu foo. Maana angalau hata angefika Form Four. amekuja lamba teuzi. Tulikuwa tunamwona hana akili kumbe anazo kaziweka tu mfukoni mbwa yule. Ametuingiza chaka sana. Leo hii anatumia LC 300 series. tunashiriki kumlipa mshahara na malupulupu lukuki.

Anyway.. nami nimegundua makosa yangu. Nimekosa mimi. Nimekosa sana. Nimekosa kila sehemu. Naenda renew kadi yangu. Sitaki tena kujifanya mjuaji.... Mbwa mie. Nitafuata ushauri wa wakubwa. Mama tena 2025 mpaka 2040. Akikataa tutamlazimisha. Apende asipende atake asitake atakuwa Rais. Kama si yeye basi angalau hata mwanaye au mjukuu wake.
 
Hahaha
 
Wahenga walisema "Ukila na kipofu usimshike mkono"

Ukifanikiwa tupasie na sie huku mkuu.
 
Uko vizuri Kaka. Wengi tumeponzwa na kutumia akili.
 
We kweli ni kilaza, sasa umeanza kumsema mwenzio badala ya kueleza yanayokuhusu wewe na kukosa teuzi.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚dah hiii hatari
 
Hata bundle likiisha data itasoma 5G
 
Unajua kufikisha ujumbe vzr.. kwa kuvaa uhusika. Oh sorry nimetumia tena akili agrrrrrh...โ˜น๏ธ๐Ÿคบ
 
Sijamuelewa mleta mada, aliyemuelewa anifahamishe.

Vijana wa JF wanasema , hizo "code" kwangu zimekuwa mtihani.
 
Mjini kuna code zake, ukijizima data ndio unapata connection
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ