GE2025 SAU watupia lawama INEC kwa dosari za uratibu wa ratiba za kampeni

GE2025 SAU watupia lawama INEC kwa dosari za uratibu wa ratiba za kampeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mgombea urais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara ameilalamikia Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) akidai kuwepo kwa changamoto katika uratibu wa ratiba za kampeni, jambo linalosababisha mkanganyiko na migongano katika maeneo ya mikutano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 17, 2025 Mjini Moshi, Kyara amesema katika kipindi cha kuelekea mwisho wa kampeni, umakini unahitajika zaidi ili kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini.

Akijibu malalamiko hayo,msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Vunjo na Moshi vijijini, Lucas Msele, amethibitisha kupokea malalamiko hayo lakini akasema kwa mujibu wa ratiba ya INEC, mgombea huyo hakuwa na ratiba ya mkutano katika Jimbo la Vunjo kwa siku ya leo.

 
Back
Top Bottom