The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Jana usiku, majira ya saa mbili hivi, nilikuwa mahali nikibadilishana mawazo na washkaji, lakini bila kutarajia, nilijikuta macho yangu yakielekea angani ambapo yaliona kitu kilichotafsiriwa kichwani mwangu kuwa cha ajabu.
Kwanza, nilidhani ni msururu wa ndege zinazopita kwenye anga la kimataifa, lakini zikienda wapi na kwanini ziliongozana vile, sikuelewa na sikuwa na majibu. Sikuweza hata kubaini haraka ni nini, na ufahamu wangu ulikuwa challenged.
Nilipowaonesha wenzangu, tukaanza kujadili kama kile tulichokiona kilikuwa kitu cha asili au kilichotengenezwa na binadamu. Sote hatukuwa na majibu ya hakika. Tulikiangalia mpaka kilipotokomea. Hakukuwa na wingu angani ambalo labda lingekificha, ila inaonekana kilitoweka tu mwishoni mwa upeo wa macho yetu.
Hata hivyo, katika kujaribu kupata uelewa zaidi, leo asubuhi nimeonesha video hii iliyoambatanishwa hapa kwa baadhi ya watu wenye udadisi wa masuala ya teknolojia na anga. Ingawa si wataalamu, ni watu tu wanaopenda kujua mambo. Kabla sijamaliza sentensi, wakanieleza kuwa nilichokuwa nimekiona ni satelaiti za Starlink.
Baada ya kuperuzi mtandaoni, picha zilithibitisha kuwa tulichokiona angani jana usiku kilikuwa ni satelati za Starlink. Andiko moja linaeleza kuwa satelaiti hizo zikiwa angani zinaweza kuonekana kama vile ni mstari wa taa angavu. Na hiki ndo hasa nilichokiona.
Lakini pia, hii si mara ya kwanza kwa satelaiti hizo kuonekana katika anga la Tanzania. Mnamo Februari mwaka huu 2024, mdau mmoja alileta uzi jukwaani akiuliza juu ya kile alichokiona. Mdau mwingine naye alileta ufafanuzi wa kile kilichoulizwa.
Napenda kuamini kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kuonekana kwa vifaa hivyo katika anga. Je, ulibahatika kuiona?
Hii ni video niliyochukuwa ikionesha satelaiti za Starlink zikipita angani, hapa Dar es Salaam.
Hii ni picha ya kutoka mtandaoni ikionesha satelaiti ya Starlink ikiwa angani.