Hatari sanaYule ni facilitator namaanisha waliotembea nae kutoka Dar es Salaam , Arusha hadi Katavi.
Huyo mpumbavu mafwele atateka na kuua wangapi? Ebu aachane na ujinga ,tangu aanze kuteka na kuua ameachive nini? Amewamaliza wanaharakati? Ana miaka michache tu kufikia umri wa kustaafu.Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam (mbele ya Mheshimiwa Jaji D.D. Ndumbaro), imetoa hukumu tarehe 29 Septemba 2026 katika Rufaa ya Jinai Namba 000029293 ya mwaka 2025.
Sativa alikata rufaa kupinga uamuzi, mwenendo, na amri za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilizotolewa tarehe 28 Novemba 2025 (Kwenye Shauri dogo la Jinai Namba 000028115 la 2025).
Katika rufaa hiyo, Sativa aliwasilisha hoja 10 akipinga taratibu zilizotumika, masuala ya katiba, na mamlaka ya Mahakama ya Kisutu. Miongoni mwa hoja zake ni kuwa:
Baada ya kupitia hoja zote, Mahakama Kuu imebaini kuwa mwenendo wote wa mahakama ya Kisutu ulienda kinyume cha Kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), bila kuwa na mamlaka chini ya Sheria ya Urereshwaji wa Watuhumiwa (Extradition Act), na ulitegemea kiapo chenye kasoro zisizorekebishika. Kutokana na hayo, Mahakama Kuu imetoa amri zifuatazo:
- Mahakama ya chini iliendesha shauri upande mmoja (ex parte) bila kutoa sababu za msingi.
- Hakukabidhiwa wito wa Mahakama (summons) bila sababu yoyote halali.
- Na nyaraka iliyotumika kuomba amri hizo (affidavit) ilikuwa na kasoro kubwa za kisheria zilizofanya kiapo hicho kutokubalika.
Huu ni ushindi mwingine mkubwa wa kisheria unaoonyesha umuhimu wa kufuata misingi na taratibu za sheria kabla ya kutoa amri nzito kama za kukamata au kurejesha raia nchini.
- Mwenendo wote wa Shauri la Jinai Na. 000028115 la mwaka 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umefutwa (quashed).
- Uamuzi na amri zote zilizotolewa na Mahakama hiyo ya Kisutu tarehe 28 Novemba 2025 zimetenguliwa kikamilifu (set aside in their entirety).
- Hati ya kumkamata (warrant of arrest) na maagizo yote yaliyotolewa kwa ajili ya kumrejesha nchini (extradite) Edge Edson Mwakabela yametangazwa kuwa ni batili na hayana nguvu yoyote kisheria (null, void, and of no legal effect).
----
Tujikumbushe kilichotokea:
Mnamo tarehe 28 Novemba 2025, Jamhuri (kupitia ACP Wilson Mlowola) iliwasilisha maombi ya dharura (Chamber Summons Ex-Parte) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Application Na. 000028115 ya 2025).
Lengo la Jamhuri lilikuwa kupata:
Jamhuri ilidai kuwa Sativa anakabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uongo chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act, Cap 443). Mahakama ya Kisutu, siku hiyo hiyo, ikasikiliza maombi hayo bila Sativa kuwepo au kupewa taarifa (Ex-Parte) na kutoa amri ya kumkamata na kumrejesha nchini!
- Hati ya kumkamata Sativa mahali popote alipo.
- Amri ya kutumia taratibu zote za kisheria kumrejesha nchini (extradition) kutoka nchini Kenya.
Sativa, kupitia Wakili wake Jebra Kambole, alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi hayo kwa kutoa hoja 10 za kisheria na kikatiba.
Pingamizi la Jamhuri Kubutuliwa (Preliminary Objection)
Mwanzo kabla ya rufaa kusikilizwa, Mawakili wa Serikali (wakiongozwa na Debora Mushi) walileta pingamizi wakidai rufaa hiyo haikustahili kupokelewa kwa sababu amri ya kukamata ni ya muda (interlocutory order), hivyo haimalizi kesi kuu ya jinai.
Jaji Ndumbaro alitupilia mbali pingamizi hilo kwa kuonyesha makosa makubwa ya DPP.
Mahakama ilibaini kuwa:
Katika uchambuzi wa kina, Mahakama Kuu ilibaini udhaifu na ukiukwaji mkubwa wa sheria uliofanywa na Mahakama ya Kisutu na Ofisi ya DPP:
- Hakukuwa na kesi yoyote ya jinai iliyokuwa imesajiliwa au kufunguliwa rasmi Mahakamani dhidi ya Sativa! Jamhuri ilisukuma tu rasimu ya hati ya mashtaka (draft charge sheet) kama kiambatisho cha maombi.
- Kwa sababu hiyo, maombi ya Kisutu yalikuwa yamefunga jambo hilo rasmi, hivyo Sativa alikuwa na haki kamili ya kukata rufaa.
A. Kukosekana kwa Kesi ya Jinai Kabla ya Hati ya Kukamata (Kifungu 14(1) CPA)
Mahakama Kuu ilibainisha kuwa Kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kinamtaka Hakimu kufanya tathmini ya kina kabla ya kutoa hati ya arrest.
Hati ya kukamata inatolewa tu iwapo kuna kesi iliyofunguliwa na kusajiliwa rasmi ili mtuhumiwa akamatwe na kuja kujibu mashtaka. Kuomba amri ya arrest bila kuwa na kesi iliyosajiliwa mahakamani ni kinyume cha sheria.
B. Mahakama ya Kisutu Kuingilia Mamlaka Asiyo Nayo (Extradition Act)
Hakimu wa Kisutu alitoa amri kwa Vyombo vya Dola na Polisi wa nchi ya nje kumkamata na kumrejesha Sativa.
Mahakama Kuu ilifafanua kuwa:
C. Hati Kiapo (Affidavit) Iliyojaa Uharibifu Usiorekebishika
- Hakimu wa Tanzania hana mamlaka kisheria kuamuru Polisi au Mahakama za nchi ya kigeni kutekeleza hati ya arrest ya Tanzania.
- Mchakato wa kumrejesha mtuhumiwa (extradition) upo chini ya mamlaka ya Waziri mwenye dhamana na si amri ya moja kwa moja kutoka kwa Hakimu wa Mahakama ya Chini.
Hati kiapo iliyowasilishwa na ACP Wilson Mlowola ilikuwa na kasoro mbaya sana za kisheria:
1) Kukosa Tarehe kwenye Jurat: Sehemu ya Kiapo cha Kamishna wa Viapo iliachwa wazi bila kuwekwa tarehe na mwezi. Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu zilishatoa msimamo mara kadhaa kuwa ukosefu wa tarehe kwenye jurat unakausha nguvu zote za kiapo hicho kisheria (incurably defective).
Uongo na Mgongano wa Maelezo: Kiapo hicho kilidai kilihakiki 'Aya ya 10' wakati hati ilikuwa na aya 9 tu! Na zaidi, kiapo kilidai taarifa ya uchunguzi ilipokelewa tarehe 24 Novemba 2024, huku hati ya mashtaka ikidai kosa lilifanyika mwaka mmoja baadaye, yaani tarehe 22 Novemba 2025!
D. Kesi ya Dharura ya "Kutamkwa kwa Mdomo"
Jamhuri ilidai shauri hilo lilikuwa la dharura kwa kumwambia Hakimu kwa mdomo tu bila kuwa na Hati ya Dharura (Certificate of Urgency) iliyosajiliwa kwenye mfumo wa kielektroniki wa mahakama au kuwasilishwa kwa maandishi.
Shauri hili linatupa picha gani wananchi?
- Umuhimu wa Mawakili Wanaoijua Sheria: Hoja ndogo za kiufundi kama vile jurat kukosa tarehe au maombi kuwasilishwa bila kesi msingi zimeokoa haki za raia.
- Ushindani wa Dola na Sheria: Inaonyesha namna vyombo vya Dola wakati mwingine vinavyotumia "short-cuts" au kuikimbiza Mahakama kutoa amri nzito bila kufuata misingi ya sheria na Katiba.
- Mustakabali wa Mhimili wa Mahakama: Uamuzi huu wa Jaji D.D. Ndumbaro unairudishia jamii imani kuwa Mahakama Kuu inaweza kusimama kama mlinzi wa mwisho wa haki pale mahakama za chini zinapopotoka au kushawishiwa kufanya maamuzi kwa haraka bila umakini.
MafweleAkitekwa tumshukuru nani.?
TanzLII is operated by the Judiciary of Tanzania and the Office of the Attorney General, Chief Parliamentary Draftsman, and publishes the law of Tanzania for
Kwa Sasa hawaweziIpo siku watamchukua tu
Wale Huwa hukumu zao za kupigiwa simu.KATIKA MAHAKAMA INAYOTIA DOA MAHAKAMA ZA TZ NI MAHAKAMA YA KISUTU...INAENDESHWA KIHUNI SANA
Labda mahakama ya rufaa maana kama alisema 'mahakama hii haiangalii uzito wa ushahidi wala kuaminika kwake'.Kazi nzuri kwa Mahakama Kuu Tanzania(Tanganyika), naamini wakina Jaji Ndunguru et al, na wao watafanyakazi tukuka, kama mwenzao wakiongozwa na Katiba,Sheria, Kanuni, marejeo ya kesi mbalimbali, Uzoefu, busara na weledi wao
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta mwenendo wa kesi uliokuwa ukihusu ombi la kumkamata na kurejesha nchini Edgar S/O Edson Mwakabela maarufu Sativa, baada ya kubaini dosari za kisheria katika mchakato huo.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dafina Ndumbaro tarehe 29 Septemba 2026, katika Rufaa ya Jinai Na. 29293 ya mwaka 2025, iliyowasilishwa na Mwakabela kupinga uamuzi na amri zilizotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Novemba 28, 2025.
Kwa mujibu wa maelezo ya uamuzi huo, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliwasilisha ombi mahakamani likitegemea kiapo cha polisi, ikidai Mwakabela alichapisha taarifa za uongo mtandaoni, jambo lililotajwa kuwa ni kosa chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao, na kwamba alikuwa akiishi nchini Kenya.
Mahakama Kuu imebaini kuwa hakukuwa na kesi ya jinai iliyosajiliwa mahakamani, huku hati ya mashtaka ikiwa imeambatanishwa tu kwenye nyaraka za maombi bila kusajiliwa rasmi.
Mahakama pia imeeleza kuwa mahakama ya chini ilizidi mamlaka yake kwa kutoa maelekezo yanayohusu polisi au mamlaka za Kenya, ikieleza kuwa mchakato wa kumrejesha mtu kutoka nchi nyingine una taratibu zake za kisheria na uamuzi wa mwisho kuhusu kumkabidhi mtu unahusisha mamlaka husika, si hakimu.
Aidha, Mahakama Kuu imebaini dosari kubwa katika kiapo cha polisi, ikiwemo tarehe ya kuapishwa kuachwa wazi na kutajwa kwa “paragraph 10” ambayo haikuwepo kwenye hati hiyo. Mahakama ikaeleza kuwa amri iliyojengwa juu ya nyaraka yenye dosari hizo haina uhalali wa kisheria.
Mahakama haikukubaliana na hoja kwamba kusikilizwa kwa upande mmoja pekee kulifanya uamuzi huo kuwa batili, ikieleza kuwa maombi ya aina hiyo yanaweza kusikilizwa upande mmoja.
Hata hivyo, katika matokeo ya mwisho, mwenendo wote wa Mahakama ya Kisutu ulifutwa, huku amri zilizotolewa Novemba 28, 2025 zikitangazwa kuwa batili na zisizo na nguvu za kisheria.
Hivyo, kwa mujibu wa uamuzi huo, hakuna amri halali ya mahakama katika shauri hilo inayomtaka Edgar Mwakabela kukamatwa au kurejeshwa nchini Tanzania.
View attachment 3681281
View attachment 3681283View attachment 3681284
Kuna mahakimu wengine walikwenda shule kusomea ujinga. Kesi ya extradition hufunguliwa mahali aliko fugitive anayelengwa! Serikali yetu imejaa wahalifu tu.Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam (mbele ya Mheshimiwa Jaji D.D. Ndumbaro), imetoa hukumu tarehe 29 Septemba 2026 katika Rufaa ya Jinai Namba 000029293 ya mwaka 2025.