sixlove
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 563
- 393
Habari wadau na wajasiliamali. Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, nataka nianze ufugaji pia wa hawa chotara. Naomba kuuliza ni baada ya muda gani naweza kuvitoa vifaranga nje vikashinda kisha jioni ndio viwe vinarudi bandani kulala. Lengo langu ni viwe vinapata hewa ya kutosha pia vijidudu na majani kwa ajili ya proteins. Maana kwa experience ya hawa wa kienyeji huwa nikiwaweka muda wote ndani( kuanzia siku moja mpaka wiki nane) nakutana na changamoto ya mafua sana, kuliko vikiwa vinashinda nje. Sasa sijajua kwa Sasso kwa ufugaji wa nje ndani NATAKIWA NIVITOE VIKIWA NA UMRI GANI? Asante