Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu Salama,

Sativa amekuwa akitafutwa toka weekend (Jumapili - 23/6/2024), baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

sativ.jpg

Edga Mwakabela (Sativa)

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata mmojawapo wa viongozi wa ACT Wazalendo Rahma Mwita alizungumza suala hili kwenye kwenye XSpaces jana 26/6/2024 kuwa yupo tayari kujitolea muda wake kuambatana na ndugu wa kijana huyo kwenda kwenye vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia kupaza sauti kuhusu kupotea kwa kijana huyu.

Edgar anaishi Mbezi kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.

Kama kelele zisingepigwa huyu ndio ilikuwa ntolee, halafu kuna chawa wanaotetea ujinga kila siku.

Kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera kuhusu kuwapoteza watu soma hapa: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Aisee, wakati wa kubadilika ni sasa, mtu akipotea wote tupige kelele, serikali ikienda kushoto wote tupige kelele. Isiwe kazi ya wanaharakati wachache au watetezi wa haki za binadamu, peke yao hawawezi. Tukiungana wote tunakuwa na nguvu.

Tuendeleze hashtag Wakuu, #KataaMachawa #KataaUozo2025, amsha kila utakayeweza kumuasha, tushikamane na kuteteana wakati wote kuleta uwajibikaji nchini.

PIA SOMA
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Wakuu Salama,

Sativa amekuwa anatafutwa toka weekend, baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata ACT walizungumza kuhusu hili.

Amepatikana akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.
yaani mtu hata akwa na matatizo yake binafsi mnasema mkosoaji katekwa sasa dawa ya hii kitu ajitokeze hazarani aseme alikuwa wapi na aliambiwa nini huko ili tujuwe kama kweli alitekwa sababu ya ukosoaji bila hivyo huyo ni mharifu tu kama wahalifu wengine
 
Sasa mtu yupo hoi kiafya lakini badala ya kusaidiwa anahojiwa kama mtu mwenye afya...
 
Wakuu Salama,

Sativa amekuwa anatafutwa toka weekend, baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata ACT walizungumza kuhusu hili.

Amepatikana akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.

Dunia ya sasa hovyo sana, mtu kaumia badala yakumpa msaada wa dharura alafu ndio ahojiwe baadae akiwa mzima, hivi kwanini watu weuzi huwa hawawezi kujifunza vitu vidogo hata kwawatu weupe?
 
yaani mtu hata akwa na matatizo yake binafsi mnasema mkosoaji katekwa sasa dawa ya hii kitu ajitokeze hazarani aseme alikuwa wapi na aliambiwa nini huko ili tujuwe kama kweli alitekwa sababu ya ukosoaji bila hivyo huyo ni mharifu tu kama wahalifu wengine
wakitokaga huko huwa hawasemi, wanakimbia tu nchi!ref Dr Ulimboka na Roma Mkatoliki!aliesema ni Mdude tu
 
Back
Top Bottom