SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa

Tukifa tutajibu nini kwa MUUMBA?.
Haya maisha ni zawadi tu tumepewa kwa kitambo kidogo.

Mambo ya dunia yasitufanye kusahau kuwa sisi ni kama ua huchanua na kupendeza ila mwisho hunyauka
 
kama alikua akitumia lugha za matusi mtandaoni huwenda akawa ni mwananchi mwenye hasira kali kamfanyia hayo yote
Mwananchi ampeleke Karakana ya Polisi Oesterbay hiyo Access mwananchi wa Kawaida anaitoa wapi??

Na bado asubuhi amchukue ampeleke Arusha ampeleke katavi pia akampige risasi???

Mwananchi wa Kawaida?? Really??
 
kama alikua akitumia lugha za matusi mtandaoni huwenda akawa ni mwananchi mwenye hasira kali kamfanyia hayo yote
Naona umekosa hata jinsi ya kuitetea serikali yako unasingizia mwananchi mwenye hasira kali

Na sisi tunahitaji kumuona huyo mwananchi mwenye hasira kali alie na uwezo wa kumteka mtu na kumpeleka kwenye karakana ya jeshi la polisi kisha kumsafirisha hadi Arusha kisha Katavi na kumpiga risasi ya kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…