Sativa ashauriwe apunguze kuwadhihaki Polisi

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Naombeni niweke wazi, mimi sio askari wala siko upande wao!!

Najua maumivu anayoyapitia Edgar Mwalebela ( Sativa ) baada ya kutekwa na kunusurika kuuwawa mwaka huu.

Sasa jamaa yetu amekuwa akishambulia askari yoyote kwa lugha ngumu na kali.

Naomba ashauriwe apunguze kufanya hivyo, achague mbinu ya kudili na adui kimyakimya. Hii mbinu ya sasa inachafua taswira yake.
 
Vitani huchagui silaha. Mtu anusurike kufa afu uanze kumbwambia aseme hivi au vile, unaumwa?

Hawa kina Sativa, Lissu hata wakitoa matusi ya nguoni tuwaelewe tu wamepita bonde la uvuli wa mauti.
 
Waambie polisi waache dhihaka kwa Watanzania.

Sativa ameongea yote kuhusu jaribio lake la kuuawa na polisi.

Mnampuuza malalamiko yake, namuunga mkono awaseme mpaka muone haya
 
Unamaanisha hao wanaoteka raia mchana kweupe na kuwapoteza ?
 
Anahitaji daktari wa saikolojia ,hapo alipo ni sawa na nyati aliyejeruhiwa Kwa risasi akikutana na binadamu yoyote lazima amsambulie ili kujihamu,amepoteza Imani na polisi, pole yake
Vitani huchagui silaha. Mtu anusurike kufa afu uanze kumbwambia aseme hivi au vile, unaumwa?

Hawa kina Sativa, Lissu hata wakitoa matusi ya nguoni tuwaelewe tu wamepita bonde la uvuli wa mauti.
Hatari sana.Apatiwe msaada wa kisaikolojia.Amepitia uchungu mwingi kati ya dunia na motoni.
 
Anayechafua taswira ya mwenzake ni yupi, Polisi au yeye mhanga?

Huyo alishaga uawa na Polisi lakini Mungu ndiyo hakutaka.

Hana cha kupoteza.

Unapompiga mtu usimchagulie kiwango cha sauti ya kulia.
 
Waambie polisi waache dhihaka kwa Watanzania.

Sativa ameongea yote kuhusu jaribio lake la kuuawa na polisi.

Mnampuuza malalamiko yake, namuunga mkono awaseme mpaka muone haya
Yani hicho ndo kibaya.
Ameelezea kabisa vizuri na kuwatambua waliomteka lakini wote wanampuuza na kumuona hamnazo

Kimbilio pekee alilobaki nalo ni kutoa machungu yake mitandaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…